2022.11.22 La gioia  ni kitabu  kuhusu horuba, mahubiri ya Papa Francisko ambayo yanaeleleza mada ya Furaha 2022.11.22 La gioia ni kitabu kuhusu horuba, mahubiri ya Papa Francisko ambayo yanaeleleza mada ya Furaha  

Kitabu kipya 'Furaha',ni mada pendwa katika hotuba za Papa Francisko!

Katika takriban miaka kumi ya upapa,Papa Francisko amejikita mara kadhaa kuzungumzia juu ya mada muhimu ambayo sasa inazaa kitabu kiitwacho 'Furaha',ambacho kinakusanya hotuba zake kuhusu fundisho hilo.Utangulizi wa kitabu hicho umetiwa saini na Monsinyo Dario Edoardo Viganò:“Si matumaini rahisi,bali ni uwezo wa kutazama historia kupitia macho ya Mungu”.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Karibu miaka 10 ya Upapa wa Francisko, amekuwa akijikita mara nyingi kuhusu suala la kufikia utunzi wa Kitabu “Furaha, ambacho kimehaririwa na kuchapishwa na Elledici na Duka la Vitabu  Vatican, ambacho kinakusanya hotuba zake mbalimbali kuhusu fundisho  hilo. Kwa maana hiyo Monsinyo Dario Edoardo Viganò, makamu Kansela wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi na Sayansi ya Jamii, katika maoni yake kuhusu kitabu kiitwacho 'Furaha' ambacho alitia saini ya utangulizi wake ameandika kuwa “Furaha ya mwamini sio ujinga au kutoweza kuona shida za historia”.  Maandishi aaliyotamani Papa, ambayo yanakusanya hotuba zakejuu ya mada hiyo  yaliyochukuliwa kutoka kwa hati za upapa, mahubiri, hotuba na ujumbe kwa lengo la kumpatia msomaji fursa ya kuanza safari yake binafsi. Kwa maana hiyo sio kitabu kinachoweza kusomwa kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho, lakini kinaweza kusomwa kwa njia isiyo na mpangilio,” alieleza monsinyo Viganò. Kwa hakika haya ni maandiko ambayo, hasa wakati huu wa maneno ya kupiga kelele, habari za kutisha na vifo, huruhusu mtu kupanua moyo, kuinua macho yake na kurekebisha tena uzoefu wa waamini.

Kanisa ni mang’amuzi ya watu wanaoishi kwa furaha, likitualika kutafakari uzoefu wa Harusi ya Kana. Simulizi  wa muujiza wa kwanza wa Yesu una ndoa katikati, ambayo, hata hivyo, kipengele muhimu kinakosekana, yaani divai ambayo ni ishara ya furaha. “Mitungi ya utakaso haina kitu,”. Na hii ndiyo ishara ya uhusiano wa upendo uliokamilika sasa kati ya Mungu na watu wake. Hata sheria na utakaso hauwezi kurejesha shauku ya uhusiano huo. Hii ndiyo sababu Yesu hayupo, lakini amealikwa. Kwa hakika, ni Kristo ndiye anayeleta divai mpya, hivyo kuidhinisha agano jipya, la milele, la mwisho na la uhakika. Muungano ambao ulizaliwa kwenye muujiza huu mkubwa wa kwanza wa divai na ambao ni wa furaha. Hii ndiyo sababu kwa Padre  Dario  amethibitisha kuwa “Kanisa ni watu wa wanaume na wanawake ambao hawaishi chini ya Sheria, lakini wanaoishi katika furaha ya kuwa wana na binti za Mungu”.

Karama ya ubatizo inatuwezesha kupokea uzima wa Mungu, hivyo kuwa watoto katika mwanawe Yesu. Na hii inatufanya tuwe na uwezo wa kuishi mahusiano, katika uhusiano na ulimwengu au uumbaji, katika njia ya Bwana. "Kipaumbele kwa hiyo si ubinafasi, lakini juu ya mengine yote, kama ilivyo kwa Mungu, ambaye kipaumbele chake kimekuwa mwana. Tofauti na kile kinachotokea kwa mwizi aliyesulubishwa pale Kalvari, ambaye katika tukio hilo alimwambia Yesu: 'Ikiwa wewe kweli ni Mwana wa Mungu, jiokoe mwenyewe, kisha uniokoe mimi pia.' "Ikiwa hutaishi uwana wako katika Mungu, mahusiano yatakuwa muhimu tu na kazi, wakati kwa njia hii furaha ya kuishi ina maana ya kuhisi uharaka wa kuishi katika njia ya Mungu.

Ili kuwezesha usomaji, kitabu imegawanywa katika maeneo matatu ya mada, au tuseme, njia tatu za kufikiria furaha, ambazo zimeainishwa kuanzia vitenzi vitatu: 'kuwa', au kitambulisho cha furaha kinachoeleweka kama mtazamo wa kibinafsi na kiroho; 'kushiriki', ambayo ni furaha ya kujitolea kijamii na urafiki; ‘kutoa ushahidi’, yaani, furaha ya kuishi katika njia ya Mungu.” “Kusoma kitabu hicho  ni sawa na kutembea kwenye kurasa, kwa njia sawa na wanafunzi wa Emau” alibanisha Monsinyo Vigano. Katika kifungu hiki cha Injili, wanafunzi wanamtambua Yesu wakati wa kuumega mkate tu, lakini wanajiuliza: 'Je, labda haifiki mioyo yetu wakati anazungumza nasi?'. "Roho Mtakatifu anatanguliza mwanamume na mwanamke kumtambua Bwana katika ishara ya kugawana mkate, lakini anafanya kazi kwanza, hata tunapotembea na mtu ambaye hajulikani".

Kitabu kiitwacho FURAHA mkusanyiko wa maelezo juu ya furaha kutoka kwa Papa Francisko
24 November 2022, 16:01