Euntes in mundum universum:Kongamano kimataifa kwa miaka 400 ya Propaganda fide
Na Angella Rwezaula, -Vatican.
Karne nne za utume wa kutangaza Injili, ndilo kwa hakika msingi wa Baraza la Propaganda Fide ambalo leo hii linaitwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. Ni historia ndefu sana na ya kina ambayo itakuwa kitovu cha Kongamano la Kimataifa kwa ajili ya Mafunzo kuanzia tarehe 16 hadi 18 Novemba 2022 katika Chuo Cha Kipapa la Urbaniana jijini Roma. Kongamano la Kimataifa la mafunzo, lililohamasishwa na kuandaliwa na Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa Watu kwa ushirikiano na Chuo cha Kipapa cha Urbaniana na Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Historia, kwa hakika linakusudia kupitia masuala msingi ya karne nne za mchakato wa maisha tangu kuanza kwake.
Mnamo 1622, Papa Gregorio XV alianzisha Propaganda Fide
Ilikuwa ni mnamo tarehe 6 Januari 1622 wakati Papa Gregorio XV alipoanzisha Sacra Congregatio de Propaganda Fide yaani Shirika Takatifu la kueneza Imani, ambalo kwa uchaguzi kisheria mnamo tarehe 22 Juni iliyofuata likawa na katiba yake Inscrutabili divinae Providentiae arcano yaani Majaliwa ya kimungu yasiyoweza kuchunguzwa, na baadaye zilifuata hata nyaraka nyingine msingi za kipapa kama ile ya Romanum decet yaani Inapaswa kuwa ya kirumi (ya tarehe hiyo hiyo), Cum inter multiplices yaani Wakati kati ya mengi (ya 14 Desemba 1622), Cum nuper yaani Tangu hivi karibuni (ya 13 Juni 1623), na hatimaye nyingine Immortalis Dei yaani Mungu asiyeweza kufa (ya 1 Agosti 1627). Shughuli maalum za Baraza hilo daima zimekuwa ni kueneza Imani ulimwenguni kote, kwa umahiri wa kipepee katika kuratibu nguvu zote za kimisionari, kutoa maelekezo kwa ajili ya utume kimisionari, kukuza malezi ya makasisi na madaraja ya makuhani mahalia, kuhimiza msingi wa taasisi mpya za kimisionari na hatimaye kutoa misaada ya kimwili na kiroho kwa ajili ya shughuli za kimisionari. Kwa maana hiyo Baraza jipya kwa wakati huo likawa chombo cha kawaida na cha kipekee cha Baba Mtakatifu na Vatican kwa ujumla kwa ajili ya kutekeleza mamlaka juu ya utume na ushirikiano wa kimisionari ulimwenguni kote.
Wazungumzaji 24 kutoka nchi 9 wa mabara 5
Katika Kongamano la kimataifa kwa maana hiyo hadi sasa shukrani kwa mchango uliowezekana wa wazungumzaji wapatao 24 kutoka nchi 9 wa mabara 5, ambapo watatoa umakini kwa tafsiri ya kihistoria ya asili ya kitaasisi ya Propaganda Fide, ambalo leo hii linajulikana kila mahali ulimwenguni kote kama Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, huku wakizingatia majukumu yaliyohusishwa na Umoja na Mapapa tangu karne ya kumi na saba, wakichunguza baadhi ya watu, takwimu husika za Wasimamizi kati ya karne ya kumi na nane na kumi na tisa na juu ya yote kuweka nuru ya shughuli nyingi na zenye matunda zilizofanywa na Propaganda Fide hadi kuzaa matunda mengine zaidi pia katika uthibitisho wa asili ya Kanisa Katoliki kwa ulimwengu wote.
Kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki 1967
Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu leo hii, ambapo Propaganda Fide, hapo zamani pia lilitekeleza kazi zilizohusishwa katika karne iliyopita kwa ajili ya Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, ambapo baadaye, likabadilishwa lna kujetegemea tangu mnamo tarehe 15 Agosti 1967 na katiba ya Kitume ya Mtakatifu Paulo VI, ya Regimini Ecclesiae Universae, yaani Utawala wa Kanisa la Ulimwengu. Na leo hii imeanza kutumika Katiba mpya ya Kitume Praedicate Evangelium yaani Hubirini Injili ya Baba Mtakatifu Francisko, ambayo uwezo wake ulikabidhiwa, kuanzia tangu tarehe 5 Juni 2022, na kwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu ambapo Papa ndiye msimamizi Mkuu wa Uinjilishaji.
Kauli mbiu Enendeni Ulinwenguni kote inaongoza
Kongamano la Kimataifa linaongozwa na kauli mbiu kutoka katika kifungu cha Injili ya [Mk 16,15] kisemacho, Euntes in mundum universum, yaani Enendeni Ulimwenguni kote kwa kutaka kuweka wazi ule mwanga wa Baraza hilo jinsi ambavyo limeweza kuhamasisha mchakato mbali mbali kuanzia na migogoro ya kidini, hadi kufikia ufunguzi wa majadiliano wazi, kukutana na Injili na mikitadha mbali mbali ya kiutamaduni, hata kuona tamaduni mbali mbali za kidini katika kuendelea bila kuchoka kukuza kazi yake ambayo inarudisha mwangwi wa asili ya utume wa Kanisa. Kutakuwa na sehemu tano za mjadala katika Kongamano ambalo litafunguliwa Jumatano tarehe 16 Novemba 2022 kwa kujikita na mada ya Baraza la Propaganda Fide: Uinjilishaji na Utume, itakayotolewa na Kardinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. Mada ya pili itakuwa ni Sura muhimu na upyaishwaji wa kitaasisi, itakayotolewa na Padre Leonardo Sileo, Gambera wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana. Na Sehemu ya tatu, itajikita katika mada Huduma ya kueneza imani kwa watu katika mabara yote, ambayo itatolewa na Askofu Mkuu Protase Rugambwa, Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu.
Kuanzia migogoro hadi mazungumzo na kukutana na tamaduni nyingi
Ijumaa tarehe 18 Novemba Kongamano litahitimishwa na sehemu ya nne na mada, Kuanzia migogoro hadi mazungumzo, itakayotolewa na Tadeus Jan Nowak, Katibu Mkuu wa Shughuli za Kipapa za Uenenaji wa Imani; na hatimaye sehemu ya tano, ambayo itakuwa na mada ya kukutana na tamaduni nyingi, itatolewa na Padre Bernard Ardura, Rais wa Kamati ya Kipapa ya Sayansi za Kihistoria. Atakaye hitimisha Kongamano hilo la kimataifa atakuwa ni Gianpaolo Romanato wa Chuo Kikuu cha Mafunzo huko Padua na Tume ya Kipapa ya Sayansi za Kihistoria.