Siku ya kimisionari ulimwenguni 23 Oktoba:nguvu za kimisionari zinapimwa kwa matendo
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Nguvu ya kimisionari ya Kanisa Katoliki inapimwa kutokana na idadi ya shughuli zake katika nyanja zake kuanzia elimu hadi kufikia afya na shughuli nyinginezo. Na katika kutazama takwimu iliyochapishwa katika fursa ya maadhimisho ya Siku ya Kimisionari Duniani Dominika tarehe 23 Oktoba 2023, inabainisha wazi kuwa Kanisa Katoliki linasimamia elimu kuanzia shule za awali 72,785 duniani zinazohudhuriwa na wanafunzi 7,510,632; shule za msingi 99,668 kwa wanafunzi 34,614,488; Shule za sekondari 49,437 kwa wanafunzi 19,252,704. Pia inawafuatilia wanafunzi 2,403,787 wa shule za sekondari na wanafunzi 3,771,946 wa vyuo vikuu. Na tena, katika nyanja ya kiafya, Kanisa linajikita na juhudi zake kwa hospitali 5,322, zahanati 14,415, hospitali za watu wenye ukoma 534, nyumba za wazee 15,204 za, wagonjwa wa kudumu na walemavu, 9,230, vituo vya watoto yatima 10,441, shule za awali 333, vituo vya ushauri na vituo vya elimu vipya vya kijamii na taasisi nyingine 34,291.
Siku ya utume au Kimisionari duniani ni yenye ladha maalum, ambayo imeaadhimishwa 23 Oktoba kwa kuomgoza na kauli mbiu: “Mtakuwa mashahidi wangu". Kwa mwaka huu pia ni matukio matatu ambayo yanatazamwa: kuadhimisha miaka 400 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Kipapa la Propaganda Fide, kumbu kumbu ya miaka 200 ya Shughuli za kwanza za Kipapa za Kueneza Imani na hatima kumbu kumbu ya miaka 100 ya huduma za kipapa zilipogeuka kuwa shughuli za kipapa. Kwa maana hiyo ni mwaka ambao unaishia kwa kuona tukio la utafakatifu kwani mwezi Mei mwaka huu alitangazwa mwenyeheri Pauline Jaricot, ambaye ni mwasisi wa shughuli za Kueneza Imani, yaani kazi ya kwanza ya umisionari. Na ilikuwa hasa Kazi ya Kueneza Imani ambayo katika mwaka 1926 ilipendekezwa kwa Papa Pio XI na kupanga siku ya kila mwaka kwa ajili ya utendaji wa kimisionari wa Kanisa zima. Ombi hilo lilikubaliwa na tayari mwaka huo Siku ya kwanza Duniani iliadhimishwa, ambayo ilifanyika kwa njia hiyo katika kila Dominika ya mwisho wa Oktoba, ambao ni mwezi wa umisionari.
Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari yana jukumu la kusaidia kifedha shughuli za kimisionari, kwa kuanzia na wazo la Mwenyeheri Pauline Jaricot la kuwashirikisha waamini wa kawaida katika kazi ya kimisionari. Kwa sasa kuna Mashirika Kipapa manne ya Kimisionari, ambayo yote yalianzishwa katika karne ya 19 ambayo ni Shirika la Utoto Mtakatifu lililoanzishwa mwaka 1843 nchini Ufaransa na Monsinyo Forbin-Janson; Shirika la Kipapa la Kueneza Imani, lililoanzishwa na Pauline Jaricot; kazi ya kimisionari ya Mtakatifu Petro Mtume, lilizaliwa mnamo mwaka 1889, kwa mwamko wa Askofu Binamu wa Nagasaki, kwa ajili ya malezi ya mapadre na kutekelezwa kwa vitendo na Stefanie na Jeanne Bigard; na hatimaye Umoja wa Kimisionari wa Kipapa ambao ni Chama cha Wakleri, Watawa na Walei ili kuamsha shauku ya utume ndani ya Kanisa. Leo hii utume wa kimisionari umebadilika sana. Nchi za Magharibi zina bidii kidogo ya umisionari. Hata hivyo, kuna majimbo mahalia yanahusika zaidi katika eneo hilo, uwepo wa nguvu zaidi wa maelekezo ya kitaifa ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa ya kidigitali, kuna familia nyingi zaidi za kimisionari.
Mashirika ya Kipapa ya Kimissionari yana jukumu la kuendelea kuliweka hai wazo la kimisionari, lenye mielekeo 120 ya kitaifa na mipango mingi. Kulikuwa na kupungua kwa makusanyo ya matoleo kwa sababu ya janga la uviko -19 mnamo 2020, baadaye uafadhali ukawepo katika sehemu ya kipindi cha mwaka 2021, wakati takwimu za mwaka 2022 zitaonesha zaidi kulingana na athari za mfumuko wa bei wa sasa. Kuna njia ambayo tayari imeoneshwa na Sinodi za Afrika ambapo inaoneshwa kuelekea katika kujifadhili wenyewe kwa Makanisa mahalia. Sio kila mahali hiiko hivyo. Kwa mfano, Sudan Kusini ambayo ni nchi yenye mahitaji makubwa au kuna jumuiya za Wakristo katika nchi ambazo wao ni wachache huko (Bangladesh, Pakistan, India) na wanahitaji msaada bila kujali masuala yote ya kisiasa, kwa sababu kuwa wachache maskini, kwa sababu wao ni wachache na nchi maskini.
Mzunguko wa Kikanisa unategemea Baraza la Kipapa la Uinjilishaji ni jumla ya 1,118, kulingana na tofauti za hivi karibuni ambazo zilizorekodiwa. Hali fulani za kikanisa zilizokabidhiwa kwa Baraza hili zinapatikana Afrika (518) na Asia (483), Amerika(71) na Australia(46) wanafuata. Wakatoliki ulimwenguni wamekua katika mabara manne, ukiondoa Australia. Kufikia tarehe 31 Desemba 2020, Wakatoliki duniani walikuwa watu 1,359,612,000 na ongezeko la jumla la 15,209,000 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Jumla ya idadi ya Maaskofu duniani imepungua kwa kitengo 1 tu, na ni sawa na 5,363. Kuna mapadre 410,219 duniani, 4,117 chini ya mwaka jana. Watawa wa kiume wasio makuhani waliongezeka kwa vitengo 274, na kufikia idadi ya 50,569.