Tafuta

Kozi ya usasisho kwa maprofesa wa seminari kuu kutoka makanisa mahalia ya Asia na Afrika katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana Roma Kozi ya usasisho kwa maprofesa wa seminari kuu kutoka makanisa mahalia ya Asia na Afrika katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana Roma 

Uzinduzi wa kozi ya 13 ya kusasisha maprofesa wa seminari kuu za makanisa mahalia

Maprofesa 22 wa Seminari Kuu kutoka mataifa 12 ya Asia na Afrika wanashiri kozi ya usasisho wa mafunzo mara baada ya mapumziko ya miaka miwili kutokana na janga la Uviko 19.Kozi hiyo inaendelea katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urubaniana Roma.Ilifunguliwa kwa Misa Takatifu na Askofu Mkuu Rugambwa.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Mara baada ya mapumziko ya miaka 2 kutokana na janga la Uviko -19,  imeanza kozi ya kusasisha mafunzo kwa maprofesa ambayo Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Waty limekuwa likiandaa tangu mnamo mwaka wa masomo wa 2012-2013 kwa Maprofesa wa Semina kuu, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana Roma na Jumuiya za Kipapa za Kimissionari. Kutokana na hilo hivi karibuni mnamo  Ijumaa tarehe 7 Oktoba 2022, Katibu wa Baraza hilo Askofu Mkuu Protase Rugambwa alifungua Kozi ya 13 ya Usasisho ambapo Maprofesa 22 kutoka mataifa 12 ya Asia na Afrika walishiriki na wanaendelea na kozi hiyo.

Maprofesa mapadre wanapata usasisho wa mada mbali mbali 

Kwa kawaida Maprofesa hao uhudhuria masomo katika madarasa hasa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, na kila mmoja kulingana na somo lake la kufundisha. Programu hiyo pia inajumuisha Semina mbali mbali zinazotlewa katika chuo Kikuu hicho cha kipapa kama vile ya Sinodi, baadhi ya makongamano kuhusu mada na siku tofauti za mafungo ya kiroho. Pamoja na uchunguzi wa kina wa baadhi ya vipengele vya taaluma mbalimbali kama vile (Taaalimungu, Falsafa, Sheria ya Kanoni ya Kanisa,  Misiolojia, yaani Utume wa kimisionari), Kozi hiyo pia ni fursa ya kubadilishana uzoefu juu ya hali halisi ya Seminari husika na Makanisa mahalia kwa wahusika wote wanaosasisha masomo yao. 

Mapadre waishi mang'amuzi ya kweli 

Kwa sababu hizo Askofu Mkuu Rugambwa katika ufunguzi huo  aliwahimiza mapadre kuishi mang’amuzi ya kweli ya ukuaji wa kiroho, kiakili, kijamii na kiutamaduni. Katika kipindi hicho cha kukaa Roma, kwa kuwasiliana na umoja wa Kanisa, kitawapa kwa dhati mwamko na nguvu mpya ya kutekeleza utume wao kwa ari mpya. Askofu Mkuu Rugambwa pia alisisitiza kwamba kozi hiyo ni kielelezo cha umuhimu ambao Ukasisi unahifadhi kwa ajili ya malezi ya kipadre na kuwajali daima waanzilishi na maprofesa wanaojitoa kwa ajili ya huduma hiyo adhimu.

Askofu Mkuu Protase Rugamba Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu
Askofu Mkuu Protase Rugamba Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu

Kwa sababu hiyo, wakati wa muhula kuanzia (Oktoba-Februari) unaendelea kutengwa kwa ajili ya kusasisha kozi kwa maprofesa ambapo kuanzia 2019, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu linahifadhi(katikati ya Februari hadi katikati ya Mei)mafunzo ya wafundaji, kwa programu maalum. Wakati wa Adhimisho la Ekaristi Takatifu kwa ajili ya uzinduzi wa Kozi ya masasisho  hayo kwa kuchukua dokezo la Sikukuu ya Bikira Maria wa Rozari, Katibu wa Baraza la Kipapa la Injilishaji wa Watu aliwaalika mapadre  hao kufuata nyayo za Mama yetu Bikira Maria, kwa maana ya kuwa chombo cha wokovu na wapenda sala.

KOZI YA USASISHO WA MASOMO KWA MAPROFESA WA SEMINARI KUU
20 October 2022, 15:23