Tafuta

2022.09.17 Utuke wa Kardinali Krajewski nchini Ukraine 2022.09.17 Utuke wa Kardinali Krajewski nchini Ukraine 

Kard.Krajewski akiwa Ukrane:Kwa mara ya kwanza sikujua nikimbilie wapi

Jumamosi 17 Septemba 2022 ilikuwa siku ngumu katika utume mpya kwa msimamizi wa Sadaka ya Kitume aliyetumwa na Baba Mtakatifu kwa mara ya nne nchini Ukraine. Licha ya kukabiliwa na risasi,waliendelea kupeleka misaada,chakula,rozari na baraka kutoka kwa Papa Francisko ili watu wasijisikie peke yao katika vita inayoendelea.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwenda Ukraine katika maeneo ya vita ili kupeleka misaada kwa watu na kumfanya Papa na Kanisa zima kuwa karibu na watu wanaoteseka ndiyo utume unaotekelezwa na Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, aambaye ni mjumbe wa Papa kwa mara ya nne nchini Ukraine kwa kufuatilia hatua hadi kiini cha mzozo huo. Mwanzo alikwenda Odessa baadaye  Zaporizhia, kwa nia ya kutaka kufika Kharkiv.

Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo
Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo

Jumamosi tarehe 17 Septemba 2022, akizungumza na Vatican News, Kardinali Krajewski ameeleza jinsi ambavyo huko Zaporizhia, siku haikuwa kama nyingine: "Leo ni siku maalum kwa sababu ni miaka tisa tangu Baba Mtakatifu aliponichagua kuwa Msimamizi wa sadaka ya kitume na tangu nilipowekwa wakfu wa  kiaskofu”, alisema.

Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo
Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo

Ni kweli kwani iIlikuwa ni tarehe 17 Septemba 2013 alipowekwa wakfu wa kiaskofu katika Ibada ya Misa  takatifu kwa uwepo wa Baba Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  Vatican. Na ndiyo siku hiyo kiukweli tarehe 17 Septemba kwa shauku ya Papa aliye mtuma ili aweze kuwa karibu kwa msaada wa dhati kwa watu wenye shida ambao wako wanaishi janga la vita vya kipuuzi, pamoja na maaskofu wawili, mmoja mkatoliki na mmoja mprotestanti ambao walisindikizwa na Mwanajeshi. Gari lao lilijaa vitu vya kutoa msaada. Mwishoni, kila kitu kilikwenda vizuri na misaada ilitolewa hata rozari zilizobarikiwa na Papa na wale waliopokea mara moja walivaa shingoni mwao.

Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo
Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo

Ni sIku maalum katika ukumbusho huo wa kuwekwa wakfu kwake wa kiaskofu na siku ya vita ambayo Kardinali alifafanua kuwa: "bila huruma", ambayo, kama tayari katika utume wake wa mwisho wakati wa ziara yake ya tatu ya kipindi cha Pasaka, alipokuwa amesema hakuna machozi na hakuna maneno. Lakini kwa siku ya Jumamosi 17 Septemba, Kardinali Krajewski alisisitiza tena kwamba “mtu anaweza kusali na kurudia tu: "Yesu, ninakutumainia”.

Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo
Kardinali Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo

Kwa hiyo katika siku hiyo walikutana na watu na kushusha chakula, lakini katika hatua ya pili  iliyopangwa ilitokea kwamba kikundi hicho kilifyatuliwa na risasi na Kardinali, pamoja na wengine, ilibidi wakimbie kujiokoa. Kwa mujibu wake alisema: "Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, sikujua pa kukimbilia... kwa sababu kukimbia hakutoshi, lazima ujue ni wapi”, alisema

18 September 2022, 11:53