Dk.Ruffini:Kwa muda mrefu Kanisa limekuwa mtandao tangu siku ya Pentekoste!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumamosi tarehe 22 Oktoba 2022, ulifanyika mkutano wa vijana wainjilishaji wa kidigitali ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ushirikiano na sekretarieti kuu ya Sinodi. Kati ya watoa mada alikuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini. Katika hotuba yake alisema kuna neno, kitenzi ambacho kinaelezea vizuri vijana, kukutana tena na sio hapo lakini pia kwa mbali na kushirikishana. Hii ni kushirikishana mawazo na mipango, hata mawazo tofauti, ndoto, wema, furaha na wasiwasi; matumaini; uhakika na hofu na nyakati za maombi. Hivi ndivyo mtandao unavyotumika, kuwasiliana; kuhusiana na ili kusikilizana. Na kuamsha hamu ya kukutana ana kwa ana; kuelewa matarajio ya watu, ugumu, matokeo.
Kanisa ni mtandao tangu Pentekoste
Kanisa lilikuwa mtandao wa muda mrefu na kabla ya mtandao wa sasa kuitwa mtandao ambapo uliitwa tangu siku ya Pentekoste na kuendelea kutangaza Injili kwa watu wote, na kuwafikia watu popote walipo, alibainisha Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Kwa kuzungumza lugha wanayozungumza, na kusikiliza lugha wanazozungumza. Hii ndiyo sababu haiwezekani kuzika zawadi za enzi ya kidijitali, na ndivyo ilivyo kwamba hatuwezi kuwa na tabia kama mtu anayezika talanta. Kinyume chake, ni lazima tuzitumie vizuri. Dk. Ruffini alisisitiza kwamba ikiwa Kanisa likihatarisha kupoteza uwezo wa kusikiliza, , uwezo wa ushirikishana, wa umoja, wa kupenda; na ikiwa linahatarisha kutembea hapo hapo au hata kurudi nyuma; lakini shughuli ya kila mbatizwa si kwenda mbele zaidi, kugeuza kisogo upande mwingine, bali ni kugundua tena na kushuhudia uzuri wa Injili. Na kwa kutumia mtandao kuwakusanya wanaume na wanawake wenye mapenzi mema, mitandao ya kijamii inaweza kuwa njia ya kushiriki historia na matendo, imani na mahusiano na mipango, mashaka na mapendekezo.
Muujiza wa Pentekoste ni wa sasa
Na ikiwa wakati fulani wa kisasa wanaonekana kuwa na roho ya Babeli; ikiwa badala ya kujenga upya ukweli wa kuwa wanachama wa mtu mwingine, wanahatarisha kujenga kingamwili ya fumbo, ambalo halijumuishi bali linabatilisha utambulisho wa mtu binafsi; au wanakuwa vyombo vya utengano badala ya muungano, wa kueneza uongo badala ya ukweli, wa kuchanganyikiwa badala ya ujuzi, jibu letu haliwezi kuwa kukimbilia mahali pengine. Badala yake ni juu yetu kuonesha kwamba njia nyingine inawezekana kila wakati, hata hapo, sasa, katika ulimwengu wa kidijitali. Muujiza wa Pentekoste ni wa leo hii na daima na ni mwitikio wa Kikristo kwa hatari hiyo ambayo inajaribu kurudia na maana ambayo ni ya kale na ina mizizi yake katika dhambi ya asili. Kwa njia hiyo Dk Ruffini alisisitiza kwamba ni juu yetu kulipatia Kanisa kama mahali pa umoja na ushirikiano kati ya watu; ni juu yetu sio kuwaainisha watu kwa msingi wa uwezo wao wa ununuzi, lakini kwa msingi wa uwezo wao wa kutoa; na kuwarudisha kwenye ukweli wa kukutana, katika uzuri wa umoja. Ni lazima kujifunza kutumia mitandao ya kijamii kwa kushiriki zaidi ujirani kwa wote. Katika mitandao, na mahali pa vitongoji na kutoa ushuhuda wa kuwa kwetu Kanisa.
Leo Kanisa linahitaji kutoka nje ya kuta zake
Dk Ruffini aliendelea kueleza kuwa leo kuliko wakati mwingine wowote ni wakati wa Kanisa la kutoka nje ya kuta zake, na sio kufikiria kutulia tu, bali wenye kuwa na nguvu; ni wakati wa kujenga ushirika kupitia zana zote za mawasiliano na kuvumbua njia za ushirikiano. Ni wakati wa kutoa uhai kwa mipango shirikishi ya kuchunguza, kusafisha, kuainisha tabia ya ziada ya kimawasiliano ya mwanadamu na kushuhudia Kanisa kama fursa ya uhusiano mwema kati ya watu, na kati ya watu na maeneo wanapokaa. Lazima kuanzisha michakato, kuhimiza ujenzi wa mtandao kulingana na njia tofauti ya Kikristo ya kutumia wavuti. Kupitishwa kutoka kwa jamii kwenda kwa jamii. Kwa jumuiya ya jumuiya zenye uwezo wa kukuza wema, na wa kuishirikisha. Kwa kutoa mifano halisi, Dk. Ruffini aidha alisema, hii ndiyo maana ya Sinodi ya kutembea Pamoja na kupanga pamoja. Ndiyo mantiki ya Petro na Paulo badala ya ile ya Romulus na Remus au ya Kaini na Abeli.
Lazima kutafuta mpango wa udugu badala ya migogoro
Mpango wa udugu badala ya ule wa migogoro. Kwa njia hiyo ni vema kusali kwa pamoja ili mchakato wa safari ya Sinodi ambao huko mwanzoni uweze kuendelea na kutoa matunda. Kwa kuhitimisha aliomba kusali kwa kutumia maneno kwenye mitandao ya kijamii ili yajenge mtandao huo unaounganisha na usiogawanyika. Kama vile Gianni Rodari, mwandishi maarufu wa Italia alivyandika kwamba: “Tunayo maneno ya kuuza, maneno ya kununua, maneno ya kutengeneza maneno. Twende tukaangalie pamoja maneno ya kufikiria. Tuna maneno ya kulia, maneno ya kunyamaza, maneno ya kufanya kelele. Twende tukaangalie pamoja maneno ya kusema. Tuna maneno ya kujifanya, maneno ya kuumiza, maneno ya kuchekesha. Twende tukaangalie pamoja maneno ya kupenda”. Na hivyo Tusali ili kupata pamoja maneno ya kufikiria, kusema na kupenda, alihitimisha Dk. Ruffini.