WYD 2023 Lisbon:Mkutano wa maandalizi huko Fatima:Tujenge madaraja!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa kuungana pamoja kama Kanisa la ulimwengu linalotembea pamoja, Papa Francisko anatamani Kanisa liwe la kisinodi na kwa mtindo huo huo. Amesisitiza hayo Kardinali Kevin Farell Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha katika hotuba yake ya ufunguzi tarehe 17 Oktoba 2022, katika Mkutano wa kimataifa wa maandalizi ya Siku ya Vijana (WYD) huko Lisbon nchini Ureno. Mkutano huo uliandaliwa na Kamati mahalia ya maandalizi kwa ushirikiano na Ofisi ya vijana ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ambapo ulihimitimishwa tarehe 19 Oktoba 2022 huko Fatima. Walioshiriki ni wawakilishi 300 kutoka nchi Mabaraza ya maaskofu, ulimwenguni, harakati za kikanisa na vyama vya kitume duniani.
Katika hotuba yake Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei Familia na maisha kwenye uzinduzi huo alikumbisha Wosia wa Kipapa wa Baada ya Sinodi wa Christus Vivit, ambapo alisema Baba Mtakatifu alitengeneza uchungaji wa vijana wa kisinodi ambao ni wa kushangaza. “Kwa njia hii, kwa kujifunza kutoka kwa wenzetu, tunaweza kutafakari vyema ukweli huo wa ajabu wenye sura nyingi ambao Kanisa la Kristo linakusudiwa kuwa. Atakuwa na uwezo wa kuvutia vijana, kwa maana umoja wake si mmoja, lakini badala yake ni mtandao wa karama mbalimbali ambazo Roho bila kukoma humimina juu yake, kumfanya upya na kumwinua kutoka katika umaskini wake”(n. 207). “Katika wao wenyewe vijana wako mstari wa mbele katika mabadiliko: “Ninataka kuwatia moyo ninyi nyote katika juhudi hii, kwa sababu najua kwamba “mioyo yenu michanga inataka kujenga ulimwengu bora. Nimekuwa nikifuatilia ripoti za habari za vijana wengi ulimwenguni kote ambao wamejitokeza barabarani kueleza tamaa.
ya kuwa na jamii yenye uadilifu na kindugu. Vijana wakiingia mitaani! Vijana wanataka kuwa wahusika wakuu wa mabadiliko. Tafadhali, msiwaachie wengine kuwa wahusika wakuu wa mabadiliko. Ninyi ndio mnaoshikilia siku zijazo! Kupitia ninyi, siku zijazo huingia ulimwenguni. Nawaomba pia muwe wahusika wakuu wa mabadiliko haya. Ninyi ndio mnaoshikilia ufunguo wa siku zijazo! Endelea kupambana na kutojali na kutoa jibu la Kikristo kwa matatizo ya kijamii na kisiasa yanayojitokeza sehemu mbalimbali za dunia. Ninawaomba mjenge siku zijazo, kufanya kazi kwa ulimwengu bora. Vijana wapendwa, tafadhali, msiwe watazamaji katika maisha. Jihusishe! Yesu hakuwa mtazamaji. Alihusika. Msijitenge, bali jitumbukizeni katika uhalisia wa maisha, kama Yesu alivyofanya. Zaidi ya yote, kwa njia moja au nyingine, pambania manufaa ya wote, wahudumie maskini, muwe wahusika wakuu wa mapinduzi ya upendo na huduma, wenye uwezo wa kupinga patholojia utumiaji hovyo na ubinafsi wa juu juu” ( 174).
Katika mapendekezo ta waraka huo, Kardinali Farrell aliwaalika washiriki wote kuacha kwamba vijana wenyewe wanakuwa mstari wa mbele. Kiukweli wao watakuwa na mawazo makubwa ya ubunifu kuhusu ni jinsi gani ya kutoa muundo wa hija ya WYD. Fursa moja nzuri ya kuandaa inaweza kuwa Siku ya vijana duniani kijimbo ambayo Baba Mtakatifu Francisko aliamua ifanyike katika Siku Kuu ya Kristo Mfalme. Katika mapendekezo ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, alitoa maelekezo katika chapisho la “Maelekezo ya kichungaji kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya vijana Ulimwengucu katika makanisa maalum.” Kwa mujibu wa Kardinali Farrell Msingi wa Kisinodi una hata sifa ya moja kwa moja ya mkutano huo uliofanyika Fatima. Kwa sababu ya jitihada zaidi zinazoonesha matazmio ya WYD ni zile za Upatriaki wa Lisbon na Kamati ya maandalizi, hiyo haina maana kwamba wengine wote wanakuwa watumiaji wa sadaka. Na hiyo isingekuwa Kanisa la kisinodi; kinyume chake alibainisha wote ni waaandaaji katika Siku ya vijana ijayo ulimwenguni. Na ni kwa wote wawajibikaji. Kardinali Farrell alisisitiza kwamba kutokana na tukio kuwa kubwa la vijana ulimwenguni, WYD inahitaji juhudi kubwa ya maandalizi. Lakini pamoja na hayo matunda yake yake yapo kwenye ngazi nyingine. Mara nyingi yaliyofichwa na madogo.
