Kard.Tagle,hati ya Papa katika mchakato wa unyenyekevu na utambuzi
Na Angella Rwezaula, – Vatican.
Matokeo ya utafiti makini na wa kujitegemea ambao hauhusu kesi za unyanyasaji wa kijinsia au matumizi mabaya ya fedha, lakini ambayo ina maana ya kuwa na wito wa kutembea kwa unyenyekevu na Mungu na mchakato wa utambuzi. Ndio maneno ya Kadinali Luis Antonio Tagle, rais hadi sasa wa Caritas Internationalis, alivyo wasilisha Hati ya Papa kuhusu shirika la Kimataifa iliyochapishwa Jumanne tarehe 22 Novemba 2022 . Kadinali Tagle aliisoma kikamilifu kwa lugha ya Kiingereza kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kiungo hicho uliofunguliwa tarehe 21 na kufungwa 22 Novemba 2022 katika ukumbi wa Aurelia mjini Roma, ambapo washiriki walikaribisha baadhi ya vifungu vya usomaji wa kifungu hicho kwa makofi. Pia walimpongeza wakati kadinali huyo alipokuwa akimkaribisha kamishna mpya Pier Francesco Pinelli, ambaye tayari ni mshauri katika sekta nyingi za usimamizi na fedha za Caritas, na Maria Amparo Alonso Escobar, ambaye atamsaidia katika jukumu hilo, kusimama ili kuwawasilishwa kwenye mkutano huo na meneja wa utetezi na kampeni wa chombo hicho chenye uzoefu mkubwa wa utetezi katika Afrika na Geneva.
Usomaji wa hati hiyo
“Tuna msimamizi mpya wa muda”, alianza kusema Kardinale Tagle, akiunganishwa kwenye dawati la mzungumzaji na Kadinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu. “Ndio, habari hii inaweza kuleta wasiwasi au kuchanganyikiwa kwa baadhi yenu. Lakini lazima muwe na uhakika kwamba uamuzi huu wa Baba Mtakatifu umekuja baada ya utafiti makini na huru wa mazingira ya kazi ya Sekretarieti na utawala unaotekelezwa na watu na vyombo vinavyohusika”. Papa amemteua kamishna wa kipekee kuzindua kwa upya ari ya Caritas Internationalis. Uamuzi uliomo katika Hati ya Papa Francisko ni matokeo ya uchunguzi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu ambao ulifichua mapungufu ya usimamizi katika muundo huo, na matokeo yake…
Kutembea pamoja
Kwa maana hiyo Kardinali aliongeza kusema “Ningependa kukuhakikishia kwamba sivyo, sivyo, sivyo, unyanyasaji wa kijinsia au unyanyasaji”, kwa kurudia mara tatu na kuongeza kuwa “siyo, tena matumizi mabaya ya pesa. Sio kuhusu hilo. Hati hiyo inaonesha wazi nia yake”. Kardinali Tagle alitoa shukrani kwa Katibu Mkuu, Aloysius John ambaye hakuwepo kwenye Mkutano huo na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uongozi na uongozi wa juu ambao kwa sasa katika kifungu cha Papa, hawapo tena madarakani. “Huu ni ni wito wa kutembea kwa unyenyekevu na Mungu na mchakato wa utambuzi, kushughulikia ukosefu wetu wa uhuru na kufuata Roho ya uhuru. Wakati huo huo, tunatembea pamoja, na tamaduni tofauti, katika maonesho yao ya kipekee ya ubinadamu”. Kardinali Tagle pia alitaja hata changamoto zinazokua ambazo Caritas inaendelea kukabiliana nazo katika kutunza maskini na waliotengwa ulimwenguni kote. Kwa sababu hiyo aliongeza kusema Hati inabainisha kwamba Sekretarieti iko tayari kusaidia wanachama na kufanya kazi kwa njia iliyounganika na mazoea bora na maadili ya Injili.
Mkutano Mkuu ujao
Baadaye mtazamo ulikuwa ni kuhamia kwenye Mkutano Mkuu ujao ambao, Kadinali Tagle alisisitiza, kwamba kwa hiyo utafika katika wakati muhimu. Ilikuwa tayari umetokea na mkutano wa 2019, wakati hakuna mtu aliyetarajia kuwa kungekuwa na janga la UVIKO-19 na hakuna mtu, miaka miwili baadaye, alijua kwamba vita vitazuka nchini Ukraine na kwamba migogoro mingine mingi iliyopo kwa miaka mingi ingesahaulika. Kwa hiyo, kazi hiyo itaendelea: “Tuna wasimamizi madhubuti ambao watatupeleka mbele, ambao watalibeba Shirikisho mbele hadi Mkutano Mkuu ujao. Na hili halitavuruga utendaji kazi wa Sekretarieti,” alihitimisha Kardinali Tagle. “Hebu tuchukue muda kufikiria jinsi mashirika yetu wanachama yanaweza kusaidia kuimarisha wakati huu mzuri.”
Msimamizi mpya wa CI, Pinelli: kujenga hali ya kuaminiana na ushirikiano
Katika dawati la mzungumzaji, Kardinali Tagle baadaye aliwapigia simu Pinelli na Amparo, ambao wote walisema kupokea jukumu hilo kwa moyo wa utumishi. Kwa upande wa Pinelli, hasa akizungumza kwa vyombo vya habari Vatican, nje ya mkutano huo alimshukuru Papa kwa imani yake na kuelezea kwamba nia yake, katika jukumu hilo jipya, ni kutaka, pamoja na watu wote wa Caritas Internationalis, kuanza michakato wa upatanisho na uboreshaji ambao unaweza kuzaa matunda kwa muda mrefu kwa chama hicho ambacho kimekuwa hai kwa miaka 70.
Kwa hivyo akiulizwa swali ikiwa uzinduzi ni wa ari ya Caritas Internationalis?, amejibu kwamba kama msimamizi wa muda ni badala ya kipengele cha kuangalia kuboresha kile ambacho tayari kimboreshwa. Amesema anakaribia huduma hii mpya kwa utulivu na unyenyekevu na anaeleza kuwa lengo la kwanza litakuwa kushirikiana na watu wa Sekretarieti na wale wote wanaoshiriki kikamilifu katika maisha ya Caritas ili kujenga hali ya uaminifu na ushirikiano.