Tafuta

Rais wa PMS,Askofu Mkuu Dal Toso Rais wa PMS,Askofu Mkuu Dal Toso 

Askofu Mkuu Dal Toso-kuchangia maisha ya Kanisa kwa wokovu duniani ni wajibu kikristo

Karama ya Mashirika ya PMS ni ile ya kuwasaidia waamini binafsi kuishi imani yao katika kiini chao kama imani ya kimisionari na ya ulimwengu mzima.Sio kitu ambacho kimewekwa juu ya imani lakini husaidia kuishi imani katika uadilifu wake.Ni katika hotuba ya Rais wa PMS,Novemba 17 katika fursa ya Kongamo la kimataifa la Euntes in mundum universum la maadhimisho ya miaka 400 ya Propaganda fide.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Njia tatu za shughuli za wakati wa  siku zijazo  za PMS  ni ushirikiano zaidi na Makanisa mahalia; kuamsha hisia za kimisionari; kuweka uhai, sambamba na Majisterio ya Mapapa, na wakati huo huo kuwa na wasiwasi kwa ajili ya missio ad gentes yaani Utume kwa watu.  Mageuzi ya kihistoria na changamoto za sasa, ndio ulikuwa mtazamo ambao wa tarehe 17 Novemba alasiri wa Askofu Mkuu Giampietro Dal Toso, Rais wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa, (PMS)  aliyowasilisha  katika mageuzi yao ya kihistoria lakini zaidi ya yote katika uhusiano wao na wa kwanza wa Propaganda Fide na baadaye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Alisema hayo katika Kongamano la Kimataifa kwa ajili ya Mafunzo Euntes in mundum universum kuenzi miaka 400 ya Propaganda fide, kuanzia 16 -18 Novemba 2022 katika Chuo Cha Kipapa la Urbaniana Roma. 

Kuzaliwa na maendeleo ya kueneza Imani ulimwenguni

Ni Kongamano la Kimataifa la mafunzo, lililohamasishwa na kuandaliwa na Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa Watu kwa ushirikiano na Chuo cha Kipapa cha Urbaniana na Kamati ya Kipapa ya  Sayansi ya Historia, kwa kutaka kupita masuala msingi ya  karne nne za mchakato wa maisha tangu kuanza kwake. Askofu mkuu Dal Toso katika hotuba yake alieleza chimbuko la Mashirika manne ya Kipapa katika mchakato wa safari ya kihistoria, uwepo wao katika nyaraka rasmi za miaka 100 iliyopita na badaye  kujikita katika uhusiano na Propaganda Fide, huku akihitimisha hotuba yake kwa kutafakari kwa kina  juu ya mustakabali wa Mashirika yenyewe kwa miaka mia mbili baada ya kuanzishwa kwa Shirika la Kueneza Imani, ambapo lilianzishwa mnamo  tarehe 3 Mei 1822, likiongozwa na Mwenyeheri Pauline Jaricot. Akitazama juu ya kuzaliwa na maendeleo ya Mashirika ya Kimisionari, Askofu Mkuu Dal Toso alisisitizakwamba kuenea kwake kwa haraka na kuongezeka kuliwezekana shukrani kwa  hisia nyeti ya kimisionari iliyokuwepo wakati huo.

Magazeti na barua za wamisionari zilitoa umani wa kupendezwa na waamini

Kipengele kilichotoa msukumo mkubwa wa kimisionari kilikuwa ni magazeti na barua za wamisionari, ambazo zilikuwa na uamuzi wa kupendezwa na ushiriki wa waamini. Askofu Mkuu Dal Toso alisisitiza jambo msingi wa maisha ya Mashirika hayo kwamba: Miaka mia moja iliyopita, yaani  tarehe 3 Mei 1922, Papa Pius XI alitaka Jumuiya tatu za kwanza ziwe za Kipapa na akazikabidhi kwa  Propaganda fide ya wakati ule: katika hilo kama chombo kikuu ambacho Papa, kwa msaada wa Makanisa mahalia ya ulimwengu mzima, aliunga mkono shughuli ya kimisionari kwa njia bora na zana. Rais wa PMS aidha likumbusha upekee wa muundo huo kwamba  tangu mwaka 1995 umekuwa ni desturi kwamba Rais wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa ni wa kipekee kwa Mashirika yote manne na wakati huo huo ni Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. Askofu Mkuu aliweza kuakisi vile vile  karama inayoamua hali maalumu ya roho ya PMS, akisisitiza jinsi ambavyo sala, upendo na habari/malezi ni nyenzo tatu zinazoweza kupatikana na kutumika kwa dhana tatu, imani, utume, ulimwengu wote, kwa kuielezea.

Karama ya PMS ni kusaidia waamini kuiishi imani yao kwa matendo ya kimisionari 

Askofu Mkuu alifafanua zaidi kwamba anaamini karama ya Mashirika hayo ni ile ya kuwasaidia waamini binafsi kuishi imani yao katika kiini chao kama imani ya kimisionari na ya ulimwengu mzima. Sio kitu ambacho kimewekwa juu ya imani lakini husaidia kuishi imani katika uadilifu wake. Askofu Mkuu aidha  alionesha njia tatu za shughuli za wakati wa  siku zijazo kwamba  ni ushirikiano zaidi na Makanisa mahalia; kuamsha hisia za kimisionari; kuweka uhai, sambamba na Majisterio ya Mapapa, na wakati huo huo kuwa na wasiwasi kwa ajili ya missio ad gentes, yaani utume wa watu. Askofu Mkuu Dal Toso alihitimisha akisema kuwa kuchangia maisha ya Kanisa kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu ni wajibu ambao pia unaambatana na waamini wote katika siku zijazo.

18 November 2022, 16:19