Viongozi wa dini ya kikristo na madhehebu mengine na Papa wameomba amani duniani!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Jumanne jioni tarehe 25 Oktoba kwa mara nyingine tena Vingozi wametia saini katika tamko la pamoja la wito wakiwa katika uwanja mbele ya magofu ya kale jijini Roma ambapo wamebainisha kwamba wakiwa wamekusanyika jijini Roma kama roho ya Assisi, wameomba amani, kulingana na mapokeo mbalimbali yao, lakini kwa makubaliano. Wao kama wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo na dini za ulimwengu, wanageukia ulimwengu kwa uangalifu na kwa viongozi wa Mataifa. Wanato sauti kwa ajili ya wasio kuwa na sauti, kwa wale wanaoteseka kutokana na vita, wakimbizi na familia za waathirika wote na waliokufa. Kwa imani thabiti wamethibitisha: “vita inatosha na migogoro yote. Vita huleta kifo na uharibifu tu, ni tukio lisilo na kurudia ambalo kwa wote ni wenye hasara. Silaha zisimame mara moja na kutangaza kusitisha mapigano kwa wote ulimwenguni. Mazungumzo yenye uwezo wa kuleta suluhishi za haki na za amani thabiti na kudumu yanapaswa kuanzishwa haraka iwezekanavyo kabla haijachelewa. Mazungumzo yamefunguliwe tena ili kufuta tishio la silaha za nyuklia".
Machungu ya Vita vya vya Pili vya Kidunia, Mataifa yaliweza kurekebisha mizozo mirefu ya migororo, kupitia mazungumzo ya pande nyingi, hadi kuzaa Shirika la Umoja wa Mataifa, ambalo ni la matokeo ya matarajio ambayo, leo hii kuliko wakati mwingine wowote ni jambo la lazima la amani. Viongozi hawa wanabainisha kwamba hakuna kupoteza kamwe kumbukumbu ya vita vya janga lile, ambavyo huzalisha kifo na umaskini. Kwa hiyo wamesema, wako njia panda ya kuwa kizazi kinachoacha sayari na ubinadamu unakufa, kinachokusanya na kufanya biashara ya silaha, kwa udanganyifu wa kujiokoa dhidi ya wengine, au badala yake kizazi kinachounda njia mpya za kuishi pamoja na sio kuwekeza katika silaha; hukomesha vita kama chombo cha kusuluhisha mizozo na kukomesha unyonyaji usio wa kawaida wa rasilimali za sayari.
Lazima kufungua mazungumzo ili kufuta hatari za silaha za kinyuklia.“Sisi kama waamini tunapaswa kufanyia kazi amani kwa njia zote zinazowezekana kwetu. Ni wajibu wetu kusaidia kuondoa silaha mioyoni na kutoa wito wa upatanisho kati ya watu. Kwa bahati mbaya, hata sisi wenyewe wakati mwingine tumejigawanya wenyewe kwa kutumia vibaya jina takatifu la Mungu: tunaomba msamaha, kwa unyenyekevu na aibu. Dini ni lazima ziendelee kuwa, chanzo kikuu cha amani. Amani ni takatifu, vita haviwezi kamwe! wamesisititiza.
Wakiendelea katika tamko hilo la pamoja wanabainisha: “Ubinadamu lazima ukomeshe vita au itakuwa vita ambayo itamaliza ubinadamu. Ulimwengu, nyumba yetu ya kawaida ya pamoja ni ya kipekee na sio yetu, lakini ni ya vizazi vijavyo. Kwa hivyo, tuwakomboe kutoka katika jinamizi la nyuklia. Tufungue tena mazungumzo mazito juu ya kutoeneza kwa silaha za nyuklia na uvunjaji wa silaha za nyuklia. Tuanze pamoja tena kupitia mazungumzo ambayo ni dawa inayofaa kwa upatanisho wa watu. Tuwekeze katika kila njia ya mazungumzo. Amani daima inawezekana! Tusifanye vita tena! Kamwe visifanyike dhidi ya kila mmoja!