Tafuta

Papaalikutana na Waziri Mkuu wa  Lussemburgo Bwana  Bettel Jumamosi 29 Oktoba 2022 Papaalikutana na Waziri Mkuu wa Lussemburgo Bwana Bettel Jumamosi 29 Oktoba 2022 

Papa amekutana na Waziri Mkuu wa Lussemberg Bwana Xavier Bettel

Baba Mtakatifu Francisko alikutana mnamo Jumamosi Oktoba 29 Waziri Mkuu wa Lussemburg na baada kukutana naye akakutana na Makatibu wa Vatican. Katika Mazungumzo yao yalijikita kuhusu uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizo mbili na masuala ya Ulaya na kimataifa katika hali halisi ya vita nchini Ukraine na suala la uhamiaji na ukimbizi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi 29 Oktoba 2022, Baba Mtakatifu Francisko alikutana mjini Vatican na Waziri Mkuu wa Lussemburg, Bwana Xavier Bettel, ambaye mara baada ya mkutano huo alikutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Katika kuendelea na mazungumzo yao walionesha kupendezwa uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili na walisisitizia  masuala mengine yanayo wahusu pamoja  kwa namna ya pekee umakini wa uhusiano kati ya  Kanisa na Serikali.

Mazungumzo yao yakiendelea kwa namna ya pekee walitazama vita nchini Ukraine na jitihada zao katika kutafuta amani. Vile vile masuala mengine yenye tabia ya Ulaya na kimataifa, miongoni mwake kuhusu mgogoro wa uhamiaji na ulazima wa kutoa usaidizi kwa wahamiaji na wakimbizi.

30 October 2022, 11:40