Tafuta

Mkutano wa Umoja wa mataifa unaendelea Mkutano wa Umoja wa mataifa unaendelea 

Kard.Parolin kwa UN:Elimu ni njia muafaka kujenga jumuiya na historia ya binadamu

Hakuna hofu ya kupyaisha michakato ya mafunzo ikiwa lengo ni kijiji cha elimu ambacho kinahamaisha maadili ya heshima, mazungumzo na mshikamano.Huu ndio ujumbe mkuu wa hotuba ya Katibu wa Vatican katika UN kuhusu:"Mkutano wa Kubadilisha Elimu.“Elimu ni njia mojawapo ya ufanisi zaidi ya kufanya ulimwengu wetu na historia yetu zaidi ya kibinadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Elimu itatusaidia kuondokana na migawanyiko mingi iliyopo katika jamii zetu, kujenga jumuiya imara na thabiti zaidi kulingana na maadili ya udugu wa binadamu na mshikamano wa pande zote.  Ndiyo mawazo yalitolewa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican katika hotuba yake tarehe 19 Septemba 2022  huko New York Marekani katika "Mkutano wa Kubadilisha Elimu", uliaondaliwa mwanzoni mwa Juma la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Kardinali Parolin katika hotuba yake alisisitiza kwamba, Papa Francisko alizungumza waziwazi umuhimu wa kuanza mchakato wa mabadiliko bila woga na wa kutazama siku zijazo kwa matumaini, akiwaalika kila mtu, kuanzia vijana, walimu, viongozi wa kisiasa na asasi za kiraia, kuwa wahusika wakuu wa muungano huu kwa kujitolea,  wao wenyewe kwa kiwango cha kibinafsi na kijamii ili kukuza pamoja ndoto ya utu katika mshikamano, kuitikia matarajio ya binadamu na mpango wa Mungu.

Kuna hata migogoro mingine ambayo inasahulika

Kardinali Parolin aidha alisema “Kuzuka kwa janga la Covid-19 na sasa vita nchini Ukraine na bila kusisahau migogoro mingine mingi inayotokea katika maeneo mbalimbali ya dunia hufanya hitaji la mkataba wa elimu wa kimataifa kuwa wa dharura zaidi, alisema.  Na alizungumzia  juu ya hitaji la kuunda kijiji cha kielimu ambamo watu wote, kulingana na majukumu yao, wanashiriki kazi ya kuunda mtandao wa uhusiano wazi na wa kibinadamu. Zaidi alikumbuka methali ya Kiafrika inayoonya kwamba “ inahitaji kijiji kizima kumsomesha mtoto. Na kwa maana hiyo alisisitiza kwamba lazima tuunde kijiji kama hicho kabla ya kuelimisha na kueleza kwamba kwanza, tunahitaji kuondoa msingi wa ubaguzi na kuruhusu udugu kustawi.

Imani katika elimu kupamania ulimwengu uwe bora

Mwakilishi wa Vatican akisukumwa na imani kubwa kwamba kupitia elimu tunaweza kupambania  ulimwengu bora, alikumbusha Kardinali Parolin kwamba  miezi michache baada ya kuzuka kwa janga la UVIKO-19, Papa Francisko  alizindua Mkataba wa Ulimwenguni wa Elimu", akisisitizia, katika ujumbe wake wa tarehe 15 Oktoba 2020 kwamba elimu ni mojawapo ya njia bora zaidi za kufanya ulimwengu wetu na historia yetu kuwa ya kibinadamu zaidi. Kwa hivyo wazo la kuhusisha watendaji na wadau wengi wa kimataifa, Katibu wa vatica alisisitiza jinsi mchakato wa utekelezaji wa Mkataba huo wa Kimataifa wa elimu umeibua mipango mingi mipya katika ngazi ya bara na mahalia.

