Tafuta

2022.11.10 Papa na Mfalme  Abdullah II Ibn Al Hussein wa Yordan 2022.11.10 Papa na Mfalme Abdullah II Ibn Al Hussein wa Yordan 

Papa amekutana na Mfalme Abdullah II bin Al Hussein wa Yordan

Alhamaisi 10 Novemba 2022 Papa amekutana na Mfalme Abdullah II wa Yordan ambapo mara baada ya mkutano huo amekutana tena na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya mahusiano na ushirikiano na Mataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 10 Novemba 2022 amekutana katika Jumba la Kitume na Mfalme Abdullah II wa Yordan ambapo mara baada ya mkutano huo amekutana tena na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na mashirika ya Kimataifa. Katika mazungumzo yao na Katibu wa Vatican kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican wameonesha uwepo wa mahusiano yao mazuri na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuongeza mazungumzo ya kidini na kiekumene, kwa kuhakikisha daima kwamba Kanisa Katoliki huko Yordan  linaweza kuendelea kuwa huru katika  utume wake.

Papa amekutana na Mfalme wa Yordani
Papa amekutana na Mfalme wa Yordani

Wakiendelea na mazungumzo hayo  aidha wameweka  wazi juu ya umuhimu wa kuhamasisha msimamo  wa amani katika Nchi za Mashariki ya Kati, hasa katika masuala ya kipalestina na mada ya wakimbizi, ambapo wamesema ulazima wa kulinda na kutia moyo uwepo wa wakristo katika Kanda hiyo. Katika mapendekezo hayo wamebainisha juu ya ulazima wa kuendelea kuhifadhi sura ya usawa wa Maeneo matakatifu ya Yerusalemu, ambayo ni maeneo ya kukutana kama  alama ya kuishi kwa amani ambamo  ukuzaji wa kuheshimiana na mazungumzo ya kweli yanapatikana.

10 November 2022, 16:11