Tafuta

Papa amemteua Padre Henry Juma Odonya kuwa Askofu wa Jimbo la Kitale, nchini Kenya Papa amemteua Padre Henry Juma Odonya kuwa Askofu wa Jimbo la Kitale, nchini Kenya 

Papa amemteua Padre Henry Juma Odonya kuwa Askofu wa Jimbo la Kitale,Kenya

Jimbo katoliki la Kitale nchini Kenyealimempata Askofu Mpya,Padre Henry Juma Odonya mara baada ya Askofu Maurice Anthony Crowley,S.P.S kung’atuka kwenye shughuli za kichungaji kutokana na umri.Padre Henry Odonya alizaliwa mnamo mwaka 1976 na alipewa daraja la Upadre mnamo mwaka 2006.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ijumaa tarehe 4 Novemba 2022, Baba Mtakatifu Francisko amekubali maombi ya kung'atuka kutoka katika shughuli za kichungaji kwa jimbo la Kitale nchini Kenya yaliyo wakilishwa na Askofu Maurice Anthony Crowley, S.P.S. na wakati huo huo Baba Mtakatifu akamteua Askofu wa jimbo hilo hilo mweshimiwa sana  Padre Henry Juma Odonya, wa Eldoret, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mfundaji katika Nyumba ya Malezi ya Shirika la Mtakatifu Patrizio katika Utume wa Nje nchini Afrika Kusini.

Wasifu wa Padre Henry Juma Odonya,   alizaliwa tarehe 10 Desemba 1976 jijini Nairobi. Alijifunza Falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Agostino Mbaga na Taalimu Mungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Thomas wa Aquinas jijini Nairobi Kenya. Alipewa daraja la ukuhani mnamo tarehe 25 Februari 2006 kwa ajili ya Jimbo la Eldoret.

Padre Odonya aliweza kufunika majukumu yake pamoja na masomo kama ifuatavyo; msaidizi wa Parokia ya Kapcherop (2006-2008) na ya  Ndalat, zote katika jimbo la  Eldoret (2008-2009); Paroko wa  Kapcherop (2009-2011) na  Kolongolo, Jimbo la  Kitale, kama kuhani wa fidei donum (2011-2013); Rais wa Chama cha Mapadre wa fidei donum nchini Kenya (2011-2014); Paroki wa Chepchoina, Jimbo la Kitale (2013-2015), la Ndalat na Mwenyekiti wa Chama cha Mapadre wa kijimbo (2015-2016;  aliendelea na masomo jijini Roma katika masomo ya Iutume wa Kimisionari {Missiology} katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana (2016-2019); Makamu  Oaroko wa Parokia ya Huruma, Jimbo la  Eldoret (2019-2020); Tangu 2020 ni mfundani katika Nyumba ya Malezo ya Shirika la Mtakatifu Patriozi kwa ajili ya Utume wa Nchi za Nje {Fidei donum}huko Afrika Kusini.

Papa ameteua Padre Henry Juma Odonya kuwa Askofu wa Kitale Kenya
04 November 2022, 12:00