Economy of Francesco:hata vijana wadogo wamejikita katika
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Sio vijana tu, bali pia vijana wadogo nao watakuwa miongoni mwa washiriki wa tukio lijalo la ana kwa ana la kimataifa la Uchumi wa Francesco (EoF), ambapo jumuiya hiyo mpya ya kimataifa itatia saini Mkataba na Baba Mtakatifu kwa ajili ya uchumi mpya ujao mwa tukio la siku tatu lililopangwa kuanzia tarehe 22 hadi 24 Septemba 2022, katika Jiji la Mtakatifu wa Assisi, Italia. Jumuiya hiyo, ambayo katika miaka hii mitatu haijaacha kukutana na kufanya kazi kwa nia ya mtandaoni, pia inaundwa na vijana wapatao ishirini kutoka nchi mbalimbali, akiwemo Ralyn Satidtanasarn anayejulikana kwa jina la utani la Lilly, mwanaharakati mdogo sana wa ikolojia kutoka nchini Thailand ambaye amekuwa akipambana dhidi ya matumizi ya plastiki kwa miaka hii.
Ingawa wengi wa vijana ni Waitaliano miongoni mwao ni kutoka ( katika Chuo cha Mtakatifu Karoli huko Milano, 'Taasisi ya Maria wa Msaada' huko Lecco na 'Ragazzi Mondo Unito' na 'Nomadelfia'), pia kuna vijana kutoka: Sria, Vietnam, Thailand, Slovakia na Brazili. Wote hawa ni kati ya miaka 13 na 17. Wavulana na wasichana wanaohusika katika mipango ya maendeleo endelevu kama vile #ZeroHunger na katika masuala ya ikolojia fungamani na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Kijana msichana mdogo wa Brazil pia atakuwepo, akihusika katika mpango wa Shule ya Pacar (Pacar School) aliyezaliwa ndani ya Mpango huo wa (EoF). Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kisayansi wa Uchumi wa Francesco Bwana Luigino Bruni ametoa maoni yake kwamba: “Wakati huu ni wakati wa uhusika mpya wa vijana na hasa vijana. Kamwe kama miaka ya hivi karibuni vijana wengi wamekuwa mstari wa mbele katika mahitaji ya mabadiliko makubwa katika uchumi na jamii, makubwa zaidi ambayo yamedaiwa katika miongo ya hivi karibuni. Greta Thunberg na Ijumaa kwa kizazi kijacho, kimewakilisha uvumbuzi muhimu zaidi wa karne ya 21 katika suala la utamaduni wa mazingira na mtindo mpya wa maendeleo. Leo vijana hawa wako kwenye mpaka wa mabadiliko duniani, wao ni walimu, wanatekeleza hukumu ya kweli kwa ajili yetu sote na tunafurahi hasa kwamba vijana, unabii wa Fransisko, wapo na wanafanya kazi katika uchumu wa Francisko (Eof) kwa njia muhimu”.
Katika mahojiano marefu maalum ambayo Ralyn alitoa kwa Marina Rosati ambaye ni Afisa wa Vyombo vya Habari kutoka Assisi kwa ajili ya The Economy of Francesco, mtoto huyo wa miaka 14 ametoa mwanha juu ya kujitolea kwa vijana kama yeye. “Hata vijana na watoto hawawezi tena kupuuza ulimwengu unaowazunguka, tumelazimika kutatua matatizo ya watu wazima kwa sababu ya hofu ya kutokuwa na maisha safi na endelevu. Watu wazima lazima waache ulimwengu bora kwa ajili ya watoto wao na vizazi vyao, na hatua madhubuti za kutatua matatizo ya leo, kama vile mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira na ukosefu wa usawa, na sio tu kuyazungumzia.”
Kujitolea kwa kijana huyo mdogo wa Thailand kulianzia kama mtoto, kama anavyosema: “Kama mtoto, siku zote nilikuwa najali na kujitolea kwa ajili ya mazingira: kama raia wa dunia, sote tuna wajibu wa kudumisha. Ingawa nilikuwa na umri wa miaka minane tu wakati huo,” amesema, “nilijaribu kufanya sawa, kupunguza plastiki na kuwaambia wanafunzi wenzangu na familia kufahamu athari zao kwa mazingira.” Kwa bahati mbaya, uanaharakati wa mtu binafsi unaweza kufanya mengi tu, kwa hiyo niliamua kushughulikia tatizo kwenye mizizi, katika ngazi ya ushirika na serikali. (....) Mapema 2020, mifuko ya plastiki ya matumizi moja ilipigwa marufuku nchini kote kwa zaidi ya wauzaji wakuu 70. Hili lilikuwa mojawapo ya mafanikio yangu. Nilijifunza kuwa masuala ya mazingira yanaathiri kila mtu, hivyo sote tuna wajibu wa kuchangia mabadiliko”."
Kwa upande wake Ralyn, Uchumi wa Francisko (Eof) ni njia nzuri ya kuanzisha mazungumzo kuhusu athari ambazo vijana wanaweza kuwa nazo kwa tabianchi na anapokuwa Assisi anaelewa wazi kile atachosema kwamba “Kwanza kabisa, ningependa kushukuru.Papa Francisko kwa mafundisho na wema alioshiriki katika miaka ya upapa wake. Pia napenda kumshukuru kwa kuwafahamisha kila mtu kuhusu matatizo ya sasa ya ulimwengu na kwa kuwaunga mkono kwa dhati vijana kama mimi ili kuinua hali zao, sauti na kusikika na watu wakuu, kama yeye, ambao wanaweza kutusaidia kuleta mabadiliko, amehitimisha kijana huyu mdogo wa miaka 14 tu.