Mbegu hizo za matumaini kati ya uharibifu na kifo
ANDREA TORNIELLI
“Wasio na hatia hulipa vita, wasio na hatia!” Maneno ya Papa Francisko yanaonekana kuwa sauti ya yule anayelia jangwani, miezi sita baada ya kuanza kwa uchokozi usio na maana na wa kutisha wa Ukraine: uharibifu, kifo na mzuka wa migogoro ya nyuklia. Mwishoni mwa Katekesi, Papa kwa kuwakumbusha majukumu ya kila mtu kwamba: “Nafikiri ukatili mwingi kwa watu wengi wasio na hatia ambao wanalipa wenda wazimu wa pande zote, kwa sababu vita ni wenda wazimu na hakuna mtu katika vita anayeweza kusema: hapana, mimi si mwenda wazimu”. Hatuwezi kuzoea kile kinachotokea, baada ya miezi kadhaa ya picha za kushtua, zinazothibitisha kifo na uharibifu unaosababishwa na silaha za kisasa na bei ya juu sana katika suala la maisha ya wanadamu wasio na hatia yaliyotolewa sadaka, familia kuharibiwa, nyumba na biashara kuharibiwa, mitaa kuharibiwa. Sauti ya Petro haijawahi kushindwa kuonesha mshikamano kwa walioshambuliwa na wale wote wanaokabiliwa na matokeo ya vita, lakini pia kuwasihi viongozi wa mataifa yanayohusika katika nyadhifa mbalimbali kutafuta suluhisho la mazungumzo.
Matokeo ya nusu mwaka huu wa vita kati ya mataifa mawili katikati mwa Ulaya ni ya kusikitisha. Makaburi ya watu wengi, watoto waliokufa na waliojeruhiwa, akina mama wa Ukraine na Urusi wakiomboleza watoto wao wachanga waliokufa mbele, mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao, hatari ya njaa na uharibifu wa mazingira unathibitisha kutokuwa na uwezo wa wakuu wa nchi na mashirika ya kimataifa na kutokuwa na uwezo wa kutekeleza sheria, kwa ujasiri na ubunifu wa kile ambacho Papa anakiita “mpango wa amani”. Wengi, wengi sana, kiukweli wanaendelea kufikiria kulingana na “mpango wa vita” na kuzingatia uimarishaji wa miungano ya zamani ya kijeshi na kukimbilia ukichaa wa kuchukua silaha kama jibu pekee linalofaa. Ulimwengu, ambao tayari umegubikwa na vita vingi sana vilivyo “megeka vipande vipande vya Vita hivyo vya Tatu vya Ulimwengu ambavyo Papa Francisko alizungumza mara kadhaa, vipo vinarudi nyuma katika Vita Baridi. Bila kutaja madhara makubwa, ugavi wa kiuchumi na nishati, unaotarajiwa katika muda mfupi na wa kati kwa nchi nyingi.
Je, inawezekana kuona dalili za matumaini katika mazingira haya ya uharibifu? Ndiyo, inawezekana. Mbegu ya matumaini ni ukarimu ambao watu wengi wamefungua milango yao kwa ajili ya wakimbizi wa Ukraine, wameleta misaada binafsi, wamehusika katika mipango ya kibinadamu bila kujiruhusu kushindwa na “utandawazi wa kutojali”. Mbegu nyingine ya matumaini inawakilishwa na mashirika, vyama na vikundi ambavyo vimeshiriki katika vitendo na mipango ya amani, mazungumzo, michakato, kujihatarisha kibinafsi katika kutembelea Ukraine iliyoko katika vita.
Mbegu ya matumaini ni ufahamu unaoongezeka, ulioenea kwa watu zaidi kuliko viongozi wao na viongozi wao wa kisiasa, juu ya hitaji la haraka la kukomesha mauaji hayo kwa njia ya mapatano na mazungumzo. Kwa sababu ikiwa kwa kuibuka kwa migogoro mipya kutaendelea kujibu misingi ya mifumo ya zamani badala ya kuthubutu katika jaribio la kujenga umoja mpya wa kimataifa, kwa bahati mbaya hatima ya ubinadamu ina hatari ya kufungwa. Hatimaye, kuna mbegu ya matumaini ambayo ni ya kwanza na muhimu zaidi kwa mwaamini. Wale wanaoamini wanajua kwamba vita vinaanzia katika moyo wa mwanadamu, na kwamba Mungu anaingilia kati katika historia na kwamba sala, hasa ya wanyenyekevu, rahisi, na wanaoteseka, inaweza kuleta mabadiliko ya hatima ya wanadamu.