Tafuta

Siku ya Uvuvi Duniani ya kila mwaka uadhimishwa kila ifika tarehe 21 Novemba  mwaka huu imenagukia katika muktadha wa  Mwaka wa Kimataifa wa Uvuvi wa Kisasa na Kilimo . Siku ya Uvuvi Duniani ya kila mwaka uadhimishwa kila ifika tarehe 21 Novemba mwaka huu imenagukia katika muktadha wa Mwaka wa Kimataifa wa Uvuvi wa Kisasa na Kilimo . 

Kard.Czerny:Unahitajika mshikamano kimataifa kusaidia sekta zinazohusu bahari

Siku ya Uvuvi Duniani ya kila mwaka imedhimishwa katika muktadha wa Mwaka wa Kimataifa wa Uvuvi wa Kisasa na Kilimo cha Majini (IYAFA 2022),uliotangazwa 2017 na Mkutano Mkuu wa 72 wa Umoja wa Mataifa.Kard Czerny:"Ni kukumbuka chanzo kikubwa ambacho hakijakadiriwa cha chakula cha bahari kwa mamilioni ya wanadamu.

Na Angella Rwezaula,  – Vatican.

Kuunganisha nguvu ili kutekeleza kwa ufanisi mikataba na sheria zilizopo na kushirikiana kutafuta suluhisho  za kiubunifu kwa matatizo yaliyounganishwa yanayoikabili dunia ya uvuvi, katika kujaribu kulinda ‘nyumba yetu ya pamoja. Huo ndio mwaliko ambao Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Kadinali Michael Czerny amebainisha katika ujumbe wake kwa ajili ya Siku ya Uvuvi Duniani inayoadhimishwa tarehe 21 Novemba  2022 kwa ajili ya Kukuza Maendeleo ya Kibinadamu, kwa serikali, mashirika ya kimataifa, mashirika ya sekta ya uvuvi, mashirika ya kidini na hasa taasisi za Kikatoliki kama vile Stella Maris na Caritas. Katika maandishi, Kardinali amekumbuka umuhimu wa samaki, chakula muhimu na chanzo kikuu cha protini yenye ubora wa juu kwa mamilioni ya watu; na amesisitiza jinsi, licha ya ukweli kwamba sekta ya uvuvi ina jukumu muhimu katika ustawi na maendeleo ya jamii nyingi, inakumbwa na matatizo mbalimbali yanayotishia kuwepo kwake.

Kulingana na takwimu za FAO, mnamo 2020, karibu watu milioni 58.5 walijishughulisha,  kwa muda tu, au mara kwa mara  katika sekta msingi ya uvuvi na ufugaji wa samaki, na sekta hii inawakilisha chanzo kikuu cha mapato na maisha kwa sehemu ya idadi ya watu duniani, hasa katika nchi zinazoendelea. Kwa maana hiyo amekumbusha Kardinali kwamba wavuvi wadogo wadogo na ufugaji wa samaki huzalisha asilimia 40 ya samaki duniani katika  kuchangia kwa kiasi kikubwa cha usalama wa chakula, lishe na afya. Licha ya jukumu muhimu kwa ustawi na maendeleo ya jamii nyingi duniani kote, hata hivyo, sekta hiyo inakabiliwa na matatizo kadhaa ya janga ambayo yanatishia maendeleo na maisha muhimu ya jamii za wavuvi na wakati mwingine, kuwepo kwa uvuvi. Vitisho kama vile mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bayoanuwai na kutia tindikali baharini ni masuala ya kimataifa yanayoathiri kila nchi na kila bahari.

Kwa hivyo, ili kupunguza athari mbaya za matukio hayo kwa jamii zetu, ushirikiano wa kimataifa ni muhimu, kama vile pia alivyo sisitiza Kardinali Pietro Parolin, katika hotuba yake katika Mkutano wa 27 wa Wanachama wa UNFCCC, huko Sharm el-Sheikh, mnamo tarehe 8 Novemba 2022. Kiukweli, ushirikiano kama huo wa kimataifa unaweza hata kuchangia katika kushughulikia shida zilizowekwa ndani na ambazo mara nyingi zinaweza kufuatiliwa, kama vile ukiukwaji wa haki za binadamu, mazingira duni na yasiyo salama ya kufanya kazi, yasiyoendana na utu wa binadamu, uchafuzi wa bahari na mito, uharibifu wa ardhi maeneo ya pwani, mbinu haribifu na zisizo endelevu za uvuvi na uvuvi haramu, usioripotiwa na usiodhibitiwa.

Tangu 2020, sekta ya uvuvi pia imeharibiwa na kuenea kwa janga la UVIKO-19 ulimwenguni kote, unasomeka Ujmbe huo. Kufungwa kwa bandari, masoko ya samaki na migahawa kumesababisha “kupungua kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za uvuvi na uuzaji wa mazao ya samaki na hivyo kupoteza ajira na kipato kwa watu wengi hasa wanawake” walioajiriwa katika sekta hiyo kwa kiwango cha juu. asilimia. Na ingawa serikali kutoka kote ulimwenguni zimeingilia kati, na kwa bahati mbaya, kutokana na mapungufu ya uingiliaji huu wa kipekee wa serikali, watu wengi wameachwa peke yao na bila msaada wa kukabiliana na shida, hata ikiwa wengine wameachwa. kusaidiwa na mashirika ya kutoa misaada, yakiwemo yale ya Kikatoliki".

Kwa kuzingatia haya yote, kwa kuwa kila kitu kimeunganishwa na sote tuko kwenye mashua moja kardinali amebainisha kuwa ni muhimu kuungana na juhudi zetu za kuunda ufahamu mpya wa kijamii na aina ya ubunifu ya mshikamano ambayo hakuna mtu anayeachwa nyuma.  Akikumbuka maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, ambaye anasisitiza jinsi sote tunaweza kushirikiana kama vyombo vya Mungu vya utunzaji wa uumbaji, kila mtu kulingana na utamaduni wake, uzoefu, kujitolea na talanta yake, Kardinali Czerny anatoa wito kwa taasisi bora na makini zaidi na sera za kusaidia, kukuza na kulinda wale wote wanaohusika na sekta ya uvuvi na familia zao.

Ujumbe wa Vatican kuhusu Siku ya Uvuvi duniani
23 November 2022, 16:13