Papa Francisko amekutana na Rais Macron kwa mara ya tatu!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 24 Oktoba 2022, amekutana mjini Vatican na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, Bwana Emmanuel Macron akiwa na Mkewe Brigite. Na mara baada ya mkutano huo, Rais Macron amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Fursa ya Mkutano huo imejitokeza kutokana na Bwana Macron kuudhuria Mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kuhusu ‘kilio cha Maskini’ ambao utahitimishwa kwa sala ya pamoja na viongozi wa dini mbali mbali kwa uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko katika magofu ya jiji la Roma kuombea amani ya Ukraine na ulimwengu mzima. Kwa hiyokatika fursa hiyo ni kwa maana ya tatu ya Rais Macron tangu aanze kutawala nchi anakutana na Papa Francisko.
Wakiwa pamoja na mazungumzo na Katibu wa Vatica, wametazama pamoja masuala yenye tabia ya kimataifa kuanzia na mgogoro wa Ukraine, na hasa umakini kwa hali halisi ya msaada wa kibinadamu. Kwa mazingatio hayo muhimu, wamejikita vile vile kutazama kanda ya Caucasus, Nchi za Mashariki na bara la Afrika.