Tafuta

Maria Carola Cecchin (zamani Fiorina), Mwanashirika wa Watawa wa Mtakatifu Giuseppe Benedetto Cottolengo alitangazwa Mwenheri tarehe 5 Novemba 2022 huko Meru Kenya Maria Carola Cecchin (zamani Fiorina), Mwanashirika wa Watawa wa Mtakatifu Giuseppe Benedetto Cottolengo alitangazwa Mwenheri tarehe 5 Novemba 2022 huko Meru Kenya 

Mwenyeheri Sr. Cecchin,mama mwema kwa maisha ya watu wa Kenya

Novemba,5 alitangazwa mwenyeheri Sr.Maria Carola Cecchin,"mama mwema".Maisha yake yote aliyatoa katika huduma ya watu wa Kenya.Mtawa huyo, alizaliwa Padua,nchini Italia na mwanashirika wa Mtakatifu Guseppe Cottolengo.Kwa njia ya maombezi yake,mtoto aliyezaliwa bila dalili za maisha alirejea kwenye uhai.Sherehe zilifanyika Meru nchini Kenya.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Sista Maria Carola Cecchin wa Shirika la watawa wa Mtakatifu Joseph Benedetto Cottolengo, ambaye alitangazwa kuwa mwenyeheri, Jumamosi asubuhi tarehe 5 Novemba 2022 nchini Kenya, ni katika nchi aliyohudumu kwa miaka ishirini. Kumbukumbu na upendo kwa jamii hivyo haikuweza kupotea  hata  wakati wa tukio kwenye uwanja wa Kinoru katika mji wa Meru, zilipofanyika sherehe za kutangazwa kuwa Mwenyeheri, iliyoongozwa na Kardinali Antoine Kambanda, Askofu Mkuu wa Kigali nchini (Rwanda), ambapo wawakilishi kutoka Laghi pia walikuwapo waliosindikizwa na paroko, Padre  Attilio De Battisti, kuwakilisha jimbo kuu la Padua na hasa parokia ya asili ya mwenyeheri mpya na Padre wa  Cittadella, ambapo mnamo Oktoba mwaka huu alikuwa mwenyeji wa hija ya wanafamilia wa mtawa huyo wa Cottolengo, wakitembelea kwa mara ya kwanza mji wa nyumbani kwa mwenyeheri mpya.

Washiriki wa misa ya kutangaza mwenyeheri kutoka maeneo mbali mbali ya dunia

Wengine walioshiriki misa hiyo ni askofu wa Meru, nchini Kenya Askofu Salesius Mugambi,  Padre Daniel K. Rono, katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kenya, Askofu Mkuu Hubertus Matheus Maria van Megen, Balozi wa Vatican  nchini Kenya, mwanashirika Antonio Crameri, wa Cottolengo, ambaye ni Mswisi kutoka Canton Ticino na askofu wa Vicariate ya kitume ya Esmeraldas nchini Ecuador, Mkuu wa Shirika  wa Nyumba Ndogo ya Maongozi ya Mungu, Padre Carmine Arice na mapadre na maaskofu wengine wengi, waamini. Pia walioshiriki ni Rais wa Jamhuri ya Kenya Bwana William Ruto, Balozi wa Italia nchini Kenya Bwana Roberto Natali, wawakilishi wa taasisi za ndani, mjukuu wa Mwenyeheri Alessandro Cecchin na uwakilishi wa watawa wa Cottolengo kutoka jumuiya za Afrika, Amerika, Asia na Ulaya na Mama Mkuu wa Shirika Sr.  Elda Pezzuto, ambaye alitoa shukrani.

Kardinali Kambanda: Sr Checchin aliiga tendo bora la upendo

Kardinali Kambanda  Kama mwakilishi wa Baba Mtakatifu katika tukio hilo katika mahubiri yake alisisitiza kwamba, mtawa huyo ambaye ni wa  shirika  lilioanzishwa na  Mtakatifu Joseph Cottolengo, aliwakilisha utakatifu wa wamisionari wengi sana ambao wamekubali kuvumilia kila aina ya sadaka na hatari ili kuleta wokovu wa Mungu kwetu. Alijitolea maisha yake nchini Kenya” kwa ajili ya huduma yake kwa watu wa Mungu jimboni Meru kwa miongo miwili. Sr. Cecchin aliiga tendo bora zaidi la upendo ambalo linaweza kufanywa ili kufanya upendo wa Kristo ujulikane kwa wengine, alisisitiza askofu mkuu wa Kigali. Kwa hakika, alitumia maisha yake ya umishonari, ili ufalme wa Mungu uenee pia nchini Kenya na jina la Mungu lihimidiwe katika nchi hii”. Kardinali huyo alikumbuka kwamba mtawa huyo alikuwa na “tumaini kamili katika utunzaji wa upendo wa Mungu na alikuja katika nchi hii kushuhudia, ili nasi tuweze kupata imani na imani ile ile ambayo hutuweka huru na hofu zote na kutuita katika uaminifu kwa Mungu”.

