Maandalizi ya Noeli:mapambo ni zawadi kutoka Friuli na Abruzzo!
Na Angella – Rwezaula;– Vatican.
Pango ambalo litapambwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, ambalo litakuwa la miti litatoka eneo la Sutrio katika wilaya ya Udine mkoa wa Friuli Venezia-Giulia, Italia kwa ajili ya siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Wakati huo huo, mti mrefu wenye mita 30 utatoka eneo la Rosello huko mlima wa Abruzzo wenye wakazi 182 tu. Hata kwenye ukumbi wa Paulo VI Vatican utapambwa pango mwaka litakalo tolewa zawadi ya serikali ya Guatemala. Huu ni uwakilishi wa maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Bwana katika Familia Takatifu na Malaika watatu. Vyote vimeandaliwa kwa kutumia ufundi wa mikono kulingana na tamadani za Guatemala kwa nguo ndefu zenye rangi, mahali ambapo rangi ya dhahabu ndio itatalawa sana katika sanamu za miti.
Uzinduzi tarehe 3 Desemba 2022
Kiutamaduni, uzinduzi wa Pango na kuwasha taa za mti wa Noeli,ufanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambapo mwaka huu itakuwa mnamo Jumamosi tarehe 3 Desemba saa 11.00 jioni majira ya Ulaya. Afla itaongozwa na Kardinali Vérgez Alzaga, Mwenyekiti wa Utawa wa Serikali ya mji wa Vatican kwa uwepo wa Sr. Raffaella Petrini, Matibu Mkuu msaidizi wa utawala huo. Asubuhi hiyo wawakilishi kutoka Sutrio, Rosello na Guatemala watakutana na Baba Mtakatifu kwa ajili ya kuwakilisha zawadi zao rasmi.
Mapambo ya mti, ambayo yataoneshwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro yatatengenezwa na vijana wa kituo cha makazi cha ukarabati wa akili "La Quadrifoglio". Ni kituo cha huduma ambapo wageni wake, waliojumuishwa kikamilifu katika mfumo wa kijamii wa Rosello, wanaweza kujihusisha katika njia ya mtu binafsi ya ukarabati, kuanzia uchunguzi na kuzuia dalili zisizo na kazi kutokana na ugonjwa wao kufikia uhuru kamili wa maisha ya kila siku. Mti mrefu uliopambwa na pango vitabaki kwenye maonesho hadi mwisho wa kipindi cha Noeli ambacho kitamalizika na sikukuu ya Ubatizo wa Bwana, mnamo Jumapili tarehe 8 Januari 2023.