Askofu Mkuu Peña Parra:Inawezekana kufanya kazi kwa umoja
VATICAN NEWS.
Nyuma ya kila tendo, kila hati, kila barua, kila uamuzi, kuna Kanisa. Hayo yalilisisitizwa na Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Vatican na mjumbe wa Papa Francisko katika Jamhuri ya Dominika kwa ajili ya kufunga Mwaka wa Jubilei ya Altagracian, katika mahojiano na Televida, chaneli ya televisheni ya katoliki ya Dominika hivi karibuni.
Mwakilishi wa Papa alikumbuka somo moja alilojifunza alipokuwa Padre kijana alipokuwa anakwenda kwenye balozi: “Ikiwa katika ubalozi inawezekana, kwa kazi ya kujitoa na makini, kwa mfano, kumteua askofu mpya katika jimbo, na askofu nzuri sana, mvuto wa hatua hiyo utakuwa mkubwa sana katika Kanisa na katika nchi anako jikita shughuli yake.
Askofu Mkuu Peña Parra alisisitiza jinsi uteuzi wa mtu sahihi kwa wakati unaofaa, mahali pazuri na kwa njia sahihi, unaweza kubadilisha historia ya jimbo, au ya kiumbe, chochote kile. Pia alieleza kwamba huu ndio umuhimu wa ukweli kwamba, kwa baadhi ya huduma za Kanisa, hata kama zikionekana kuwa za urasimu, Papa huwateua maaskofu ambao wamekuwa na uzoefu wa kidiplomasia, kulingana na ujuzi wao wa ulimwengu na hali halisi mahalia.
Alipoulizwa kuhusu uzoefu wake katika Jamhuri ya Dominika, Askofu Peña Parra alishirikisha hisia zake na kusisitiza ushuhuda wa imani ya Wadominika, hasa ibada kwa Bikira Maria wa Altagracia, Mama na Msimamizi wa taifa alisema kwamba anaondoka kwa furaha kwa sababu ameona kwamba inawezekana kufanya kazi pamoja, katika umoja.
Ikumbukwe kwamba kila tarehe 21 Januari inasherehekewa siku kuu ya Mama Yetu wa Altagracia anayechukuliwa kuwa mama msimamizi wa kiroho wa watu wa Dominika, na mlinzi wa yote ambayo ni ya Amerika ya Kusini. Alipewa jina la Altagracia kwa sababu hakuna mwingine zaidi yake ambaye ni Mama Mungu anayeweza kutupa watoto wake idadi kubwa ya neema.