Kwa Mabalozi wa Kipapa,Kard Parolin:tumkabidhi Maria maombi ya amani kwa ajili ya ulimwengu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku ambayo Mama Kanisa alikuwa anaadhimisha Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bikira Maria, mama wa Yesu Mkombozi wa dunia, kila ifikapo tarehe 8 Septemba, yalifanyika masifu ya jioni katika Kikanisa cha Kipapa Sistina, na Mabalozi wawakilishi wa Kipapa duniani kote, iliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican. Katika viti vya mbele walionekana makardinali wenye kofia nyekundu wakati nyuma na pembeni, kofia za zambalau za maaskofu wakuu wanaowakilisha Papa katika mataifa mbali mbali duniani na wakuu wa Curia Romana, pamoja na wakuu wa Sekretarieti ya Vatican na wawakilishi wa kudumu wa Vatican wasio maaskofu katika Mashirika ya kimataifa. Kwa maana hiyo moyo wa masifu ulikuwa ni siku kuu ya kuzaliwa kwa Mama wa Mkombozi Maria.
Maria hatapendwa vya kutosha
Kardinali Pietro Parolin akianza mahubiri yake alieleza jinsi ambavyo alikuwa na furaha ya kuwa katikati ya sala ya usiku ikiwa ni siku ya pili ya mkutano wa Wawakilishi wa Papa mjini Vatican, kwa uwepo wa Mama wa Yesu kwa jinsi ya mwili na Mama yao wa kiroho. Kardinali aliongeza: “Hatupaswi kuogopa kumwilishwa ujitoaji mpole wa kimwana kwake yeye, hatutasema vya kutosha juu ya Maria, na hatutampenda vya kutosha". Kardinali akinukuu maneno yaliyosemwa na Kadinali Ratzinger (yaani Papa Mstaafu Benedikto XVI )ambaye alikumbuka alipokuwa kijana alikuwa na mashaka kuhusu kanuni fulani za kale kuhusu Maria, zilionekana kutiliwa chumvi kwamba kwangu, sasa ninaelewa kuwa leo hii ni kweli, na ni halali zaidi kuliko hapo awali”, alisema Kardinali Parolin.
Dhamana maalum ile kati ya balozi na Bikira
Kardinali Parolin akiendelea alisema:“ Ikiwa tunataka kuwa Wakristo ni lazima tuwe wa Maria, ni lazima tutambue uhusiano unaomuunganisha Maria na Yesu. Maria ni jamaa kabisa wa Yesu. Iwapo ujitoaji kwa Maria unaomuacha Yesu, ungepaswa kukataliwa, lakini kinyume chake ni ukweli. Ni muhimu kumpenda Mungu. Mtakatifu Louis de Montfort, mpendwa sana na Papa Yohane Paulo II, alisadikishwa na hilo. Umoja huu wa Maria na Yesu ni muhimu sana leo hii, kwa sababu adhimisho la leo ni kwa heshima ya Kuzaliwa kwa Maria, lakini maana yake halisi ni Umwilisho wa Neno. Kwa hilo, kiukweli, Maria alizaliwa. Na tabia hii ya sikukuu hii ni ya maana sana kwetu, kwa sababu sisi sote pia katika utume wetu tunahusiana na mwingine”, alisisitiza Katibu wa Vatican.
Tumkabidhi maombi yetu ya amani kwa Maria
Kardinali Parolin amekumbusha kwamba mnamo mwaka wa 2019, Papa Francisko alikuwa amesema, kwamba balozi hajiwakilishi yeye mwenyewe, bali Kanisa na hasa Mrithi wa Petro katika eneo maalum. Kwa maana hiyo “katika kufanana na Maria, tumeitwa kumpenda na kumwiga na kuiga wema wake, ambaye ni kielelezo katika imani na mapendo. Anatufundisha kuwa na nguvu na huruma”. Hivyo basi, Kardinali aliwaalika wote waliohudhuria kukabidhi sala ya amani kwa maombezi ya Bikira Maria katika ulimwengu huu wa machafuko, ili atupatie siku za amani. Na pia katika wasiwasi huo kwa ajili ya ulimwengu mzima, Kardinali Parolin aliona uhusiano wa kipekee kati ya wawakilishi wa Papa na Maria kwa sababu, alisema, "Balozi ana wema kwa watu wote moyoni. Tukikumbuka hali zote za migogoro, ugumu na mateso tunayojua sasa hivi tumrudie Maria kwa kusema: “Utupe siku za amani”, Kardinali anahitimisha.