Mwaliko wa kuona wenyeheri kielelezo cha bidii ya umisionari

Kardinali Kambanda aliwaalika waamini kuona katika wenyeheri  kielelezo cha bidii ya umisionari kinachostahili kuigwa kwani  Sr. Maria Carola, alisema aliwapatia mfano wa kufuata wakati wa maisha ya kila mtu  na hivyo ni juu yao kuendeleza maisha haya ya umisionari katika ulimwengu wa leo, unaohitajika zaidi. Askofu mkuu wa Kigali  pia alisema kwamba Sr  Cecchin alitumia maisha yake katika nchi hiyo akitoa heshima kubwa kwa Mungu na kwa Kanisa. Alimpenda “Bwana sana hivi kwamba alitamani kuwa mikono yake, kuwafikia maskini. Alimwamini sana hivi kwamba alikubali ugumu na majaribu yote ambayo maisha yamemhifadhi. Naye akafanya upendo wake huo wa kiinjili unaotusukuma tusitafute faida yetu wenyewe, bali kujitoa kabisa, tukijisahau ili kukumbatia wema wa wengine. Sr. Maria Carola aliishi kama hivyo: kwa Mungu kabisa, aliyejitolea kabisa kwa maskini. Familia ni moja wapo ya taasisi ambazo mfano wa Mwenyeheri Maria Carola unaweza kutumika na akionya juu ya hitaji la kukomboa familia kutoka kwa kile alichokiita upendo wa uwongo na kuomba, kinyume chake, upendo wa kweli ndani ya familia kutokana na ushuhuda wa kujitolea wa mtawa huyo.

Muujiza wa uponyaji wa mtoto

Kutangazwa kuwa mwenyeheri kumefikia hatima yake mara baada ya  miaka miwili ya kutambuliwa fadhila za kishujaa za mtumishi wa Mungu Maria Carola Cecchin mnamo tarehe 23 Novemba 2020 na chini ya mwaka mmoja baada ya kukubaliwa rasimi mnamo tarehe 13 Desemba 2021 kuhusu muujiza uliohusishwa na maombezi ya  Sr. Cecchin kwa  mtoto, aliyezaliwa bila ishara yoyote ya uhai mnamo tarehe 14  Aprili 2013 akiwa ndani ya gari kando ya njia iliyokuwa ikielekea Matiri nchini Kenya na akafufuka kimuujiza baada ya sala ya dhati ya mtawa mwingine, Sista Katherine, kwa Sista Maria Carola Cecchin.

Kujiunga na Shirika la Wakotolengo 1896

Fiorina, kama alivyokuwa anaitwa hapo awali, alikuwa ni mtoto wa tano kati ya watoto wanane, ambaye alizaliwa mnamo tarehe 3 Aprili 1877 huko Laghi ya Cittadella, Jimbo kuu katoliki la Padua italia,   na tangu akiwa na umri mdogo sana alihisi wito wa kujiweka wakfu kwa Mungu na mnamo tarehe 27 Agosti 1896, akiwa na umri wa miaka 19 alijiunga katika Nyumba Ndogo ya Maongozi ya Kimungu huko Torino Italia ambapo mnamo tarehe 2 Oktoba 1897, alianza unovisi kwa kutumia jina la Sista Maria Carola. Mnamo tarehe 6 Januari 1899 aliweka nadhiri zake za kitawa. Katika wito wake kulikuwa na shauku kubwa ya kujitoa, kumpenda Mungu na roho na kuishi kikamilifu karama ya Cottolengo.Mnamo tarehe 28 Januari 1905, Sr huyo aliondoka kwenda Barani Afrika, pamoja na sista mwengine   na wamisionari wawili wa Consolata.

Alifuata kauli mbiu ya mwanzishi kuwa Upendo wa Kristo unatusukuma

Kwa Sr. Maria Carola kilikuwa kipindi cha kuzaa matunda kwani alitumwa kwanza huko Limuru, baadaye Tuthu, ambako alifundisha katekisimu na kutembelea wagonjwa vijijini, kisha aliteuliwa kuwa mkuu wa nyumba huko Iciagaki, Mugoiri, Wambogo. Akiwa hapo aliweze kuishi maisha ya ajabu, ambapo ilikuwa  wakati wa Vita vya Kwanza vya Kidunia, kwa kuongozwa na kauli mbiu ya Cottolengo ambayo ni Caritas Christi urget nos! Upendo wa Kristo unatusukuma na hatimaye alikwenda huko Tigania-Meru ambayo ilikuwa ndiyo kituo chake cha mwisho. Katika maandishi kuhusu fadhia zake za kishujaa , yanabainishwa kwamba walimwita mama mwema na uwepo wake kwa watawa na wamisionari ulikuwa unaleta amani. Kwa maana hiyo hakuweza kurudi tena Italia, akiwa mgonjwa sana, akafa kwenye meli iliyokuwa ikimrudisha nyumbani kwake, mnamo  tarehe 25 Oktoba 1925.

Mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwenye mawimbi ya bahari ya shamu

Na mwili wake, kwa sababu ya maagizo ya usafi, ulikabidhiwa kwenye mawimbi ya Bahari Shamu. Mwanamke mwenye busara na mwenye hekima, lakini mwenye bidii na mwenye huruma, alikuwa akirudia Na bônamort a pagràtut yaani Kifo kizuri kitalipa kila kitu. Kwa sababu kila kitu ni kwa ajili ya Mbingu katika maisha ya Sr. Maria Carola, ambaye bila kuchoka alitoa ushuhuda wa upendo wa Mungu kwa maskini zaidi ya maskini huku akitoa pamoja na huduma za haraka sana, upendo mkuu zaidi wa tangazo la Yesu, Mwokozi wa pekee wa dunia.

Mwenyeheri mpya Sr. Maria Carola Cecchin,huko Meru Kenya

imesasishwa tarehe 9 Novemba 2022.

08 November 2022, 17:05