Kard.Parolin huko Congo:Nchi ya mgogoro na unyonyaji irudi kuwa ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Uroho wa malighafi, kiu ya pesa na madaraka hufunga milango ya amani na kuwakilisha shambulio la haki ya watu ya kuishi na utulivu. Amani iwe katika nyumba hii! Amani iwe katika ardhi ya Congo, irudi kuwa nyumba ya udugu! Makofi kwa pamoja ya kwaya na zaghroutah, vigeregere vya kawaida vya wanawake wa eneo hilo la kiafika kama utamaduni, viliinuliwa na umati wa waamini zaidi ya 100,000 waliokuwepo kwenye eneo la Bunge la Kinshasa, wakati wa Kadinali Pietro Parolin akitoa wito wake kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inayotishwa kwa miaka na vikundi vyenye silaha na unyonyaji na masilahi ya uporaji. Ni mahali pale pale ambapo Mtakatifu Yohane Paulo II aliadhimisha Misa mnamo mwaka 1980 na 1985, ambapo Katibu wa Vatican Kardinai Pietro Parolini, Dominika tarehe 3 Julai 2022 ameongoza Misa Takatifu ya Ekaristi kwa ajili ya kuombea Amani na Upatanisho wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kama ilivyokuwa ikikumbusha kitambaa kikubwa cha bluu kilichokuwa kimepambwa kuzunguka jukwaa.
Katika siku yake ya pili akiwa barani Afrika, Kadinali Parolin amekumbatia watu wote kwa niaba ya Papa Francisko ambaye hakuweza kwenda lakini ambaye asubuhi hiyo ya Dominika aliadhimisha Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro pamoja na Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma. Akikaribishwa na maaskofu na mapadre wa Kinshasa wa majimbo jirani, kwa nyimbo za ngoma, gitaa la umeme na kwa ngoma nyingine za vikundi vya watoto waliovalia mavazi meupe kwa ajili ya Kupata Komunio ya Kwanza, Kardinali Parolin aliwasili Ikulu kabla ya saa 10 asubuhi, ambapo nje ya jengo alipokelewa na Kadinali Fredolin Ambongo Besungu wa Kinshasa, na watoto wawili, Fred na Trésora, ambao wamesoma barua ikisema: “Karibu kati yetu, Mwadhama". Baadaye walimpatia maua ambayo, kutokana na hisia, za furaha yalianguka chini na ambayo kardinali aliyaokota chini na kurudia kusema mara mbili: "Merci", yaani asante.
Kwa bahati nzuri angani hapakuwapo na joto sana katika msimu huu, japokuwa kulikuwa na harufu kali ya uvumba ambayo ilitawala juu ya majivu ambayo yalieenea Kinshasa yote. Wakati huo eneo la tukio ungeweza kuona majengo mawili ya juu na wakati huo huo mji uliojaa msururu wa magari ya kawaida na vile vile pikipiki. Hata hivyo, anga lilichangamshwa na waamini, kama kawaida wakati wa sherehe za kidini katika maeneo hayo. “Tunamkaribisha Kardinali. Hebu tumwimbie Bwana wetu!” Amepaza sauti kuhani kutoka jukwaani, huku kwaya iliyovalia kanzu nyeupe na njano ikiimba nyimbo kwa Kifaransa na Kibantu, huku wakiyumba na mikono. Kardinali Parolin alikuwa mwishoni mwa msafara mrefu, huku akisalimiana na umati kwa mkono mmoja na mwingine kushikilia msalaba wa mbao. Alisimama na baadhi ya wanawake kwenye viti vya magurudumu waliokuwa wakiinua mikono yao juu; na baadaye aliweza kupita katikati ya watoto ambao walikuwa wakicheza ngoma ya utamadunisho wa misa na kupanda altareni. Alisimama mbele ya sanamu ya Bikira Maria, na baadaye kuanza ibada ya misa Takatifu.
