Tafuta

2022.08.09 Kardinali Czerny akiwa katika Jumba la Makumbusho huko Auschwitz Birkenau  katika maadhimisho ya miaka 80 ya kifo Mtakatifu Edith Stein( Benedetta wa Msalaba). 2022.08.09 Kardinali Czerny akiwa katika Jumba la Makumbusho huko Auschwitz Birkenau katika maadhimisho ya miaka 80 ya kifo Mtakatifu Edith Stein( Benedetta wa Msalaba). 

Kard.Czerny,aongoza misa huko Auschwitz kwa ajili ya miaka 80 ya kifo cha Edith Stein!

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu,aliadhimisha Misa 9 Agosti katika Mji wa mauaji ya kimbari kwa ajili ya kumbukumbu ya mfiadini na msimamizi mwenza wa Bara la Ulaya,akikimbuka kwa hisia kali za bibi yake ambaye aliishia hatima yake kwenye mauaji hayo ya kinazi.Kwa maombezi yao Kiongozi huyo ameombea amani kwa Ukraine na ulimwengu mzima.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Michael Czerny Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu aliongoza Misa Takatifu katika Siku Kuu ya Mtakatifu Teresa Benedetta wa Msalaba (Edith Stain) ambaye pia ni Msimamizi mwenza na wengine wa Bara la Ulaya, ambapo Mama Kanisa anakumbuka ufiadini wake kila ifikapo tarehe 9 Agosti ya kila mwaka. Misa hiyo takatifu iliongozwa katika Konventi ya Wamonaki wa Wakarmeli wa Oświęcim / Auschwitz nchini Poland. Kwa kawaida kila baada ya miaka 10 maadhimisho ya siku hiyo uadhimishwa kwa siku kuu kubwa mno, kwa mfano mnamo 2012 wakati wa miaka 70 tangu kifo cha mtakatifu huyo,  alishiriki kuadhimisha misa hiyo alikuwa ni  Kardinali Joachim Meisner, Askofu Mkuu wa Coloni nchini Ujerumani.

Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba)
Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba)

Kardinali Czerny katika mahubiri yake alisema ili kuchunguza yaliyopita, na kuelewa vyema ni vuzuri sasa na kujitolea kwa ajili ya  wakati ujao, ambapo “tunahitaji kuangazia kwa Neno la Mungu, taa ya hatua zetu na mwanga katika njia yetu” (Zab 118). Injili ya Mathayo iliyosikika, ilioonesha mojawapo ya mifano mitatu ambayo Yesu alitangaza mara tu alipotoka kwenye Hekalu, akiwa ameketi mbele ya Mlima wa Mizeituni (rej. Mt 24:3), kwa lengo la kuwafundisha wanafunzi wake juu ya umuhimu wa kuziangalia ishara zinazoambatana na kuja kwa Bwana. Kwa bahati alisema kwamba Yesu alikaa katika mwelekeo wa mlango uitwao ‘Porta Bella’ (Matendo 3, 1-10), ambao ulikuwa ni mlango wa kuingilia wale waliokuja kutoka Mlima wa Mizeituni kwa upande wa mashariki wa Hekalu. Kulingana na mapokeo ya Kiyahudi, yenye msingi wa maandiko ya kinabii (taz. Ez 10,18s; 11,22s), Hekalu lilipoharibiwa, Shekhinah (שכינה) yaani uwepo wa kimungu” waliondoka katika (Sancta Sanctorum).  Kwa njia hiyo walitegemea kuwa Siku moja, hekalu litakapojengwa upya, Shekhinah iweze kurudi kupitia Lango zuri, kwa sababu Masiha atakuja kutoka Mashariki kwa uvuka mlango huo huo (rej. Mk 11:1-11), Yesu mwenyewe angeingia Yerusalemu kwa ushindi, kinabii na kimasiya kupitia mlango huo.

Madhabahu ya Kwanza kwa ajili ya Kumbu kumbu ya Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba) Lubliniec,Poland
Madhabahu ya Kwanza kwa ajili ya Kumbu kumbu ya Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba) Lubliniec,Poland

Mifano yote mi tatu iliyosimuliwa katika tukio hilo Kardinali Czerny alisema imeunganishwa na himizo la lazima la Yesu: “Kesheni kwa sababu hamjui saa ambayo Bwana atarudi” . Hasa, mfano wa wanawali kumi ni mfano unaotufanya tusome maana ya kina ya historia yetu ya kila siku katika suala la wokovu au upotevu. Inatuongoza kujitambulisha na wanawali wapumbavu, kuanzisha mchakato wa uongofu unaotuwezesha kuwa kama mabikira wenye busara. Mfano huo haukusudii kuvuruga, au kusababisha hofu, lakini kusudi lake ni kufunua ukweli tu wa kimungu, na wakati ujao unaotungoja ni ule wa kukutana na Bwana-arusi! Mara nyingi alisema Kardinali kwamba tunapuuza siku na saa ya kuwasili kwa Bwana-arusi, lakini Yesu anatuhimiza kusherehekea uzuri wa kila siku kama hatua ya kuelekea kwake, kutoka kwa jinsi tulivyo kutoka kwa ubinafsi wa dhambi zetu pamoja na wema. Ili kukutana naye na kupokea vazi la arusi kutoka kwake, kwa kuvaa Bwana (Rum 13:14). Uwepo wetu ni matarajio tendaji, msafara unaoendelea kama Mtakatifu Gregory wa Nissa anavyouelezea kuwa “yeyote anayepanda haachi kamwe, huenda kutoka mwanzo hadi mwanzo kupitia mwanzo usio na mwisho”. Wakati mwingine, inahitaji juhudi kubwa, ujasiri wa kuondoka katika maeneo ya faraja, na kuruhusu Mungu atende tena ndani yetu” Alisisitiza Mkuu wa Bataza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu.

Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba) Lubliniec,Poland
Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba) Lubliniec,Poland

Kwa kubadilishana na uzoefu uzoefu wake binafsi kwamba katika miaka ya sitini, baada ya kupata shahada katika Chuo Kikuu cha Chicago, alibahatika kujua na kupongeza kazi na wazo la Edmund Husserl, kama yeye aliyezaliwa huko Mrqavia na asili inayofanana ya kiyahudi. Kwa njia ha Husser, alimtambua Edith Stain 1891-1942).  Hata familia ya mama yake, wazazi na ndugu wawili walikuwa wakatoliki lakini walikuwa wakishitrikishaba asili ya kiyahudi kwa kuchukuliwa na maadui. Bibi yake Anna na babu yake Hans na wajomba zake Georg na Carl Robert wote waliteswa Terezín, babu yake Hans akafa. Bibi yake na wajomba zake wakapelekwa kwenye kambi kuu ya Auschwitz. Na kutoka hapo wajomba zake walitumwa kwenye makambi ya kazi na mwishowe wakauawa huko. Kardinali Cerny ameeleza kwamba kutokana na kuwa na kumbu kumbu hiyo yote, kwake yeye imekuwa ni heshima kubwa na kuwa na hisia kali saa ya kuadhimisha miaka 80 tangu kuzaliwa mbinguni Mtakatifu Edith Stain, ambapo siku hiyo inaangukia mwaka huu kwa namna ya pekee na ambayo inawahimiza kufanya kumbukumbu ya wakati uliopita. Na zaidi akifikiria vita vya Ukraine na ukatili mwingi wa vita ambao umeendelea katika sehemu mbali mbali za dunia. Mateso ambayo yanawaweka watu wa Ukraine na Urusi, idadi kubwa ya wakimbizi inayozidi kuongezeka na waathirika, ambalo wanalazimisha kurudi kusumbua akilini hali ya mauaji ya kimbari. Tukio hilo linapaswa kumfanya kila mmoja ajiulize juu ya safari ambayo imetimizwa ya ubinadamu tangu kuisha kwa vita ya Pili ya dunia karibu miaka 80 iliyopita na leo hii.

Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba) Lubliniec,Poland
Mfiadini Sr Edith Staein( Benedetta wa Msalaba) Lubliniec,Poland

Katika historia halisi ya Edith Stein kuna  mfano wa jinsi maisha yaliyotumiwa katika upendo yanaweza kuwa njia ya uwazi, ya kugeuka sura polepole katika Mwana aliyefanywa mwanadamu. Kwa hija yake kama mwanamke, kama mwanafalsafa, mwalimu, mtafakuri na mtakatifu, tunaweza kutumia usemi mzuri wa hati nzuri ya kipapa ya Veritatis Splendor: “Fahari ya ukweli hung'aa katika vilindi vya roho ya mwanadamu” (VS 2). Hakika, utafutaji wa ukweli uliashiria uwepo mzima wa Edith na hata katika miaka ambayo alijitangaza kuwa “atheist” yaani asiyejali maswali ya imani, dhamiri yake dhaifu ya maadili na uaminifu wa kiakili ulimfanya kukataa viashiria visivyo na uhusiano mwema. Alasiri ya tarehe 2 Agosti, mawakala wawili wa Gestapo walibisha hodi kwenye mlango wa Komventi ya Wataw Wakarmeli ya Echt ili kumchukua Sr. Teresa Benedetta, pamoja na Sr Mwenzake Rosa. Walipelekwa kwenye kambi ya kupanga ya Westerbork kaskazini mwa Uholanzi, tarehe 7 Agosti walipelekwa pamoja na wengine wengi hadi kwenye kambi ya maangamizi ya Auschwitz-Birkenau. Tarehe 9 Agosti Sr. Teresa wa Msalaba alipitia mlango wa chumba cha gesi ambako alipata kifo. Baada ya kuvuka kizingiti, alikutana uso kwa uso na Bwana arusi, hivyo kutia muhuri mapatano ya ndoa na Kristo aliyesulubiwa, ambayo alijitayarisha kama bikira mwenye busara, akihifadhi mafuta ya upendo kwa Mungu.

Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu amekiri kwamba Bibi yake hadi sasa hajuhi alizikwa wapi na Auschwitz bado inaunganisha ushuhuda na masalio ya Mtakatifu Teresa Benedetta wa Msalaba na historia na roho ya bibi yake, popote mabaki yake yalipo. Kwa hivyo, aliongeza kusema “kwangu ni ya kusisimua sana kusherehekea kumbukumbu hiinya   Edith Stein na wakati huo huo na mahali pale pale, maadhimisho ya miaka 77 ya Anna Löw, kuomboleza na kumheshimu bibi yangu kwa kufikiria kuunganishwa tena na familia nzima na pia kwa Mtakatrifu Benedetta”. Hatimaye kwa maombezi yao amesema kuombea amani katika nchi ya Ukraine na katika dunia na ameomba wale ambao historia zao za kibinafsi na za familia ni za Kiyahudi na za Kikristo, wachangie katika mazungumzo ya lazima kati ya imani zote ili kuishi kama ndugu wote, katika nyumba yetu ya pamoja.

MAHUBIRI YA KARD. CZERNY KATIKA KUMBU KUMBU YA MT EDITH STEIN
10 August 2022, 14:51