‘Vita di Gesu’,tukio katika uzuri wa Injili:uwakilishi wa kitabu cha Tornielli!
Na Angella Rwezaula; - Vatican
Katika barabara zenye vumbi za Galilaya na Palestina, akifuta machozi ya Yoshua mdogo na mama yake Rebeka, aliyefarijiwa na heri ya Mahubiri ya Mlimani, akisikia sauti na ladha ya harusi huko Kana, akikutana na macho ya Zakayo kwenye kijani kibichi, la tumbo la mkuyu, akitabasamu pamoja na Yesu ambaye mfuko uliotayarishwa na mama yake kwa ajili ya kuanza maisha ya watu wote. Hisia na na mhemko zinazotolewa na nguvu ya neno lililoandikwa na sauti ya muziki, ziliashiria uwasilishaji wa kitabu kipya kiitwacho “ Vita di Gesù”, yaani Maisha ya Yesu, Jumatano tarehe 12 Oktoba 2022 mchana katika Chuo Kikuu cha Lumsa jijini Roma.
Mtunzi wa Kitabu hiki kipya ni Mhahariri Mkuu wa vyombo vya habari vya Vatican, Dr. Andrea Tornielli. Kitabu, chenye utangulizi wa Papa Francisko, tunda la mapokeo mapana ya biblia lakini juu ya uvumbuzi wote wa mwandishi, unaofuatilia miaka 33 ya Mwana wa Mungu na mikutano, halisi au ya kufikirika, yenye wahusika wengi kutoka Injili hadi kufikia ambaye amepewa uso na jina. Miongoni mwa waliosikiliza katika Chuo Kikuu hatua chache kutoka Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro (maaskofu na makardinali na Gambera Francesco Bonini walikuwepo), ilionekana karibu kuwagusa wahusika hawa, kwa kuangalia kwa macho yao na kuzungumza nao, shukrani kwa liwaya kama la kimapenzi ambapo mwandishi Dr. Tornielli.
Ladha hiyoe ilifurahishwa kupitia usomaji wa vifungu viwili kwa sauti ya Alessandro De Carolis, kati kati ya nyimbo nzuri zaidi kwenye Radio ya Vatican. Sauti ya ala ya kusisimua ya Violin ya Bahari iliyotengenezwa kwa mbao za boti za wahamiaji wengi wanaokimbia kutoka Afrika ilipigwa. Muziki huo wa violin, ambao kijana Lea Sabatini alicheza kwa wimbo wa Ave Maria yaani Salamu Maria, wa mtunzi Schubert's ni zawadi ambayo alitaka kumpatia mwandishi wa kitabu kama “fadhila za kurasa zake ambazo ni kitu adimu katika ulimwengu huu” kama ilivyoelezwa. Naye Arnoldo Mosca Mondadori, mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la 2Casa dello Spirito e delle Arti,2 lililoanzishwa mwaka 2012 huko Milano likifanya kazi kwa ajili ya kuhamasisha jamii na maendeleo ya walio hatarini zaidi.
“Tunacheza kwa ajili ya uzuri wa Injili, wa maisha ya Yesu”, alisema Mondadori ambaye tayari aliwasilisha kitabu cha Tornielli huko Milan mnamo 29 Septemba, iliyopita pamoja na Askofu Mkuu Mario Delpini, wa Jimbo Kuu katika Gereza la Opera, ambapo mipango mingi ya shirika hilo lisilo la kiserikali linafanya kama vile: utengenezaji wa Ostia au uundaji wa vyombo vya muziki. Wote wawili Mondadori na Tornielli walirejeea jioni hiyo kueleza uchaguzi wa maungamao kama mahali pa uwasilishaji wa kwanza kwa sababu hakuna mahali pengine ambapo unaweza kuona matukio kutoka katika Injili yanaishi. Hivi ndivyo ilivyokuwa wiki mbili zilizopita wakati mfungwa alipomuuliza Askofu Mkuu Delpini swali la kuhuzunisha: “Ulizungumza kuhusu msamaha, lakini nina tatizo: sina tena mtu wa kuuliza kwa sababu nilimuua. Nani anaweza kunisamehe?”
“Mtu aliyeuawa yuko mbinguni, aliye mbinguni huona mambo kwa macho ya Mungu na yuko tayari kusamehe”, alijibu askofu mkuu Delpini. “Uendelee kuomba msamaha kwa nguvu na utaona jinsi mwanga wa kirafiki, tabasamu, ambalo hutoka mahali ambapo hatuwezi kufikiria na kukuambia: umesamehewa. Kwa kifupi, kipande cha maisha ya Yesu kinaendelea hadi leo”.
Kwa njia hiyo utimilifu wa ujumbe wa Kristo ni moja wapo ya nguvu za kitabu cha Tornielli, alichosisitiza Kardinali Tolentino katika hotuba yake ya kuthaminiwa, iliyotanguliwa na makadirio ya kipande cha Nyuso za Injili, kipindi kilichobuniwa na Dr Tornielli mwenyewe na Lucio Brunelli iliyotangazwa na Rai wakati wa Pasaka. Kwa upande wa Kardinali Tolentino, alisema pia mtu wa herufi, mshairi, mtunzi wa tamthilia, hatuwezi kukabiliana na fumbo la umwilisho bila kutumia masimulizi. Mantiki nyuma ya kitabu ni ile ya kusema katika msingi wa Injili nne; kwa hiyo halikuwa swali la kujenga upya au si maisha ya Yesu bali ni kusimulia kwa msaada wa mpango wa masimulizi kupitia maneno ya kutafakari ya Papa Francisko, ambaye anaikaribia Injili kwa kuingia, kuihuisha na kuifanya iwe ya sasa.
Maisha ya Yesu yanaingia katika kile ambacho Ricoeur alikiita shughuli za uvumbuzi Mkuu wa Baraza aliendelea kusema, kuwa “Kwa kitabu hiki kitu tofauti kinafanyika, kwa uhakika kwamba kukutana na Yesu ni suala la moyo, la kuonekana, la hisia zinazotoka kwenye matumbo. Kwa upande wa Kardinali Tolentino pia sifa ya mawazo, ambayo Dr. Tornielli aliyesema katika utangulizi kama nguvu ya kuendesha simulizi yake: “Inaweza kuonekana kama udhaifu, lakini badala yake ni nguvu. Sio tena, kwa namna hiyo, fikira kama kichaa juu ya nyumba au crux theologorum, bali ni hali ya lazima ya kujua ukweli”. Ufahamu wa maovu na wema kamili hauwezi kupatikana bila kuwaza, Kadinali alisema, huku akirejea uthibitisho wa mtaalimungu wa Dominika Timothy Radcliffe: “Kikwazo kikubwa zaidi kwa Ukristo sio ulimwengu lakini umaskini wa ishara na simulizi.
Kwa hiyo matumaini kwamba kitabu hiki kizuri na cha lazima kinaweza kusomwa na watu wengi kwa njia ya kuimarisha uhusiano na Yesu, kumwelewa kutoka kwa mtazamo mpya. Matashi mema mengine muhimu, lililonukuliwa katika ukumbi na msimamizi wa Mkutano mwandishi wa habari wa Televisheni ya Italia (TV2000) Bi Cristiana Caricato, ni lile la mwandishi katika uwekaji wakfu wa kitabu kwa Joseph mdogo, mjukuu wake kwamba “Ni matashi mema kwamba anaweza kukutana na mhusika mkuu wa kitabu hiki na ili neema iumshukue ya kujiruhusu kuvutiwa naye”.