Maaskofu wapya 80 wanafanya kozi mjini Roma Septemba 5-17
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuna Maaskofu 80 walioteuliwa hivi karibuni katika ngazi ya kikanisa ambapo sehemu ya kwanza ya Baraza la Kipapa la Kimissionari barani Afrika, Asia, Amerika na Australia ambao wanashiriki katika Semina ya Masomo iliyohamasishwa kwa ajili yao na Baraza hilo la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Semina imefunguliwa Jumatatu tarehe 5 Septemba 2022 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Paulo Mtume, kwa Maadhimisho ya Ekaristi Takatifu ambayo imeongozwa na Kardinali Luis Antonio G. Tagle wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu ambapo semina hiyo itamalizika Jumamosi mnamo tarehe 17 Septemba, kwa Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na kutokuwapo mkutano wa pamoja na Baba Mtakatifu Francisko. Desturi ya Seminari za Masomo, iliyoanza tangu mwaka 1994, inalenga kuwapa Maaskofu wote walioteuliwa hivi karibuni kuongoza mipasho ya kikanisa ya maeneo ya umisionari, kipindi cha muda, mwanzoni mwa utume wao, kutafakari na kuimarisha maisha yao. Huduma ya Maaskofu, mazungumzo na kusalia. Kwa sababu hiiyo watoa mada ni watu wenye mamlaka katika ulimwengu wa kikanisa. Ratiba yao inajumuisha wato mada watatu kila siku, ikifuatiwa na mjadala, na kazi ya kikundi. Ufunguzi wa siku unaanza na maadhimishoa ya Ekaristi na masifu na hitimisho kwa sala ya masifu ya jioni.
Semina imegawanyika katika mada 8 msingi
Semina hiyo imegawanywa katika mada 8 msingi, ambazo kila moja inatafakariwa kwa kina na watoa mada tofuti . Mada ya kwanza inahusu “Uhusiano wa Askofu wa Jimbo na Baraza la Uinjilishaji”, na itashuhudia kufanyika kwa siku mbili za masomo zikifunguliwa hotuba ya Askofu Mkuu Protase Rugambwa (kuhusu “Huduma ya Baraza hilo kuelekea Makanisa Mapya mahalum ” na Giampietro Dal Toso ambaye atajikita na mada Matendo ya Papa ya Utume wa kimisionarri, Miundo, umahiri na shughuli zake”). Mada ya pili, inahusu Curia Romana ambayo itaoneshwa siku ya Jumatano tarehe 7 Septemba 2022 na Askofu Marco Mellino, ambaye atawasilisha mageuzi ya Curia Romana Kirumi, na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Kuhusu Vatican na uhusiano na Mataifa, na baadhi ya maelekezo juu ya mahusiano na serikali mahalia.
Mada ya unjilishaji, vyombo vya habari mazungumzo ya kiekumene na Liturujia
Siku mbili za masomo ya kina zitawekwa kwa ajili ya uinjilishaji, ambazo ni tarehe 8 na 9 Septemba, huku zikigusa juu ya tangazo la imani, matumizi ya vyombo vya habari, mazungumzo ya kiekumene na kidini, taasisi za elimu, huduma ya upendo na Barza la Maaskofu. Miongoni mwa wengine watakuwa Askofu Mkuu Rino Fisichella, Askiofu Mkuu Angelo Vincenzo Zani na Kardinali Luis Francisko Ladaria Ferrer. Mada ya Liturujia (“Il munus sanctificandi del Vescovo”) itazungumziwa kwa kina tarehe 10 Septemba na Kardinali Arthur Roche, wakati huo huo Dominika tarehe 11 Septemba Maaskofu watapata siku ya mapumziko ya kiroho huko Castel Gandolfo, kwa mita iyakayo hubiriwa kwa Kardinali Raniero Cantalamessa. Watoa mada mbalimbali watakikita na mada ya Wakleri, mnamo tarehe 12 na 13, na hotuba hizo kutoka kwa Katdinali Lazzaro You Heung-Sik, na Askofu Vincenzo Viva, na Askofu Charles Jude Scicluna, na Padre Armando Nugnes na Padre Hans Zollner. Askofu Giuseppe Sciacca na Askofu Juan Ignacio Arrieta watazungumza juu ya mada ya miundo ya majimbo mnamo tarehe 14 Septemba 2022. Mada mbili za mwisho zilizoguswa na Seminari, Maisha ya watawa na Walei, tarehe 15 na 16 Septemba, zitazungumzwa kwanza na Askofu Mkuu José Rodriguez Carballo na Sista Genowefa Kudlik, na ya pili, Kadinali Kevin Joseph Farrell, na Dk. Linda Gisoni, Dk Gabriella Gambino. Mada ya mwisho ya Semina, itatazama Makatekista katika maeneo ya utume ambayo itawasilishwa kwa Kardinali Richard Kuuia Baawobr, Askofu wa Wa.