Jumuiya ya vyombo vya habari Vatican imempongeza Padre Federico Lombardi
Na Angella.Rwezaula – Vatican.
Katika Kanisa la Bikira Maria, Trapontina jijini Roma, Jumanne tarehe 6 Septemba 2022 imefanyika misa kwa ajili ya kumbukizi ya zawadi ya maisha ya miaka 80 ya kuzaliwa kwa Padre Federico Lombardi, (SJ) na miaka 50 tangu alipowekwa wakfu kuwa Padre. Katika ibada hiyo iliyoongozwa naye akisaidiana na baadhi ya Mpadre, wanaofanya kazi katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano, na waamini wengi wake kwa waume wanaofanya kazi na wale ambao tayari wamestaafu. Wote wamefika kwa lengo la kumpongeza Padre Lombardi ambaye kwa muda mrefu alikuwa Mkurugenzi wa Matangazao na zaidi ya kuwa katika Kituo cha Televisheni Vatican na Ofisi ya Vyombo vya ahabri Vatican.
Padre Rombarid katika mahubiri yake kwanza amemshukuru Mungu kuadhimisha Ekaristi katika Kanisa hilo, ambalo limemkubusha miaka iliyopita wakisali pamoja katika miktadha mingi tofauti na nzuri lakini pia ya huzuni, kwa kuyaweka yote mbele ya Bwana kama jumuiya, walioalikwa kuhudumia Kanisa na ulimwengu wa Mwasiliano ya kijami. Lakini zaidi haya kuishi uhusiano mwingi wa urafiki, ushirikiano, wa kibinadamu na kiroho kati ya wote. Kwa maana hiyo sasa baada ya kupita kati kati ya maisha na zaidi ya nusu ya maisha ya kikuhani, ni vema kuwa na fursa ya kukutana ili kusali hata katika siku hizi za kumbukiza. Padre Lombardi ameshukuru urafiki wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambao wameandaa siku hiyo. Kiukweli amehisi kutostahili kwa sababu kwa wiki wandishi wa habari wamezungumza mengi kuhusu yeye, hata kama kwa hakika ndiyo kazi yao. Lakini walifanya mambo mengi kuhusu yeye. Kwa maana hiyo ameomba azungumze kidogo na zaidi azungumze kuhusu Yesu kwa sababu yeye ndiye aliyewaunganisha mahali pale.
Padre Lombardi akianza na somo lilosoma kutoka kwa Mtakatifu Paulo na ambalo analipenda kwa miaka mingi amesema wamini wa watu walikuwa wanapenda kufuata, na hata leo hii mara nyingi kufuata, kwa kutafakari kiibada, kuzungukia maisha ya Yesu ambayo hayakuwakilishwa katika makanisa yetu ya wakati wa karne za imani. Hata yeye alijifunza kushangaa kwenye kuta za makanisa ya kizamani au vikanisa vidogo vidogo vilivyoko kwenye milima mitakatifu. Kuna wakati unafikia amesema mahali pa mwisho na kubaki bila neno mbele ya kile kinachowakilishwa machoni. Labda sio hiyo tu katika mchakato wa hija, lakini hata katika safari yetu ya maisha. Padre Lombardi amekumbuka somo la Injili ambapo Yesu alikufa msalabani katikati ya majambazi wawili waliosulibiwa kwa moyo ulio wazi uliofunguliwa na mshale na ukatoka damu na maji. Padre amesema “Sijui ukurasa wa kuvutia zaidi kuliko Maandiko haya. Sijui picha iliyo kubwa zaidi. Kwa miaka mingi nimehisi kuvutiwa zaidi na zaidi, na kana kwamba nimetiishwa nayo”. Kwa maana hiyo Mbele yake hakuna maneno mengi ya kusema. Inahitaji kutafakari kwa macho na hasa kwa mtazamo wa roho. Kama anavyoandika Mtakatifu Yohane kuwa ni kuinua mtazamo juu yake.
Juu ya msalaba kulikuwa kumeandika neno katika kina cha sheria ya huruma ya Bwana, ukafunguliwa kwa sababu ulikuwa unatunza na amejionesha kwa muda mrefu katika safari ya kutafakari na kujitoa kabisa bila kujibakiza hadi tone la mwisho. Yesu mwenyewe katika wakati kipindi cha kina na cha kutufariji alikuwa amesema “ Jifunze kutoka kwangu mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo”, na sasa ni kuacha moyo ukatwe vipande kwa ajili yetu. Na utume umetimia hasa sisi tunaweza kujifunza hadi mwisho. Karne nyingi za kutafakari Yesu Msalabani na moyo wake uliofunguliwa unaangaza fumbo hili la maaana kubwa. Mtakatifu Pualo anazungumaza utajiri mkubwa mno. Ni zawadi ya Yesu ambaye anakufa ili kutupatia uzima, uzima wake unaotoka kwa Baba, tumaini la uzima wa milele. Kiukweli kama ilivyosikia Injili “ tuna hakika kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu na atatufufua sisi pia pamoja na Yesu na kutuweka karibu naye pamoja naye. Hizi ndizo sakramenti na kwa sababu hii zinatolewa katika nyakati mbalimbali na katika hali tofauti za safari yetu”.
