Kard.Krajewski amesali mbele ya kaburi la halaiki
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Huduma ya Kipapa katika safari yake ya Nne nchini Ukraine ameielezea kuwa hakuna maneno ya kusema na kueleza vya kutosha kwa kile alicho kiona kwa maana ya siku ambayo ilikuwa ngumu sana ana ambayo ilimwacha moyo wake kuwa mzito na kwamba ni sala tu ambaye inaweza kulainisha moyo huo. Akiwa Karkhiv, mahali alipofika usiku, asubuhi yake aliweza kuwa na Askofu Pavlo Honcharuk, wa jimbo la Kharkiv-Zaporizhia, huko Izyum, eneo ambalo limeachwa hivi karibuni na Warussi na mahali ambapo wamekuta miili ya watu karibia 500 imefukwa kwenye kaburi la halaiki. Kardinali amesimulia kwamba waliweza kuadhimisha na kuona wanaume vijana na hasa polisi na kundi la Wazima Moto, wanajeshi wakiwa na mavazi meupe wanachimba na kutoa ndani ya kaburi la halaiki miili ya maskini waukraine waliouawa bila huruma, wengine labda miezi 3 -4 iliyopita na wengine hivi karibuni hapo. “Hapa ni kubaki na mshangao tu wa kuogopya. Ninajua kuna vita na vita havina huruma, kuna hata vifo. Kwa hakika kuna wingi namna hii katika eneo ni jambo gumu la kusimilia na kulielezea” alisema Kardinali Krajewski.
Kuondoa miili kwa ukimya, kwa ushiriki wa hisia kali na kugusa. Kardinali Krajewski alingalia na kuona kwa wale walioitwa kwa kazi chungu ya huruma ya kila mtu. Na kusema kwamba: “Kuna jambo moja ambalo lilinigusa sana: Vijana hawa wa Ukraine walikuwa wakitoa miili hiyo kwa namna nadhifu, ya kimya, kimya kabisa. Ilionekana kama maadhimisho, hakuna aliyezungumza lakini kulikuwa na polisi wengi, na askari karibu watu wasiopungua 200. Wote kwa ukimya, kwa heshima ya ajabu kwa fumbo la kifo. Kulikuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwa vijana hawa”. Ilikuwa wakati wa kugusa moyo sana kuona jinsi miili hiyo ilivyobebwa. Ilionekana kuwa walikuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya familia zao, kwa ajili ya wazazi wao, watoto wao, ndugu zao. Askofu na mimi tulitembea kati yao, niliongoza roari ya huruma bila kusiki na tulibaki hapo kwa masaa matatu hivi..Sikuweza kufanya kitu kingine chochote zaidi ya kusali. Ilikuwa kama maadhimisho ya huruma, ishara ya bure kabisa. Hii ndiyo imabaki kwangu na sasa nimerudi Karkhiv, niko kwenye Kanisa na ninafikiria juu ya vijana hao. Ilikuwa siku ngumu, ambayo pia ilikuwa na ziara ya kituo cha polisi, iliyogeuzwa kuwa chumba cha mateso”.
Akiendelea alisema “Nilijua nitawakuta wengi wamekufa lakini nimekutana na wanaume ambao wameonesha uzuri ambao wakati mwingine umejificha mioyoni mwetu. Walionesha uzuri wa kibinadamu mahali ambapo kunaweza kuwa na kisasi tu. Lakini hapana. Maneno ya Maandiko Matakatifu yalikuja akilini kwamba uovu lazima ushindwe na wema kila wakati. Uhakika ambao kweli upo kwenye majeraha ya vita hivi”. Ikumbukweli Siku tatu zilizopita Kadinali huyo wa Poland walilengwa risasi lakini hawakudhurika wakati akipeleka msaada Zaporizhia pamoja na maaskofu wengine wawili, mmoja mkatoliki na mmoja wa kiprotestanti, na akifuatana na mwanajeshi wa Ukraine.
"Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu – aalisema kwa Vatican News - sikujua wapi pa kukimbilia ... kwa sababu kukimbia hakutoshi, unahitaji kujua wapi". Mwishowe, kila kitu kilikwenda sawa, hakuna mtu aliyejeruhiwa na misaada ilitolewa hadi mwisho, hata rozari zilizobarikiwa na Papa na aliyezipokea mara moja akaziweka shingoni.