Tafuta

Ili Ulimwengu, uweze kuokolewa unahitaji haki ya chakula. Ikiwa hakuna haki ya chakula hakutakuwa na amani na wala kuwa na  utulivu. Ili Ulimwengu, uweze kuokolewa unahitaji haki ya chakula. Ikiwa hakuna haki ya chakula hakutakuwa na amani na wala kuwa na utulivu. 

Haki ya chakula ni lengo linaloweza kufikiwa

Usalama wa chakula duniani,ambao pia ni kama mahakama ya kimataifa ya usalama,unahitaji kusitisha janga la njaa kwa kuonesha mifano ya uzalishaji,usindikaji, usambazaji wa chakula na kubuni kwa upya miundombinu ya kiuchumi,kifedha na kisheria ili kuhakikisha haki ya kila binadamu.

Na Angella Rwezaula -Vatican.

Ili Ulimwengu, uweze kuokolewa, unahitaji haki ya chakula. Ikiwa hakuna haki ya chakula hakutakuwa na amani na wala kuwa na utulivu. Picha ya meli za Kiukreni zilizopakiwa na nafaka na kufungwa bandarini, zilizokwama kama mateka sababu ya mzozo, zinafanya kuonesha uwazi wa changamoto ya kimaadili na adili yenye changamoto kubwa. Kwa maana hiyo ni kuema kuwa mgogoro wa aina tatu: mgogoro wa kivita, mgororo wa Uviko  na mgororo wa mabadiliko ya tabia nchi ambavyo vimewaka wazi kabisa na kufichua mwingiliano usioweza kutenganishwa wa mambo ambayo yanaunda hali inayoweza kusababisha kifo katika ulimwengu. Vikosi vya wenye njaa, milioni 840 ifikapo 2030, vina uzito juu ya hatima ya kila mtu.  Kwa sababu ukosefu wa usalama wa chakula ni usemi ambao hauwezi kushindwa kuwa wa kustaajabisha mbele ya dhuluma kali ya wale waliotengwa na mkate wa kila siku ni matokeo ya mafundo yote ambayo hayajatatuliwa na ambayo yanapunguza na kutishia jamii ya wanadamu kwa ujumla.

Usalama wa chakula duniani, ambao pia ni kama mahakama ya kimataifa ya usalama, unahitaji kusitisha janga la njaa kwa kuonesha mifano ya uzalishaji, usindikaji, usambazaji wa chakula na kubuni kwa upya miundombinu ya kiuchumi, kifedha na kisheria ili kuhakikisha haki ya kila binadamu. kwa chakula, na chakula bora na endelevu. Kwa miaka kumi na tano, ghasia za kutafuta mkate, kuanzia Cairo hadi Baghdad, Sudan, na kwingineko  zimechochea migogoro inayoivuruga sayari. Na tatizo kubwa linaweza pia kutatuliwa kwa kurudisha sera za chakula na kilimo kwenye umoja adilifu, zikitenganishwa na kiuchumi na, zaidi ya yote, mifumo ya kifedha ambayo imeshindwa. Muundo mpya wa mzunguko, kutoka katika jumuiya za wakulima wa ndani, hadi usindikaji na usambazaji wa chakula kwa njia endelevu, unaweza kuzalisha mazingira ya amani na utulivu ambapo vita si rahisi kufanya; pia kwa sababu hakuna meli za kuzuia na ngano inaweza kukua mahali popote bila unyonyaji wa hajabu  na jangwa la mazingira.

Hii ndiyo hali iliyojitokeza katika siku ya utafiti uliokuwa unaongoza na mada Msimwache mtu nyuma: uzalishaji bora, lishe bora, mazingira bora kwa wote, ilioandaliwa na Ubalozi wa Vatican katika makao ya FAO, IFAD na WFP, Jukwaa la Roma la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayoongozwa na Wakatoliki na mwenyekiti wa Maadili ya Kibiolojia na Haki za Binadamu katika Vhuo Kiukuu cha Kipapa cha Regina Apostolorum na Chuo Kikuu cha Ulaya cha Roma hivi karibuni. Kardinali Peter Turkson, Kansela wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi, akiwahutubia washiriki wa siku hiyo alisema kuwa  uharaka huo ulionekana, kutoka kwa waingiliaji  kati na waendeshaji kwenye siku hiyo. Kuzuia  mfumko wa bei ya chakula na mbegu, kwanza kabisa, na chakula na maji ya bure kutoka katika ukiritimba wa kifedha ambao unafanya kuwa ya chini (kupitia njia ya kunyakua ardhi na kunyakua maji). Haki ya chakula sio lengo lisilowezekana. Kwa maana hiyo kuna nia, zana na vipaji”, Katika hotuba hiyo Kardinali alisema wanachohitaji ni ujasiri wa kuweka vipaji na ubunifu katika huduma ya kitu kipya.

