Tafuta

Hotuba ya Kardinali Parolin katika Umoja wa Mataifa. Hotuba ya Kardinali Parolin katika Umoja wa Mataifa. 

UN:Mkutano kati ya Kard Parolin na Lavrov huko New York

Katibu wa Vatican na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Urussi wamezungumza nje ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko jijini New York,Marekani.

Na Angella.Rwezaula – Vatican.

Ni mazungumzo daima kwa sasabu kuna uwezekano unaowezesha kuleta mamadiliko ya mambo. Alikuwa amethibitisha katika Ndege ya kurudi kutoka Kazakhstan Baba Mtakatifu kwa  mara nyingine kwa waandishi wa habari ambao akizungumza nao  kuhusu ni dira ipi ya kidiplomasia ambayo inaongoza kwa kawaidia Vatican kwa namna ya pekee katika miezi hii kwenye muktadha wa vita kati ya Urussi na Ukraine. Mwelekeo wa kufuata kwa wote ambao ni wahudumu wa Papa Francisko kuanzia na Katibu wa Vatican ambaye kwa hakika  Alhamisi 22 Septemba 2022 akiwa nje ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York Marekani, aliweza kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urussi Serghei Lavrov.

Na Septemba 22 hiyo  akizungumza katika Mkutano wa X na Marafiki wa Ctbt ambacho ni kikundi kilichoundwa mnamo 2002 wa Australia, Canada, Finland, Ujermani, Japan na Nchi za Ulaya Mashariki, Kardinali mwenyewe alikuwa amebainisha kuwa kuongezeka kwa mivutano ulimwenguni na marudio ya hatari za matumizi ya silaha za nyuklia ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kupatikana kwa  Mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya nyuklia na  kuanza kutumika. Uthibitisho wa Kardinali Parolin unaunga mkono miito mingi ya Papa Francisko ya kuondoa kila aina ya viwanda vya utengenezaji wa silaha na kusitisha biashara ya silaha. Hata hivyo Jumatano, wakati wa Katekesi ya Papa Francisko mara baada ya tafakari yake alionesha ukaribu na msaada wa kwa watu wa Ukraine aliowaita ni ‘watukufu na mashahidi’.

Papa Francisko kwa maana hiyo  alisisitiaa jinsi ambavyo vita hivyo vibaya, kwa baadhi wanafikiria silahana za nyuklia, wenda wazimu na pia kuwashirikisha kile ambacho alisimuliwa na Kardinali Krajewski, ambaye kwa sasa yuko njiani kurudi Roma kutoka katika utume kwenye tamasha la vita nchini Ukraine. Papa alisema: “Alinisimulia uchungu wa watu na matendo maovu ya kutisha, maiti zilizopigwa ambazo wanazipata”. Kwa kusisitiza zaidi mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika 18 Septemba, pia alisema njia mojawapo tya kuondokana na mzmzo ni mazungumzo tu. “tusisahau kuwa amani inawezakana ikiwa silaha zinazima na kuanza mazungumzo!

23 September 2022, 15:43