Vatican katika harakati za msaada wa tume za kulinda amani na wakimbizi wa Kipalestina
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Amani sio tu kutokuwepo kwa vita na inaweza kupatikana kwa njia ya haki na kwa njia ya mazungumzo,tu, kutafuta upatanisho na maendeleo ya pande zote. Katika sura hiyo kwa kunukuu kifungu cha Mtaguso wa Piili wa Vatican cha Gaudium et spes, Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa, alitayarisha jukumu la ujumbe kuhusu kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na kwa ajili ya wakimbizi wa kipalestina katika hotuba kwa ajili ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mada hiyo aliyotoa Jijini New York Marekani tarehe 7 Novemba 2022.
Lengo la operesheni ni ulinzi wa raia katika maeneo ya migogoro
Katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mada ya opereshi ya amani na wakimbizi wa kipaletina, Askofu Mkuu Caccia alisema operesheni za ulinzi wa amani ni ishara ya matumaini kwa sababu ni kwa kazi ya pamoja tu ndipo mataifa yanaweza kuondokana na kutojali kwa kimataifa. Lengo kuu la operesheni hizi ni ulinzi wa raia, kama ilivyoombwa na mataifa mwenyeji, lakini ambayo mara nyingi hayana njia au nia ya kisiasa ya kuidhamini. Ni kwa njia hii tu operesheni itakuwa na uhalali na uaminifu unaohitajika kukubaliwa na watu. Zaidi ya hayo, mbegu za amani zinaweza kukua tu pale ambapo historia ya mtu inaweza kustawi na kwa sababu hiyo Vatican, linasisitiza vyema kwamba shughuli nyingi za ulinzi wa amani zina kipengele maalumu katika kuheshimu haki za binadamu. Juhudi za kuzuia na kutokomeza matukio ya unyanyasaji wa kingono na unyonyaji ambayo yametokea katika baadhi ya matukio huko nyuma pia yanalizingatiwa. Kwa sababu hiyo alisema ukiukaji hu, "sio tu kwamba unakiuka utu wa binadamu kwa wathirika, lakini pia hupunguza uaminifu kati ya tume na wakazi wa eneo mahalia wanaohudumiwa.
Wasiwasi kuhusu ukosefu wa fedha katika UNRWA
Katika hotuba nyingine kwenye mkutano mkuu, Vatican ilieleza kuunga mkono shirika la Umoja wa Mataifa linalosaidia wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Kati UNRWA, ,hasa kuhusu mchango katika elimu ya vijana wakimbizi. Askofu Mkuu Caccia alionesha hata hivyo wasiwasi wake juu ya ukosefu mkubwa na unaoongezeka wa fedha kutoka kwa wakala, ambao unatishia kukata misaada kwa wale walio katika mazingira magumu zaidi. Ukosefu wa fedha, zaidi ya hayo, huongeza umaskini miongoni mwa wakimbizi wa Kipalestina, na hivyo kukuza kukata tamaa ambayo inaweza kusababisha matukio ya vurugu, alisema.
Salamu za rambirambi kwa mwandishi wa habari wa Palestina aliyeuawa
Kwa hakika, Vatican pia ilonesha masikitiko yake katika kuongezeka kwa ghasia huko Palestina na Israel na matokeo yake kupoteza maisha ya binadamu. Hasa, mateso yalioneshwa juu ya kifo cha mwandishi wa habari wa Kikatoliki Shireen Abu Aqleh mwezi Mei iliyopita mwaka huu, pamoja na matumaini kwamba kwa kuleta nuru ya ukweli juu ya kifo chake, familia yake na wale walio karibu naye watapata kitulizo fulani. Matumaini ya Mwakilishi wa Vatican ni kwamba viongozi wa Israel na Palestina wanaweza kusikilizana kwa umakini na heshima, wakishiriki mazungumzo na kuelewana. Vile vile Vatica ilisisitizia umuhimu wa kutafuta suluhisho la mji mtakatifu wa Yerusalemu, likiomba kuwekewa sheria maalum, iliyohakikishwa kimataifa ambapo matakwa mbalimbali yanatungwa kwa upatano na uthabiti, kwa namna ambayo hakuna chama kinachoweza kupuuza haki za wengine.