Tafuta

 Papa Luciani Papa Luciani  Tahariri

Mkristo aliyegeuka kuwa Papa anatualika juu ya umuhimu wa Injili

Kutangazwa kwa Yohane Paulo I ni mwaliko wa kugundua unyenyekevu ambao unaruhusu kutafsiri kwa dhati katika maisha ya fadhila za imani,matumaini na mapendo.

ANDREA TORNIELLI

Mnamo tarehe 8 Februari 1970 katika mahubiri yake ya kwanza kama Patriaki wa Venezia kwenye Basilika ya Mtakatifu Marko, Albino Luciani alirudia maneno ambayo  kwa miaka kumi na moja iliyokuwa imepita alikuwa amesema kwa waamini wa Vittorio Veneto, mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Askofu. Maneno hayo yalikuwa ni kwamba “Katika mambo makubwa, Mungu wakati mwingine anapenda kuyaandika si juu ya shaba au marumaru, bali hata juu ya mavumbi; ili andiko likikaa, lisivurugike wala kutawanywa na upepo, kwa maana hiyo ni wazi kwamba sifa hiyo ni ya Mungu kabisa. Mimi ndiye vumbi. Shughuli ya  Patriaki na Jimbo la Venezia ni mambo makubwa yaliyounganishwa na vumbi; Ikiwa wema kidogo utatoke  nje kutokana na  muungano huo, ni wazi kwamba sifa hiyo ni huruma ya Bwana”.

Katika maneno hayo   ya “Mimi ni vumba” ni siri kubwa ya maisha ya mkisto ambayo Albino Luciani alishuhudia kwa muda wake mrefu wa maisha. Utakatifu wa Yohane Paulo I, mkristo aliyegeuka Papa mnamo tarehe 26 Agosti 1978 na ambaye leo hii baada ya miaka 44 amekuwa Mwenyeheri, ni historia rahisi ya mtu ambaye kila hatua ya maisha yake alimkabidhi Mungu na kujiweka kwake. Kwa kujikabidhi kwake huko kulitokana na dhamiri yake ya kuwa mdogo. “Bila mimi hamwezi kufanya chochote”, aliwaambia Yesu marafiki zake. “Rudi nyuma yangu, Shetani! Mnazareno alimwambia Petro, mara baada ya kumkaripia kwamba hasingweza kupata mateso na kifo.  Ni maelekezo mawili msingi ambayo Albino alifuata kwa kipindi kirefu cha maisha yake. Neema ya kujijua mdhambi, mwihitaji wa kila kitu; neema ya kutokuhesabu nguvu binafsi, akili binafsi, mikakati binafsi, lakini kwa  kuhitaji msaada na uwepo wa aliye juu vilimwezesha kuwa kuhani, Askofu na Papa kushuhudia uso wa Kanisa tulivu na aminifu.

Kanisa linaloishi Injili kila siku na halina haja ya kufyatua matifaki ili kufanya waone uwepo wake. Kanisa lenye uwepo wa kukaribisha, kufariji na matumaini ya wote, kuanzia na aliye mdogo zaidi, walio maskini zaidi, waliobaguliwa na wasio wakilishwa.  “Kutokana na kipimo cha unyenyekevu, ndiyo inafanya kujua maendeleo yetu ya kiroho”, kama alivyo kuwa anasema Mtakatifu Francis wa Sales, Mtakatifu ambaye alipendwa na Luciani. Kwake Yeye, aliyekuwa mtu mkubwam msomi na aliye jiandaa na uwezo wa kuzungumza kwa namna rahisi, alijua kuzungumza na kufanya aeleweke  kwa wote, ndivyo  alikuwa namna hiyo.  

Utambuzi kutoka kwa wengine, mtoto huyo wa Kanisa la Veneto, unafundisha kila aina ya mgeni kuondokana na kimbele mbele cha yoyote, ambacho hakuwahi kutamani vyeo maarufu na ambaye kabla ya kuchaguliwa karibu kwa kauli moja katika mkutano huo alikuwa akifikiria kuondoka kwenda kuwa kama mmisionari barani Afrika mara tu angefikia umri wa kisheria wa kung’atuka katika mamlaka ya Kanisa la Venezia, ni ishara ya matumaini kwa wote. Kwa sababu kama alivyosema msimamizi wa mchakato, Stefania Falasca, kwamba ili kuwa mwenyeheri, sio kwa sababu ni  Papa na wala upapa wake, lakini  awali ya yote ni mkristo ambaye alijikita yeye mwenyewe kwa Yote katika Injili,  kwa kujitambua kuwa “mavumbi”. Mkristo ambaye alisali kila siku akisema kwamba: “Bwana nichukue mimi jinsi nilivyo na nifanye niwe jinsi wewe utakavyo”, aligeuka kuwa chombo ambacho Mungu wa Huruma aliandika kurasa nzuri sana na  ambazo leo hii ni muhimu kuliko hapo awali kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili ya ulimwengu.

TAHARIRI YA DK TORNIELLI MKISTO ALIYEGEUKA KUWA PAPA

 

03 September 2022, 17:27