Tafuta

Mwezi wa Kimisionari na mwezi wa Maria. Mwezi wa Kimisionari na mwezi wa Maria. 

Siku ya Kimisionari ulimwenguni 2022:Utume ni ule ule bali tofauti wa mitindo mipya

Katika mahojiano na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari katika fursa ya Siku ya Kimisionari duniani Oktoba 23amesema:“Utume unaendelea kuwa jukumu la Kristo la kutangaza Injili na kuunda jumuiya mpya za Kikristo.Mfumo ambao kwa haya yote yanatambulika leo hii yanabadilika.Kwanza kuna uwepo mkubwa zaidi wa walei pia wa familia katika ulimwengu wa wamisionari".

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Ni wakati muhimu sana wa mwezi huu wa Oktoba ambao unajikita zaidi katika  roho ya kimisionari. Na Siku ya Kimisionari  Duniani itaadhimishwa Diminika tarehe 23 Oktoba, ambayo mwaka huu inaongozwa na mada ya “ Mtakuwa mashahidi wangu. Katika ujumbe wa tukio hilo, Papa Francisko alikumbuka kwamba Kanisa ni la kimisionari kwa asili. Mwaka huu, Papa aliandika kwamba, Siku hii inatupatia fursa ya kuadhimisha baadhi ya matukio muhimu kwa maisha na utume wa Kanisa, kwanza kabisa kwa miaka 400 iliyopita, illianzishwa Shirika la Propaganda Fide ambalo leo hii linaitwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na kwa miaka 200 iliyopita, zilianzishwa Shughuli ya Kueneza Imani. Katika kufafanua jinsi ambavyo utume unazidi kubadilika, Vatican News ilifanya mahojiano na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari Askofu Mkuu  Giampietro Dal Toso na Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu ambaye alisema kwamba leo hii utume unabadilika kwa sababu si kuzungumza  tena kutoka Kaskazini hadi Kusini lakini  ni kwa digrii 360, akiongeza kusema kwamba katika wakati wetu utume: “lazima upenye mazingira ya kiutamaduni tofauti na yale ya miaka hamsini iliyopita”.

Utume ni Agizo la Bwana wa Kanisa lake

Na akifafanua kuhusu utume alisema utume ni agizo ambalo Bwana ametoa kwa Kanisa lake na ambalo, kwa karne nyingi, Kanisa limetekeleza. Mabadiliko ambayo  leo hii yapo  yanahusishwa na hali, hasa hali za kiutamaduni. Na njia ambayo utume unafanywa  pia unabadilika. Utume unaendelea kuwa jukumu la Kristo kutangaza Injili na kuunda jumuiya mpya za Kikristo. Njia ambayo haya yote hufanyika leo yanabadilika. Kwanza kabisa, kuna uwepo mkubwa zaidi wa walei na pia wa familia katika ulimwengu wa kimisionari. Kwa upande mwingine, ile ya makuhani na ya kitawa imepunguzwa. Na ni tofauti sio tu katika nchi za Magharibi. Pia ni tofauti katika maeneo ya utume, kwa mfano  utamaduni wa kidijitali unabadilisha njia ya maisha katika maeneo yote. Pia ni utume unaobadilika kwa maana kwamba, hata katika maeneo yenye mapokeo marefu zaidi ya Kikristo, kuna haja ya kuanzisha tena na kuhamasisha upya historia hii kwa tangazo jipya la imani.

Ulimwengu wa kidijitali

Askofu Mkuu Dal Toso akijibu ni jinsi gani ya kutekeleza hayo mbele ya ulimwengu wa kidijitali amesema kwamba huu ni ulimwengu ambao wamegundua hitaji la kuwepo zaidi na zaidi. Juhudi za kuwepo katika mazingira haya ya kidijitali zinaongezeka miongoni mwa Idara zao120 za kitaifa. Kwa kutoa mifano kadhaa alisema  kutoka katika video fupi zinazofanywa hadi sala, au katika nchi zingine na hii inahusu ulimwengu wa vyombo vya habari , kwa maana wanaona jinsi radio za Kikatoliki zinavyofanya huduma kubwa katika uinjilishaji kwa sababu mara nyingi ndio njia pekee ya kuwafikia waamini. Ni muhimu kutambua hitaji hilo la  uwepo katika ulimwengu wa kidijitali  na sio wa kuamua, lakini inaweza kuwa msaada wa kufikiria, sababu ya kutoa fursa za kukutana na Bwana.

