Tafuta

2022.07.02  Ziara ya Kardinali Parolini jijini Kinshasa na  Sudan Kusini 2022.07.02 Ziara ya Kardinali Parolini jijini Kinshasa na Sudan Kusini 

Congo,Kard.Parolin akutana na Waziri Mkuu Sama&saini kati ya Kanisa na serikali!

Mikataba mitano inayofafanua hadhi ya kisheria ya Kanisa katika nyanja za afya, fedha,huduma ya kichungaji na kujitolea kwa jamii ilitiwa saini mjini Kinshasa na mawaziri na rais wa Baraza la Maaskofu Congo DRC.Kard Parolin alisema:“Jiwe Msingi la ushirikiano mpya,wenye amani na matunda zaidi wa Kanisa na mamlaka ya kiraia.Kardinali Ambongo:Ni hatua iliyosubiriwa kwa zaidi ya miaka sita.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa Kanisa Katoliki la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 2 Julai, 2022 itakumbukwa kama siku ya kihistoria. Kwani tarehe hiyo huko Kinshasa makubaliano mahususi yalitiwa saini kati ya (Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Cenco) na Serikali, ambayo inatambua  sasa hali halisi ya Kanisa, ambayo hadi sasa imesajiliwa na Serikali kama shirika lisilo la kiserikali. Hafla hiyo ilifanyika mbele ya Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, mara baada ya mkutano wa faragha wa zaidi ya nusu saa na Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde.

Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC
Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC

Zaidi, ya hayo kwa mikataba iliyotiwa saini tarehe 2 Julai 2022 na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Afya, Sheria, Fedha, Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu, Mambo ya Ndani na Rais wa Baraza la Maaskofu DRC Cenco, Askofu Mkuu   Marcel Utembi Tapa, Mkataba wa Mfumo uliosainiwa na Vatican  unatekelezwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu  tarehe 20 Mei 2016, kuhusu masuala yenye maslahi kwa pamoja. Mkataba huo ulitiwa saini mjini Vatican na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa, na Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo wa Congo, Bwana Raymond Tshibanda N’Tungamulongo. Kwa kuzingatia uhuru na uhuru husika kwa Kanisa na Serikali, ilianzishwa mfumo wa kisheria wa mahusiano ya pande zote mbili na hasa, iliidhinisha nafasi ya kisheria ya Kanisa Katoliki katika nyanja ya kiraia na uhuru wake katika shughuli za kiutume na katika udhibiti wa Kanisa masuala ya uwezo wake.

Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC
Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC

Kwa kuidhinishwa mnamo mwaka 2019, na kuanza kutumika mwaka wa 2020, Makubaliano ya Mfumo hayajawahi kutumika kikamilifu. Hati ya mwezi Juni 2020 ya Waziri Mkuu Sama Lukonde iliomba itekelezwe na hivyo kutambuliwa kwa Kanisa kama chombo cha kisheria. Baada ya miezi ya mazungumzo  na uhamasishaji mkubwa kutoka katika Kanisa la Congo ,  Ubalozi wa  Kitume na Wizara zinazohusika, Tume mchanganyiko baadaye  ikatayarisha mikataba mitano maalum inayosimamia maeneo ya kufundisha dini shuleni, taasisi za elimu za Kikatoliki, shughuli ya usaidizi ya ustawi wa jamii. Kanisa, huduma ya kichungaji katika taasisi za magereza na hospitali, sheria ya mali na kodi.

Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC
Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC

Katika hafla iliyohudhuriwa katika Chumba cha Mikutano cha waziri Mkuu walitia saini  na kubadilishana zawadi wakati huo makofi ya nguvu yakifuatia. Hatua hii ni dhihirisho la nia ya rais kuelezea heshima ya ziara ya Kardinali, alisema   waziri mkuu kwa  Kardinali Parolin. Kwa upande wake Katibu wa Vatican, alisisitiza kwamba Makubaliano yanajumuisha ushirikiano ambao umeunganisha Kanisa Katoliki na mamlaka ya kisiasa ya nchi hii kwa karne nyingi, kwa huduma ya watu wote. Maslahi ya Kanisa, katika mahusiano haya na mamlaka ya kiraia, kimsingi yanaelekezwa kwenye ushirikiano kwa ajili ya maendeleo shirikishi ya binadamu ya watu wote, bila ubaguzi wa kikabila au kidini, na hasa walio maskini zaidi na wenye uhitaji zaidi, alisema Kardinali. Na ni matumaini yake kuwa Mkataba wa Mfumo haungewakilisha tu mwisho wa mchakato mrefu, lakini msingi wa ushirikiano mpya, mzito zaidi na wa utaratibu. Hiyo ni, ushirikiano wa amani na matunda wa Kanisa na mamlaka ya kiraia na utambuzi sahihi wa mchango wake kwa manufaa ya wote.

Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC
Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC

Maneno haya yaliungwa mkono na Askofu Mkuu wa Kinshasa, Kadinali Fridolin Ambongo Besungu, ambaye akiwa kando ya afla hiyo alitoa maoni yake kwa Vatican News,  kuhusu siku hiyo ya kihistoria kwa Kanisa la Congo DRC iliyotarajiwa kwa zaidi ya miaka sita hivi. Kuanzia wakati huo, kila kitu kitakuwa rahisi kwao  katika nyanja za elimu, afya, masuala ya kijamii, kwa kila jambo wanalofanya kwa ajili ya maskini, kwa kazi zote ambazo wamekuwa wakifanya kwa miaka mingi. Kwa hakika, Kanisa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linafanya mengi kwa ajili ya watu: linasimamia zaidi au chini ya 50% ya shule, kimsingi , shule za msingi na sekondari; katika nyanja ya afya  ambapo ina asilimia 40% ya vituo vya afya.

Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC
Ziara ya Kardinali Parolin nchini Congo DRC

Hadi sasa, hata hivyo, Kanisa lilisajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali (NGO). Lakini Kanisa sio Shirika lisilo la kiserikali  NGO alisisitiza Kiongozi wa Kanisa la Congo na kwamba  halijawahi kujikuta katika  hali hiyo . Kwa kuogezea alisema: “Makubaliano hayo kwa hivyo yanatoa msukumo mpya. Ikiwa tulifanya kazi hapo awali lakini hakuna mtu, kuanzia na askofu katika jimbo lake, alijua nini haki na wajibu wa Kanisa kwa serikali, kuanzia leo mambo ni wazi zaidi. Na tunajua kuwa kazi yote iliyofanywa inafanyika ndani ya sheria inayotambuliwa na serikali”.

04 July 2022, 16:05