Kardinali José Tolentino Calaça de Mendonça Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, 2022. Kardinali José Tolentino Calaça de Mendonça Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, 2022. 

Kardinali José Tolentino Calaça de Mendonça: Baraza Kipapa la Utamaduni na Elimu

Papa amemteuwa Kardinali José Tolentino Calaça de Mendonça kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Mkutubi mkuu wa Maktaba ya Kitume Vatican na Mhifadhi mkuu wa Nyaraka za Faragha za Vatican. Kardinali José Tolentino Calaça de Mendonça alizaliwa huko Mchico, nchini Ureno tarehe 15 Desemba 1965.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 26 Septemba 2022 amemteuwa Kardinali José Tolentino Calaça de Mendonça kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Mkutubi mkuu wa Maktaba ya Kitume Vatican na Mhifadhi mkuu wa Nyaraka za Faragha za Vatican. Itakumbukwa kwamba, Kardinali José Tolentino Calaça de Mendonça alizaliwa huko Mchico, Jimbo Katoliki la Funchal, nchini Ureno tarehe 15 Desemba 1965. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 28 Julai 1990 akapewa Daraja takatifu ya Upadre.

Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.
Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.

Katika maisha na utume wake kama Padre, amewahi kuwa ni Mshairi maarufu na Mwanataalimungu mahiri nchini Ureno katika miaka ya hivi karibuni. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Juni 2018 akamteuwa kuwa Mkutubi mkuu wa Maktaba ya Kitume mjini Vatican na Mhifadhi Mkuu wa Nyaraka za Faragha mjini Vatican. Tarehe 28 Julai 2018 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu. Tarehe 5 Desemba 2019 akateuliwa kuwa ni Kardinali na kusimikwa rasmi tarehe 15 Desemba 2019. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Septemba 2022 akamteuwa kuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.

Utamaduni na Elimu
27 September 2022, 16:34