Kard.Parolin:uongozi wa wanawake unazaliwa kutokana na mafunzo jumuishi na ubora
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Mkutano ulioandaliwa na Caritas Internationalis, tarehe 27 na 28 Oktoba 2022 katika makao makuu ya UNESCO huko Paris, kwa kuongozwa na mada ya uongozi wa kike, Jambo la kwanza ambalo Kardinali Pietro Parolin katibu wa Vatican alifanya ni kuomba serikali za kimataifa kuonesha nia ya kweli, ujasiri wa kuchochea mara kwa mara kama maji yasiyotembea linapokuja suala la hali ya wanawake. Kardinali alisema uongozi wao katika nyanja za maisha ya kiraia unawezekana tu kutokana na elimu ya ubora na jumuishi. Hata hivyo UNESCO yenyewe ilichochea moja ya tafakari kuu ya mwakilishi wa Vatican. Katika Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, hasa inayohusiana na jinsia, Kardinali Parolin alisema ni wazi kwamba lazima kuwe na nia ya kuweka kwa nguvu msimamo unaofanana na usiobadilika, ambao hauvumilii dhana yoyote ya kianthropolojia, pamoja na ile iliyopendekezwa katika shule za Kikatoliki. Na kwa hivyo Vatican ina wasi wasi mkuvwa wa kupinga baaadhi ya mienendo fulani ya kiitikadi, kwa kisingizio cha kujibu matamanio fulani ambayo wakati mwingine yanaeleweka na huishia kudhalilisha uelewa wa wanawake na haki zao.
Mwakilishi wa Vatican ameomba kwa maana hiyo mataifa kuwa na ujasiri wa kuwekeza, na hivyo kurudisha nyuma ule uhusiano wa aibu na usio na usawa kati ya matumizi ya umma katika elimu na fedha za silaha, na pia ujasiri wa kuzingatia kikamilifu hali ngumu na chungu wanazoishi mamilioni ya wasichana na wanawake. Hii alisema ni kuzuia kufanya zoezi tupu katika hotuba wakati mtu hatafakari kikamilifu juu ya msingi bora wa elimu, unaoeleweka kama njia kuu ya kushughulikia kwa uangalifu ukosefu wa usawa wa kimuundo ambao unadhoofisha kuishi kwa raia, pia inaonekana katika jinsia, lile pengo ambalo bado linaendelea katika nchi nyingi.
Kwa mujibu wa Katibu wa Vatican, alibainisha kuwa kujumuisha ni lazima kuwa tayari kuunganisha vipengele vyote vya jamii ili kutoa njia za maendeleo za binadamu zenye ubunifu na zinazowajibika, zinazotosheleza hadhi ya wanawake. Wasichana ambao wanaweza kusoma bila vikwazo, badala ya kulazimishwa kama inavyotokea katika sehemu mbali mbali nyingi kwa kuacha shule, itakuwa vigumu kwao kuwa wanawake na mama katika umri ambao hawako tayari kimwili na kihisia kufanya hivyo, pamoja na yote ya kulazimishwa ndoa za utotoni. Hiki ni kipengele cha kwanza cha elimu jumuishi, ambayo Kadinali Parolin alichanganua na elimu bora yaani, ile isiyohusisha kiwango bora cha elimu na hadhi ya kijamii, lakini ambayo inaweza kutoa mawazo muhimu yenye uwezo wa kutathmini miundo ya maendeleo, uzalishaji na matumizi, kupendekeza vigezo vya haki ya kijamii vinavyolenga kuwasaidia walio dhaifu na wasio na ulinzi zaidi kutokana na uovu na upotevu ”.
Hitimisho la hotuba hiyo lilimulika maadili ya mwanamke kama zawadi kwa ubinadamu, yale ambayo yanaonesha licha ya mazungumzo fulani ya wanawake kudai mahitaji yenyewe uvumbuzi wa wanawake ambapo ubora zaidi wa maisha yana shughuli zinazolenga kuamsha wengine, katika ukuaji wao, na ulinzi wao. Wanawake wana uwezo wa kuelewa ukweli kwa namna ya pekee: kujua jinsi ya kupinga shida, kufanya maisha bado yawezekane hata katika hali mbaya sana na kung'ang'ania kwa ujasiri kwa ajili ya siku zijazo. Mchango unaoboresha uhusiano wa kibinadamu na maadili ya roho, kuanzia mahusiano ya kila siku kati ya watu, ambayo kwa upande wa Kardinali Parolin hufanya jamii iwe na deni kwa wanawake na kazi zao, hasa katika nyanja ya elimu.
Bila kusahau Kanisa ambalo, kwa kutambua ucheleweshaji na mapungufu ambayo yamechochea aina za ubaguzi wa wanawake pia ndani kwa sababu ya mawazo ya kiume, leo hii inawaona wanawake wakishiriki hatua kwa hatua katika vyombo vya ushirika na vya kufanya maamuzi vya ya Sekretarieti Vatican na Kanisa kwa wote, hadi kushikilia nyadhifa za uwajibikaji ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwa makasisi tu”. Kwa hakika haiwezi kuwa suala la kupandishwa cheo kwa kupunguzwa katika ugawaji upya wa majukumu badala yake ni uelewa wa lazima wa jinsi ya kutoa nafasi kwa uhalisi wa kike ili kuimarisha Kanisa kwa njia ya maana zaidi na ya uamuzi, Kardinali Parolin alibainisha.