Papa akutana na Waziri Mkuu wa Montenegro
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Mazungumzo kati ya watendaji wa kisiasa, hali ya nchi za Balkan na kujiunga na Umoja wa Ulaya ni baadhi ya masuala yaliyozungumziwa katika Sekretarieti ya Vatican Jumatatu tarehe 10 Okotba 2022 na Waziri Mkuu wa Montenegro, Bwana Dritan Abazović, yaliyopokelewa asubuhi hiyo katika mkutano na Papa Francisko kwenye Jumba la Kitume.
Mara baada ya mazungumzo na Papa yaliyochukua takriban dakika 25, Waziri Mkuu alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Katika mazungumzo kama ilivyo tolewa maelezo kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, vimebainisha kwamba wakati wa mazungumzo yao ya dhati katika Sekretarieti ya Vaticanpongezi ziliolewa kutokana na uhusiano mzuri wa nchi mbili uliopo na nia ya kuendeleza ushirikiano katika sekta zenye maslahi ya pamoja. Zaidi ya hayo, mchango chanya wa jumuiya ya Kikatoliki kwa jamii ya Montenegro ulisisitizwa.
Wakiendelea na mazungumzo hayo walizingatia ukweli wa ndani wa nchi, wakirejea haja ya mazungumzo jumuishi kati ya wahusika wote wa kisiasa kwa manufaa ya wote ya Montenegro. Hatimaye, ripoti imebainisha kwamba walitazama baadhi ya masuala ya kikanda ikiwa ni pamoja na hali ya nchi za Balkan Magharibi na kujiunga kwao kwa Umoja wa Ulaya.
Wakati wa ugeni huo ukiwa katika jumba la kitume walipata nafasi ya kubadilishana zawadi, Papa Francisko alimpatia Waziri Mkuu baadhi ya nyaraka za Kipapa, kama vile Ujumbe wa Amani wa mwaka huu, Hati ya Udugu wa Kibinadamu, kitabu cha Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV. Mbali na hilo pia kuna tawi la mzeituni wa shaba na kitabu chenye kichwa “Hebu tuote”, kwa kujitolea. Na Abazović alijibu zawadi hiyo kwa kumpatia Papa Francisko kitabu chake cha hivi karibuni kilichochapishwa huko Balkan, mnamo 1494.