Tafuta

Jimbo katoliki la Torit, Sudan Kusini, limepata Askofu Mpya Padre Emmanuel Bernardino Lowi Napeta. Jimbo katoliki la Torit, Sudan Kusini, limepata Askofu Mpya Padre Emmanuel Bernardino Lowi Napeta. 

Padre Emmanuel B.Lowi Napeta ni Askofu Mpya wa Jimbo la Torit,Sudan Kusini

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo katoliki la Torit,Sudan Kusini,Mheshimiwa sana Padre Emmanuel Bernardino Lowi Napeta,wa Jimbo kuu Khartoum,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Matayo Jimbo la Khartoum.Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 24 Oktoba 2004 kwa ajili ya jimbo la Khartoum.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tarehe 8 Novemba 2022, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mpya wa Jimbo katoliki la Torit, Sudan Kusini, Mheshimiwa sana, Padre Emmanuel Bernardino Lowi Napeta, wa Jimbo la Khartoum, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Matayo Jimbo hilo Kuu Katoliki la Khartoum. Wasifu wake, Askofu Mteule Emmanuel Bernardino Lowi Napeta alizaliwa mnamo tarehe 19 Desemba 1973 huko Kapoeta, katika jimbo la Torit. Alifundwa katika seminari Ndogo ya Mtakatifu Augustine huko Khartoum (1994-1995) na baadaye Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo huko Khartoum (1996-2003). Mnamo tarehe 24 Oktoba 2004 alipewa daraja la Upadre kwa ajili ya Jimbo Kuu la Khartoum.

Shughuli za kichungaji kuanzia na masomo ya juu

Katika maisha yake ya huduma  ya kichungaji aliweza kufunika nyazifa  mbali mbali ambazo ni pamoja na mafunzo kama Paroko Msaidizi wa Roho Mtakatifu huko  Omdurman, Khartoum (2004-2007); Mkurugenzi wa Taasisi ya Makatekista kwa ajili ya Milenia ya Tatu,  huko Khartoum (2007-2010);  Aliendelea na Mafunzo ya  Shahada ya kwanza ya  Elimu ya Sayansi na Elimu ya dini (2010-2012), Uzamili wa Elimu ya Uchungaji wa Vijana na Makatekista katika Chuo Kikuu cha Kipapa  cha Salesian Roma (2012-2014); Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro na Paulo huko Khartoum (2014-2017);  na hatimaye tangu  2017,  hadi uteuzi huo amekuwa Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Matayo  jijini  Khartoum nchini Sudan Kusini.

Papa amemteua Askofu mpya kwa ajili ya Jimbo katoliki la Torit,Sudan Kusini
08 November 2022, 17:30