Shukrani kwa Katibu Mkuu kuhitisha mkutano huo

Vatican kwa maneno ya Kardinali Parolin, alimshukuru Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kuitisha mkutano huo juu ya suala muhimu kama hilo. Na Kardinali pia akakazia juu ya umuhimu wa kujenga upya muungano dhaifu wa elimu kwa kutambulisha vizazi vipya maadili ya heshima, mazungumzo na mshikamano kupitia uwekezaji wa rasilimali bora zinazopatikana katika elimu bora. Akiwa na mawazo ya ujumbe uliotumwa na Papa wakati wa uzinduzi wa Mkataba wa Kimataifa wa Elimu 2022, tarehe 12 Septemba iliyopita, Kardinali Parolin aliwaalika wale wote wanaofanya kazi katika nyanja ya elimu kuongozwa na kile alichokifafanua kuwa nguzo nne:kwanza, kanuni msingi wa kujijua binafasi, ikifuatiwa kwa karibu na kumjua jirani yako, ambayo  inatuhimiza kukumbuka nyingine, hasa wale walio katika mazingira magumu. Kanuni ya tatu ni kujua uumbaji, ambao hututia moyo ili kutunza nyumba yetu ya pamoja. Mwisho lakini sio kidogo ni kanuni ya kujua yaliyopita, ambayo inathibitisha mwelekeo wa asili ya mwanadamu kuelekea usio na mwisho, ili kupanua upeo na uwezo wa kugundua siri kuu za maisha.  Kardinali alieleza kwamba ni mvutano huo kuelekea hatima na wito wa ubinadamu ambao unaipa elimu maana yake ya ndani zaidi na kuwashawishi vijana juu ya thamani yake.

Mtazamo wa Elimu unahitaji kujitoa

Ni mtazamo kamili wa elimu ambao unahitaji kujitoa maalum. Kwa maana hiyo Kardinali Parolin alikumbuka mwaliko wa Papa Francisko kwa mashirika ya elimu duniani kote kupitia mipango na mitaala yao, kwa kuwalekeza wajikite katika njia saba maalum. Awali ya yote, kumfanya mwanadamu katika thamani na heshima yake kuwa kitovu cha kila juhudi za elimu, rasmi na zisizo rasmi; kusikiliza sauti za watoto na vijana ambao tunawapitishia maadili na maarifa, ili kujenga pamoja mustakabali wa haki, amani na maisha yenye heshima kwa kila mtu; kuhimiza ushiriki kamili wa wasichana na wanawake vijana katika elimu; kuona familia kama mahali pa kwanza na muhimu pa malezi. Kuelimisha na kuelimishwa kwa hitaji la ukarimu na hasa kwa uwazi katika hali zilizo hatarini zaidi; kutafuta njia mpya za kuelewa uchumi, siasa, ukuaji na maendeleo ambazo ziko katika huduma ya mwanadamu na familia ya mwanadamu, katika muktadha wa ikolojia fungamani; kulinda na kukuza  nyumba yetu ya kawaida ya pamja, kuilinda kutokana na unyonyaji wa rasilimali zake, kwa mujibu wa kanuni za ugawaji sawa, mshikamano na uchumi wa mzunguko. Kusudi kuu ni  kuifanya elimu kuwa muhimu kabisa, kushinda tofauti kati ya nyanja zake za utambuzi, kihemko na kimaadili".

Kanisa katoliki katika nyanja ya elimu Ulimwenguni kote

Kardinali Parolin pia alikumbusha kwamba, Kanisa Katoliki, ambalo tangu asili yake limesindikizwa  na uinjilishaji na uenezaji wa maarifa, utamaduni na sayansi,  kwa njia za monasteri kama kitovu cha utamaduni, kupitia shule nyingi zinazohusiana na Makanisa mahalia pamoja na msingi wa vyuo vikuu vya kwanza vya nchi za Magharibi,  dunia inaendelea kujihusisha kuwa mstari wa mbele katika elimu na karibu shule 220,000 na vyuo vikuu 1,365 vilivyoenea katika mabara yote, ambapo zaidi ya wanafunzi milioni 70, wengi wao wasio wakatoliki na wasio Wakristo, wanapata elimu bora.

Hotuba ya Kardinali Parolin katika Umoja wa Mataifa
20 September 2022, 16:26