Amani, udugu na furaha yalikuwa ni maneno ya kwanza ambayo Kardinali Parolini alitamka katika mahubiri yake kwa lugha ya kifaransa. Akiendelea alisema “Ni ndoto ambayo tunatamani kukumbatia, lakini ambayo kwa bahati mbaya uzoefu wake ni njia ndogo sana katika nyakati hizi za kukosekana kwa utulivu na migogoro. Hasa hizo ni ahadi za Ufalme wa Mungu zinazotimizwa na ahadi ambazo tunatamani sana ndani yetu. Ndiyo, tunahisi ndani yetu wenyewe kwamba tumeumbwa na kwamba tumekuja ulimwenguni kwa ajili ya amani ambayo si ya muda mfupi tu kati ya vita, kwa ajili ya udugu ambao sio bora lakini wenye ufanisi, kwa furaha iliyojaa na kufurika”. Akiwa ambele ya watu waliojeruhiwa na matatizo kama vile kutokuwepo kabisa kwa ajira, uchafuzi wa mazingira na katika sehemu ya mashariki na vurugu kali, Kadinali Parolin amewahimiza wasikubali ukiwa na kukatishwa tamaa. Kwani amesema kishawishi cha leo hii ni kujisalimisha mbele ya hali halisi, karibu na kujiuzulu kwa bahati mbaya na labda bila kujua, kutoroka katika majukumu ya mtu, kuangukia katika aina fulani za uonevu, kuwaachia wengine mzigo wa kukunja mikono kwa bidii katika kujijenga kwa upya.
Katika hilo Kardinali amesema hapa ni lazima kutenda na kuifanya kwa uhakika kwamba Mungu yuko kazini. Ndiyo, Mungu yuko kazini, amerudia tena kusema katibu wa Vatican. Kwa maana hiyo, upweke, huzuni, kutokuwa na uhakika na kukata tamaa lazima viwekwe kandoni. “Mungu anatuita kutazama wakati ujao: pamoja, umoja, kushinda roho yoyote ya ubaguzi, mgawanyiko wowote wa kikundi, kabila na mali. Pamoja naye, ambaye ni baba na mama, Kardinali Parolin ameendelea, kusema kuwa tunaweza kukabiliana na kesi yoyote, kwa sababu yeye hayuko mbali, lakini anatembea nasi. Nyayo zake hazina kelele, lakini zinafungua njia. Mungu, kila siku ipitayo haiwakilishi jambo lingine la kukatisha tamaa, bali utimilifu wa ahadi yake ya amani”.
Kardinali Parolini aidha ameelekeza mtazamo wake juu ya amani huko mashariki mwa nchi hiyo kwamba, kiukweli amani inatishiwa kila mara na vikundi vyenye silaha na unyonyaji na masilahi ya kikatili, ambayo nchi imekuwa mwathirika wake kwa muda mrefu. Tamaa ya malighafi, kiu ya pesa na madaraka hufunga milango ya amani, na kuwakilisha shambulio la haki ya watu ya kuishi na utulivu. Lakini Yesu anaendelea kututuma sisi wanafunzi wake ili tuweze kurudia maneno yale yale aliyosema: “Amani iwe katika nyumba hii! Amani iwe katika ardhi ya Congo. Irudi kuwa nyumba ya udugu! Na hivyo wito wa Kardinali Parolin ni kwa ajili ya Wakristo kuwa idadi kubwa ya watu na kwa viongozi wote wafanye kazi kwa ajili ya amani katika nchi hiyo, iliyobarikiwa na uzuri wa uumbaji, lakini zaidi ya yote kwa ajili ya utajiri wa roho zinazoijaza.
Kwa niaba ya Papa ambaye ujumbe wake kwa njia ya video ulitolewa mapema kwa wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini ulioneshwa tena kwenye skrini kubwa kabla ya kuanza sherehe ambapo Katibu wa Vatican amewaachia ujumbe wa matumaini kwamba: “Msife moyo, hata kama matarajio yanaonekana kuwa barua iliyokufa kwao. Majina yetu tayari yameandikwa mbinguni, sisi ni watoto wa ufufuko, mashuhuda wa matumaini! Amehitimisha mahubiri yake.