Tafuta

Papa Yohane  XXIII Papa Yohane XXIII   Tahariri

Mtaguso na Kanisa, “Mama wa upendo kwa wote”

Miaka sitini ya Mtaguso wa II wa Vatican, mchakato wa safari inayoendelea.

ANDREA TORNIELLI

“Kanisa Katoliki, kwa kuinua mwanga wa ukweli wa kidini kwa njia ya Baraza hili la Kiekumene linataka kujionesha kuwa mama mwenye upendo wa wote, mwema, mvumilivu, mwingi wa huruma na wema…” Imepita miaka sitini tangu wakati Yohane XXIII alipozindua Mtaguso wa II wa Kiekumene wa Vatican. Katika mazungumzo ya dakika 37 kwa lugha ya kilatino, mnamo tarehe 11 Oktoba 1962, Papa mzee  mbele ya washiriki  maaskofu wapatao  2449  waliokuwa wameunganika pamoja na umati mkubwa ambao uliwaona kwenye msululu  katika maandaano marefu katika uwanja wa Mtakatifu Petro, ulikuwa unapelekea utimilifu wa ndoto na msukumo uliofuatiliwa kwa bidii.

Papa Roncali asingeweza kupeleka meli peke yake ambayo ilikuwa inaanza siku hiyo bandarini. Ni Yeye tu kwa hatua ya utulivu wa maamuzi na mkulima na uwezo wa kufahamu mambo chanya ya alama za nyakati, aliweza kuthubutu sana, kuchukua uamuzi ambao watangulizi wake waliacha. Ni Yeye tu aliweza kufungua mtaguso. Ni Yeye akiafuatwa na Paulo VI aliweza kupeleka mbele utimilifu wa kazi ya Mtaguso wa II wa Vatican, kwa kufanikiwa katika muujiza wa kuwa na hati zote za mitaguso iliyopigiwa kura karibu kwa moyo mmoja. Papa Montini angeweza kuteseka baadaye katika makumi ya miaka  ijayo kuhusu upinzani ule wa ndani na migawanyiko ile katika “ushahidi wa uvumilivu” ili kuweka usukani wa Mtubwi wa Petro  kuwa thabiti na ili kuepuka kutumbukia kwenye kina kifupi kutokana na kurushwa kwa nyuma au kugonga miamba kutokana na kwenda mbele bila kudhibitiwa.

Miaka 60 baadaye, safari ile bado haijatimilizika. Papa Francisko, akiwa mstari wa mbele kati ya wafuasi wa Petro, katikati ya karne ambaye hakuishi moja kwa moja kwa tukio hilo, kama Baba wa Mtaguso au kama Mtaalimungu, kiukweli anatembea kwenye njia hiyo. Anafanya kwa kukumbusha kuwa lengo moja tu ambalo Kanisa linaishi ni tangazo la Injili kwa wanawake na wanaume leo hii. Majisterio (Mafundisho) ya sasa ya Askofu wa Roma, yanaangazwa katika maneno yaliyotamkwa kwa dhati miaka sitini iliyopita na Papa Yohane: Kushuhudia uso wa Kanisa, mama mwenye upendo kwa wote, mwema, mvumilivu, mwingi wa huruma na wema yaani mwenye uwezo wa ukaribu na huruma, mwenye uwezo wa kusindikiza aliye katika giza na katika hitaji. Kanisa ambalo halijiaminishi peke yake na halifuati nguvu za kidunia au umuhimu wa vyombo vya habari, lakini kwa unyenyekevu linajiweka nyuma ya Bwana wake, likimtumaini Yeye tu.

Papa Mwema Yohane XXIII
11 October 2022, 16:08