Propaganda Fide kwa miaka 400 imeongoza shughuli za kimisionari

Propaganda Fide au kwa maana nyingine Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, katika miaka yake 400 ya historia, imekuwa na inaendelea kuwa na nafasi kubwa katika kusindikiza na kuratibu kazi kubwa ya kimisionari na Makanisa mahalia, pamoja na taasisi kuu za kidini za kimisionari. Katika miaka hii 400, Propaganda Fide kwa namna fulani imeongoza shughuli ya umisionari wa Kanisa. Mashirika ya Kipapa  ya Kimissionari yameunga mkono kazi hii kuu ya  Baraza hilo kwa sura mbili. Kwanza kabisa, kwa namna ya uhuishaji wa kimisionari, kuwahamasisha watu wote wa Mungu kwa umuhimu wa utume na kusaidia kifedha shughuli za kimisionari. Hivyo kusaidia kuundwa kwa majimbo na seminari, nyumba za watawa na monasteri, nyumba za malezi ya makatekista. Mashirika ya Kipapa ya  Kimissionari kwa upande wake, yanaweza kufanya kazi hii kutokana na kuungwa mkono na watu wengi duniani.

Askofu Mkuu Giampiero Dal Toso,Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari na Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu
Askofu Mkuu Giampiero Dal Toso,Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari na Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu

Katika mahojiano hayo hawakukosa kutazama hali ya Ukraine ambapo akijibu mwelekeo gani wa Mashirika ya Kipapa ya Kimissionari yanaweza kusaidia watu wa Ukraine alisema, katika nchi hiyo yenyewe Ukraine sio eneo la umahiri wao  kwa sababu iko chini ya uwezo wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki. Kilichotokea, ni kwamba idara kadhaa za kitaifa, sio tu barani Ulaya, bali zote  zilihimizwa kutoa msaada, hasa katika awamu ya kwanza, wakati kulikuwa na wimbi la kwanza la wakimbizi. Na waliunga mkono hatua ya Makanisa mahalia huko Poland, Slovakia, Hungaria na Romania. Kwa hiyo ni kujitoa kuunga mkono hatua ya Kanisa mahalia kuwasaidia wakimbizi.

23 Oktoba siku ya Kimisionari ulimwenguni:’Mtakuwa mashuhuda wangu’

Ikumbukwe kwamba ‘Ninyi mtakuwa mashuhuda wangu’, ndiyo kauli mbiu inayoongoza  mwezi Oktoba wa kimisionari iliyotolewa katika kifungu cha Matendo ya mitume (Mdo 1, 8) Ni ushauri ambao bado ni muhimu  kwa sasa na unatualika kutangaza Habari Njema hadi miisho ya dunia na kueneza upendo wa Mungu kupitia neno na matendo. Mwaka huu pia uliadhimishwa siku ya kutangazwa Mwenyeheri mwanzilishi wake Pauline Jaricot, iliyofanyika tarehe 22 Mei 2022 na kuzaliwa kwa Kazi ya Kueneza Imani, inayojulikana leo kama Utume ambapo imetimiza miaka 200 ilipoanzishwa huko Lyon nchini Ufaransa.  Siku ya kimisionari  Duniani itaadhimishwa tarehe 23 Oktoba, ambapo parokia za  sehemu mbalimbali za dunia zitashiriki kuandaa siku hiyo.

Siku ya Kimisionari duniani 23 Oktoba
19 October 2022, 15:29