Neno ujasiri pamoja na wajibu, limerudi tena na tena ambapo Kardinali Turkson, hasa, aliikumbuka kwa kuorodhesha njia nne za kufuata ili kujiweka katika huduma ya kitu kipya. Kufupisha umbali kati ya wazalishaji wa ndani na mfumo wa uzalishaji, ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na kuhakikisha uthabiti wa mlolongo wa chakula ambapo alitoa mfano kuwa {kinyume chake, mawazo ya meli za nafaka za Kiukreni zilizochukuliwa mateka katika kurudi bandari, kwamba ni mfano wa udhaifu mkubwa wa mlolongo wa chakula). Baadaye kuweka mahitaji ya jumuiya za kiasili katikati ya mjadala wa kimataifa na, kupitia chaguo la upendeleo la maskini, shirikiana nao ili kutumia vyema hekima na uzoefu wao katika usimamizi endelevu wa mfumo ikolojia.

Sehemu ya tatu ni kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali, kupitia mfano wa mzunguko wa uzalishaji wa chakula kwa mfano (kuzalisha, kutengeneza upya, na kulinda). Hatimaye, labda kazi ngumu zaidi ni ile ya kurekebisha usanifu wa kiteknolojia na kifedha ambao hutumika kama mfumo wa mfumo wa chakula. Chakula lazima kiwe huru kutoka katika hadhi ya bidhaa ya kawaida. Wadau wa kubahatisha wa fedha lazima wakome. Kwa mujibu wa Kardinali Turksoni alikumbuka kauli mbiu ya Expo 15 huko Milano Italia kwamba, Tunapokuwa familia moja basi kutakuwa na chakula kwa kila mtu". Kwa maaha hiyo katika migogoro mitatu inahitahi ardhi, kazi na paa la nyumba.

Jukumu la kueleza kwa kutumia zana gani za kutekeleza utume wa kijasiri uliooneshwa na Profesa Stefano Zamagni, rais wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii. Kwanza kabisa, aliweka wazi kwamba simulizi la upungufu wa chakula ni uongo, kuwadhuru maskini.  Dunia, inazalisha chakula kwa watu bilioni 12 katika uso wa idadi ya watu wanane na upotevu mkubwa wa chakula. Umaskini na njaa hutegemea tu, jinsi tunavyofanya mambo ya  kazi. Mkusanyiko wa aina za kilimo-chakula, alisema, huku akikumbuka kwamba mbegu za dunia kwa kiasi kikubwa ziko mikononi mwa mashirika 4 ya kimataifa na hivyo  lazima kuvunjwa. Bado tunahitaji ujasiri ili kulazimisha mfumo wa kutokuaminika na kuunda Bodi ya Uthabiti wa Mfumo wa Chakula ambayo inashughulikia bei.

Naye Profesa Alberto Garcia Gomez, mkuu wa Kitivo cha Maadili ya Biolojia cha Regina Apostolorum, alisema kuwa Wachumi wa uwongo wanabishana kuwa haiwezekani. Lakini ni ujinga, alisisitiza hayo kuwa tangu 2005 kanuni 15 zinazohusiana na haki ya kupata chakula zimeingizwa katika sheria za kimataifa na zinaweza kuanzishwa. Bioethics ina kila kitu cha kufanya na mambo ambayo yanaathiri udhalilishaji wa utu wa mwanadamu, alisema. Na ukweli unaonaweza kufanyika ulithibitishwa na uzoefu kutoka katika nyanja hiyo na  Francesca Benigno wa Focsiv kuhusu mpango wa  ukombozi wa wakulima wa Myammar na Mariangela Giorgi wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani ambayo, ni miongoni mwa mipango  mingi iliyoonesha kuwa wanawake wakulima huko Peru na bustani za familia huko Argentina.

Uzalishaji na usambazaji wa chakula ni muhimu duniani ili kutomwacha yeyote nyuma
03 November 2022, 14:36