Kuna usikivu wa kimya kwa wito kwa Kristo katika huduma ya kikuhani na kwa wito wa maisha ya kitawa, kuna hata mbegu nyingine za wakati ujao za ndoa, na kuna miito kwa wahitaji na uundaji ambao uwainue vijana na kuwaamsha katika matendo ya upendo hai. Ni harakati zote ambazo zinakuja kutoka kwake Kristo. Upendo wake unawaamsha vijana kama alivyofanya kwa Maria kuelekea kilima cha Yuda ili kumtembelea binadamu yake Elizabeth. Kwa mtazamo huo Kardinali Farrell alitaja maneno ya Ujumbe wake Papa Francisko kwa siku ya vijana ya XXXVII, wakati alipokumba Mama wa Mungu kutembelea watu wake. Ni pale pale Fatima kiukweli, Bikira aliwatumia kizazi chote ujumbe wa nguvu upendo wa Mungu ambaye anaalika uongofu, na uhuru wa kweli. Kutokana na hayo ndipo mwito wa kuunda jumuiya yenye nguvu ya sala katika hali mahalia. Kwa upande wa Kardinali alisema kufanyika mkutano huo wa moja kwa moja kwa sababu ndiyo ishara ya ujenzi wa madaraja kati ya mataifa na tamaduni. Hii ndiyo maana ya Siku ya Vijana duniani ambayo inawakilisha tangu kuzaliwa kwake.
Ujumbe wake huu kamwe haujawahi kuwa wa zamanai na leo ni wa lazima sana. Mkutano huo ni wa kipekee wa Kanisa la ulimwengu katika safari na ndiyo tamaini la Baba Mtakatifu Francisko kuwa kanisa la Kisinodi. Huo ulikuwa ni mkutano wa kwanza wa uwepo wa moja kwa moja kati ya wawakilishi wa kichungaji baada ya WYD ya Panama, kwa sababu ya janga la Uviko-19 kwa sababu mkutano wa mwisho ulikuwa umefanyika kwa njia ya mtandao mwezi Novemba 2020, ambapo waliweza kushiriki kati ya wengine, Kardinali Manuel Clementi, Patriaki wa Lisbon, Askofu Mkuu Ivo Scapolo Balozi wa Vatican, Askofu Ornelas Carvalho, Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ureno, Askofu Americo Aguir Askofu Msaidizi wa Lisbon na Mratibu Mkuu wa WYD, wajumbe wa kamati ya maadalizi na Augusto Santosi Silva ,Mwenyekiti wa Bunge la Ureno .
Ikumbukwe kwamba katika Siku ya vijana ulimwenguni itakayoanza tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023, inaongozwa na ishala muhimu. Uwasilishaji kwa vijana wa Ureno Msalaba wa Hija na Picha ya Mama Yetu, Salus Populi Romani, yaani Afya ya Watu wa Roma ndizo, alama za Siku ya Vijana Ulimwenguni, ambazo zilikabidhiwa mnamo tarehe 22 Novemba 2020, katika siku ya Sherehe ya Kristo Mfalme. Kati ya Novemba 2021 na Julai 2023, alama za WYD zinaendelea kufanya hija kupitia majimbo 21 ya Ureno, ili kutangaza mkutano mkubwa zaidi wa vijana ulimwenguni ambao utafanyika katika msimu wa joto wa 2023, huko Lisbon.
Maandalizi ya kila Siku ya Vijana Duniani, utambuzi wake na mvuto unaotiwa chapa katika mkutano wa vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia na Papa, umekabidhiwa kwa wsimamizi, yaani, watakatifu waliotangazwa kuwa watakatifu au katika mchakato wa kutangazwa kuwa watakatifu ambao ni wenye heri. Kwa ajili ya Siku ya vijana (WYD) Lisbon 2023, Kamati ya Maandalizi mahalia ilipendekeza wasimamizi 13, wanawake, wanaume na vijana ambao, kama Kardinali alivyothibitisha, kwamba wameonesha kuwa ‘maisha ndani ya Kristo hujaza na kuokoa vijana wa nyakati zote’. Walinzi na wasimamizi hao, ambao walizaliwa katika jiji linalohudumiwa na Siku ya Vijana (WYD) au wanatoka nchi nyingine, ni mifano kwa vijana wote kwa kila nyakati. Watakatifu hao na wenyeheri ni: Mtakatifu Yohane Paulo II, Mtakatifu Yohane Bosco, Mtakatifu Vincent, Mtakatifu Anthony wa Padua, Mtakatifu Bartholomew shahidi, Mtakatifu Yohane wa Brito, Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati, Mwenyeheri Marcel Callo, Mwenyeheri Johana wa Ureno, Mwenyeheri Joao Fernandes, Mwenyeheri Maria Clara wa Mtoto Yesu, Chiara Badano na Mwenyeheri Carlo Acustis
Wasimamizi wa siku ya vijana kijimbo katika kuelekea uliwenguni
Maandalizi ya WYD Lisbon 2023 pia yamekabidhiwa kwa walinzi wa Jimbo kwa Siku ya Vijana Duniani. Kwa hivyo, kila jimbo limechagua watakatifu ambao ni marejeo ya kila hali halisi ya kijimbo na ambao, kwa mfano wao na ulinzi, watasaidia katika safari ya kuelekea siku ya vijana duniani (WYD) Lisbon 2023.