Kard.Semeraro:maisha ya Mwenyeheri Maria Costanza yalikuwa Ekaristi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wamonaki themanini, Ndugu wadogo Wafransiskani thelathini, mapadre sitini, maaskofu tisa na makadinali wawili na waamini wengi kutoka eneo la Fabriano, katika eneo la mkoa wa Marche, Italia walikuwapo katika maadhimishi ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu, Kardinali Angelo Semeraro mara baada ya kutoka Mjini Vatican, katika Misa ya kutangazwa kwa watakatifu wawili Scalabrini na Zatti. Kwa maana hiyo akiwa pamoja na Askofu wa Fabriano Matelica, Askofu Francesco Massara, Dominika jioni, tarehe 9 Oktoba 2022 alitangazwa Sr Maria Costanza Panas, Mklara mkapuchini katika Kanisa kuu la Mtakatifu Venance k uwa Mwenyeheri. Kardinali Semeraro katika mahubiri yake alikumbuka mtawa huyo katika nuru ya Injili ya Dominika iliyosimulia habari ya kuponywa kwa watu kumi wenye ukoma, kati ya hao ni Msamaria pekee ndiye anayerudi kwa Yesu akiwa na roho ya shukrani na shauku ya kumjua yule aliyemrejeshea afya kutokana na maradhi si ya kimwili tu, lakini pia kijamii.
Maria Costanza Panas alizaliwa 1918-1963
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Agnese Pacifica Panas, na ambaye alizaliwa katika eneo la Belluno mnamo mwaka 1896, akasomeshwa na watawa wa Kanosa. Shauku yake ilikuwa kuingia miongoni mwa Maklara, Maskini Wakapuchini wa Fabriano, jiji maarufu la utengenezwaji wa karatasi nzuri na ambao alikuwa ameanzisha kuandikiana barua. Alivaa nguo za kitawa kwa kufunga nadhiri mnamo tarehe 18 Aprili 1918 na kuchukua jina la Sr. Maria Costanza. Maandishi yake ni pamoja na yale ya mazoezi ya nidhamu kali, vitabu vidogo mbalimbali vya kutafakari na mashairi mengi. Akiwa amepooza kitandani tangu mwaka 1960, alitoa mateso yake hasa kwa ajili ya Papa Yohane XXIII na kwa ajili ya mafanikio ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatikani. Kifo chake kilimjia mnamo tarehe 28 Mei 1963 na Mchakato wa kutangazwa kwake kuwa mwenyeheri ulianza mnamo tarehe 10 Oktoba 1983, miaka ishirini baada ya kifo chake. Masalia yake yanatunzwa katika nyumba ya watawa ya Waklara Maskini Wakapuchini huko Fabriano nchini Italia. Baba Mtakatifu Francisko alimtangaza kuwa Mtumishi wa Mungu tarehe 10 Oktoba 2016.
Ibada ya kushukuru ni Ekaristi
Kardinali Semeraro pia alikumbusha kwamba katika utamaduni wa Kiyahudi wa wakati wa Yesu, Msamaria hakuwa elekezo la ukabila tu, lakini hata jina la mgawanyiko, adui na hata mtu hasiye amini. Kwa kuzingatia maana hiyo, mtazamo wa Msamaria wa huruma ya Yesu ulidhihirishwa kwake na ambao ni thamani zaidi. Kardinali Semeraro alisisitizia juu ya mwenendo wa Mungu ambao ulimpendeza kwa kumwona Msamaria aliyerudi kushukuru. Katika muktadha huo, ni bora kujiuliza ni aina gani ya shukrani ambayo Bwana anataka kutoka kwetu? Labda ni ile ya kukaa katika miguu ya Yesu. Na ndiyo ilikuwa ibada ya shukrani yaani Ekaristi kwa maisha yake hapa duniani ya Mwenyeheri Maria Costanza Panas na ambaye alikuwa ni mkuu wa Monasteri hadi kifo chake, mwitikio wake kwa wito wa utawa na hali yake ya kiroho.
Altare ni shule ya fadhila zote
Katika maandishi yake aliandikia kwamba: “Altare ni shule ya fadhila zote, mahali ambapo, pamoja na Yesu, Maria Mama na Mama mwingine Kanisa, hupatikana. Na tena: “Heshima ya Kanisa ni utakatifu wa watoto wake [...] Iweni watakatifu kuwa binti wa kweli wa Kanisa, kuliheshimu na kulipenda Kanisa, ambalo ni upendo mkuu, huruma tele ya Moyo wa Yesu wetu (Ukurasa 751-752)”. Kardinali alisema kujitoa na kuamini kwake ilikuwa ndiyo programu ya maisha ya Maria Costanza. Mfano unaotuaeleza kwamba ni shukrani tu ambayo hutoa ukamilifu kwa maisha yetu.
Muujiza
Maandishi kutoka Baraza la Kipapa la Mchakato wa kutangazwa mtakatifu yalitiwa saini kufuatia kutambuliwa kwa muujiza unaohusu uponyaji wa mtoto mchanga kutoka Mtakatifu Severino huko mkoa wa Marche, aliyekuwa anasumbuliwa na mateso makali ya umbu kutokana na upungufu wa damu na kutokwa na damu katika ubongo; viungo vingi kushindwa kufanya kazi. Kiukweli mnamo 1985, walikuwa ni babu na bibi wa mtoto huyo waliomba maombezi yake. Mtoto aliyeponywa, ambaye sasa ni mtu mzima,alikuwepo katika Kanisa Kuu la kutangazwa Mwenheri hyo Mtawa Mkapuchini.