Askofu Mkuu Gallagher yuko nchini Algeria katika afla ya miaka 50 ya uhusiano na Vatican!
Na Angella Rwezaula; – Vatican
Kuanzia Jumananne tarehe 25 hadi 26 Oktoba Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, yuko kwenye ziara nchini Algeria katika fursa ya tukio la kumbukumbu ya miaka 50 tangu kuanza kwa uhusiano wa kidiplomasia wa Vatican na nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.
Kwa mujibu wa ratiba yake iliyotplewa rasmi na mtandao wa Sekretarieti ya Vatican @TerzaLoggia, ziara hiyo kwa kufika ni kutembelea Makumbusho ya mashahidi huko Algiers, au kumbukumbu ya waathirika wakati wa vita vya ukombozi. Hii itafuatiwa na mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani, Bwana Brahim Merad, na Waziri wa Masuala ya Kidini, Bbwana Youcef Belmehdi. Askofu mkuu pia atakutana na mkuu wa Msikiti Mkuu wa Algeri, Mohamed Mamoune El Kacimi El Hassini, na atafunga siku ya kwanza ya ziara hiyo kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Algeria, Bwana Abdelmajid Tebboune.
Jumatano tarehe 26 Oktoba 2022 ni siku itakayofunguliwa kwa kutembelea Monasteri ya Tibhirine, mahali ambapo waliuawa watawa wa Kitrapist kati ya 1994 na 1996, waliotangazwa kuwa wenyeheri mnamo mwaka wa 2018 huko Oran. Mara baada ya hapo, Askofu Mkuu Gallagher atakutana na wanadiplomasia na mamlaka za kiraia na, baadaye, Kanisa mahalia na hatimaye kurudi jijini Roma.