Tafuta

Katibu Msaizidi wa Vatican akitia saini kitu cha wageni wakati wa kitembembea Dili Mashariki wa Timor Katibu Msaizidi wa Vatican akitia saini kitu cha wageni wakati wa kitembembea Dili Mashariki wa Timor 

Ask.Mkuu Peña Parra:amefungua Ubalozi mpya wa Vatican nchini Timor Est

Katibu Msaidizi wa Vatican yuko Jijini Dili kwa ajili ya kuzindua Ubalozi mpya wa Vatican.Na ametoa hotuba katika Chuo Kikuu Katoliki kuhusu hati ya Abu Dhabi,ambapo amejikita kuzungumzia chumvi kama ishara ya udugu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Matumaini ni kwamba Ubalozi mpya wa kitume wa Vatican, unaweza kusaidia kama ishara ya dhati ya umakini na wasi wasi wa Baba Mtakatifu daima ambao amekuwa nao kwa ajili ya watu wa Timor Est  na kwa ajili ya waamini, ikiwa ni kuonesha upendo wa Baba Mtakatifu kwa Kanisa Katoliki mahalia ili waweze kutiwa moyo na kupyaishwa kwa waamini wote. Kardinali Edgar Peña Parra,  Katibu Msaidizi wa Vatican ametumia fursa tarehe 20 Septemba 2022 akiwa jijini Dili kwa waliokuwapo kuzindua makao mapya ya  utume mpya wa kidiplomasia. Miongoni mwake ni Rais  Ramos-Horta, mtunzwa Nobel ya Amani 1996. Ubalozi mpya kwa ujumla wa  jengo lote  ni rangi ya kijani, kwa makubaliano na mafundisho ya Papa katika Waraka wake wa Laudato sì inaonesha shauku ya maelewano ya kisanifu. Na hiyo ni ishara ya uhusiano mzuri kati ya Vatican na Jamhuri ya Demokrasia ya Timor Est.

Katibu Msaidizi wa Vatican akimsikiliza rais wa Timor Est
Katibu Msaidizi wa Vatican akimsikiliza rais wa Timor Est

Ufunguzi wa Ubalozi mpya umefika katika mwaka ambao wanaadhimisha miaka 20 ya uhuru wa Nchi na ukarabati wa vifungu vya mahusiano ya kidiplomasia , yanayoshuhudia hata maendeleo makubwa yaliyotendeka  hadi sasa  kati ya nchi mbli, shukrani kwa matendo ya makubaliano ya 2015, yanayotazama mantiki mbali mbali ya maisha na huduma ya Kanisa katoliki katika Nchi ambapo wakatoliki kwa zaidi ya miaka 50  inakuwa ni chanzo cha nguvu na kutiwa nguvu kwa watu , iwe wakati nyanja kama  ule wakati hasi, alisisitiza Askofu Mkuu  Pena Parra. Ni Ushuhuda wa kweli wa Papa Francisko kwa njia ya kumteua Kardinali wa kwanza katika historia ya Taifa hilo, Askofu Mkuu wa Dili, Virgilio do Carmo da Silva. Kwa maana hiyo Askofu Mkuu Parra alisisitiza  kufurahishwa pia  maamuzi ya Bunge katika kukubali Tamko la Udugu wa Kibinadamu, lililotiwa saini huko Abu Dhabi, mnamo 2019, na Papa Francisko na Imam Mkuu wa Al Azhar al-Tayyib, mahali ambapo yale yaliyomo, yameingia katika mtaala wa shule na yataongoza vijana katika shauku zao, kuwa wazalendo wema na si tu kwa nchi hiyo, lakini hata kwa ulimwengu. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Vatican alisema hii ni  kwa sababu “kwa vifungo vya hadhi za watu wote, tunaweza  kuingeza maridhiano ya kweli na amano kwa ajili ya amajeraha ya wakati uliopita na kuunda jamii ya haki na matarajio mema kwa kizazi kijacho”.

Katibu Msaidizi wa Vatican akiwa pamoja na Rais wa Timor Est
Katibu Msaidizi wa Vatican akiwa pamoja na Rais wa Timor Est

Katika umuhimu wa mafunzo kwa kizazi kijacho Askofu Mkuu Peña Parra alikuwa amefanya rejea ya tarehe 19 Septemba akizungumza katika Chuo Kikuu Katoliki cha Timor Est wakati wa mkutano wake uliokuwa inajikita juu ya Tamko la Abu Dhabi, ambapo katika hotuba yake,  Katibu Msaidizi wa Vatican alikuwa ametoa tafakari kuhusiana na umuhimu wa hatua hiyo katika muktadha wa mazungumzo ya kidini na katika maisha ya  Timor Est. Askofu Mkuu Peña Parra, katika kukumbuka maadhimisho ya misa Takatifu ya Mtakatifu Yohane Paulo Pili, mnamo 1989, katika uwanja mkubwa wa Tasi-Tolu, alikuwa amesisitiza umaarufu wa hotuba kuhusu: “chumvi ya dunia, akirudia kazi yake mara mbili. Kwanza ili “kutoa ladha” na ya pili “kuhifadhi”. Kutokana na hiyo  ndipo umuhimu wa chumvi ni kama ishara ya udugu , na kama ilivyo mfano ambao unatolewa na watu wa Timor Est ambao alisema, sio maridhiano tu ni kupatanisha. Ladha ya udugu ambayo ni hali ya lazima sana kwa ajili ya kufikia amani kama ilivyotajiwa katika Hati ya Abu Dhabi.

Katibu Msaidizi wa Vatican akiwa pamoja na Rais wa Timor Est
Katibu Msaidizi wa Vatican akiwa pamoja na Rais wa Timor Est

Chumvi kwa maana hoyo kama ladha ya udugu na kama ya kuhifadhi maisha, shukrani hata kwa Elimu na kuelimisha. Kwa njia hiyo maamuzi ya Bunge na Serikali ya Timor Est kuchukua  hatua ya Hati ya Abu Dhabu katika mitaala ya shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu, kwa mujibu wa Askofu Mkuu Peña Parra, inaleta maana kubwa kihistoria kwa sababu ni “kama ilivyo chumvi kuhifadhi chakula, iweze kuwa na uwezekano wa kuhifadhi kile ambacho wanajifunza, kwa namna ya kufunza dhamiri daima kuwa komavu”. Aidha alisisitiza kuwa “Mazungumzo ya kidini ni chamvi msingi ya kuleta ladha na kuhifadhi udugu ambapo kwa namna hiyo kama alivyoelekeza Papa Francisko kwamba sio tu fursa lakini ni huduma ya dharuru na ambayo haiwezi kubadilishwa kwa ubinadamu”.

UBALOZI MPYA WA VATICAN NCHINI TIMOR EST
21 September 2022, 17:16