Kubatiza, kusehehe, kutia moyo kwa mpako, kutoa mkate wa kila siku, kubariki kwa furaha, na katika uchungu, katika maisha na katika kifo, au hata kusindikiza kwa upendo, kwa neno la Mungu au kwa ukimya uliojaa upendo na mtazamo wa Yesu katika ulimwengu na katika maisha yetu. Hiyo inaeza na lazima kufanya kuhani na inaweza kufanywa kwa jina la Yesu kwa nguvu ya Yes una si kwa jina binafasi ambayo wala haistahili kitu. Padre Lombardi amesema alivyoruhusiwa kufanya uzoefu na jumuiya ya wana habari Vatican katika mchakato wa miaka na anawashuku kwa sababu anahifadhi kama vile tunu msingi katika safari yake.
Padre Lombardi ameshukuru kwa dhati na kwa furaha, ameshukuru kwa moyo uliofunguliwa wa Yesu na kwa sakramenti ya maisha ambapo amependa kuifikiria kama kisima cha maisha yaliyopyaishwa, ya maana ya maisha zaidi ya chuki na kifo. Hiyo ina maana ya maadhimisho yao. “Ni lazima pia tuseme kwamba tukitazama msalaba na moyo wa Yesu, hata kama tumeguswa kwa njia ya ndani sana na ya kibinafsi ndani ya kina, hatuko peke yetu hata kidogo. Aidha amependa kutazama pamoja kwamba awali ya yote kuna Maria Mama wa Yesu na mama yetu ambaye alikuwa chini ya msalaba, na mwanafunzi aliyependwa na Yesu ambaye anawakilisha sisi sote, wanawake wengine ambao walitembea njiani na Yesu ambao tunakutana nao katika njia za msalaba na watatusaidia kujua mwokozi, Wapo wanaobishana na kutoa maoni na wanaojiuliza; kuna yule askari aliyestaajabu na mkuki wake mkononi, kwanza kwa jeuri yake na kisha kuongoka... Kwa kifupi tupo wote na tunaomba siri hii kubwa ifunuliwe maishani mwetu, siku hadi siku.
Kabla ya kuhitimisha, Padre Lombardi amependa kufikiria mkutano wa sala uliozaliwa hasa kwa wale waliofanyaka kazi na kwa namna nyingine nyingi katika mawasiliano Vatican huku wakitafsiri kwa lugha mbali mbali wakati wa siku kuu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Na walikuwa wakitazama Altare ya Mtakatifu Petro penye masalia yake kwamba: “Sisi pia tunapaswa kuendelea kutazama kwa mshangao altare hiyo, si ile tu iliyo kwenye kaburi la Petro, bali katika kila altare. Sisi pia lazima tukimbilie kuonesha uso wa Yesu ulioandikwa kwa neema moyoni, kama ujumbe muhimu na mzuri zaidi. Kwa hivyo kazi yetu itaendelea kupata maana yake kutoka katika chanzo”. Ikumbukwe Padre Lombardi katika maisha yake, amebahatika kufanya kazi na Mtatifu Yohane Paulo II, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI na Baba Mtakatifu Francisko katika huduma kwa Kristo na kwa Kanisa lake takatifu
Dk.Ruffini:Padre Lombardi alitufundisha kuwa mtaro wa vita vyetu sio mahali pengine ni mahali tulipo sisi
“Ikiwa tuko hapa leo wengi na tunafurahi kuwa hapa ni kwa sababu sisi sote ni watoto wa Padre Federico Lombardi kwa njia tofauti, kitaaluma, watoto wa kiroho ambao walikua kwenye mabega yake kama Mjesuiti, mwandishi wa habari, Mkristo mwenye shauku ya Injili ambayo alijua jinsi ya kuwa na anaendelea kuwa mwalimu na shuhuda wa huduma isiyo na ubinafsi kwa Kanisa na kwa Vatican. Mwenyekiti wa Baraza la Mawasiliano, Dk Paolo Ruffini ndivyo alimwelezea kama ishara ya kumsalimia Padre Lombardi kwa niaba ya wote, akitoa kiini kwa hisia ya pamoja Kwa maana hiyo Dk. Ruffini katika afla ya kupongeza, kwenye makao makuu ya Mawasiliano aliorodhesha baadhi ya sifa zake ambazo zimemfanya kuwa zawadi kwa wengine, kama vile maneno yake, “kuwapo kwake kila wakati”, “uwezo wa kusikiliza, kujibu, kuelezea, umaridadi wake, na ucheshi wake”. Aidha uvumilivu wake na fadhila ya watu wa mlima”.
Dk. Ruffini ameendelea kusema kuwa “sote tumejifunza kutoka kwake kuhusu shauku ya mazungumzo, shauku kwa wale wanaofikiria tofauti, udadisi wa ulimwengu, nia ya kujaribu kubadilisha kile kinachowezekana na unyenyekevu wa kuelewa kuwa kila kitu kinawezekana, kwa sababu sio kila kitu kinategemea sisi”. Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa maana hiyo amesisitiza juu ya shauku ya Padre Lombardi, katika nyayo za Mtakatifu Ignatius wa Loyola, kwenda karibu bila kutambuliwa, ingawa yeye si mtu wa nusu nusu”. Padre Federico yuko hivyo na alitufundisha hivyo kwamba mtaro ambamo vita vyetu vinapiganwa sio mahali pengine. Ni pale tulipo sisi”, am amehitimisha Dk. Ruffini.