Tafuta

2022.07.03 Kardinali  Pietro Parolin akutana mashirika ya kitawa na watu wanao wahudumia jijini Kinshasa 2022.07.03 Kardinali Pietro Parolin akutana mashirika ya kitawa na watu wanao wahudumia jijini Kinshasa 

Kard.Parolin awafariji maskini,wazee na wagonjwa wa kishasa!

Katika ubalozi wa Vatican huko DRC,Kardinali Prolini alikutana na mashirika ya kitawa mahalia na wasaidizi wao:watoto,wazee,vijana,walemavu au walioachwa na familia zao kwa tuhuma za uchawi.Katibu wa Vatican aliwaletea bembelezo la Papa: “Ninyi ni mfano kwamba upendo,wakati unasambazwa,haumaliziki bali unaongezeka na kukua”.

Na Angella Rwezaula – Vatican

Mara baada ya Misa ya asubuhi, Kardinali Parolin alipaka kutembea kwa mara ya mwisho wa safari katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa wanadamu waliojeruhiwa zaidi. Wazee, watoto, wanawake waseja pamoja na watoto wao, wanandoa, vijana, wote wameunganishwa na dhehebu moja lile la mateso. Kile ambacho huchukua sura ya kukataliwa na unyanyapaa wa kijamii, ugonjwa na ulemavu wa akili, kuachwa, hata na wanafamilia wenyewe. Mateso yanayoponywa wakati fulani kwa upendo tu na bila hata huduma maalum za matibabu, ambayo hukosa, kati ya mambo mengine, rasilimali za kiuchumi za kuwategemeza  na mashirika ya kitawa na ukweli wa kikanisa ambao hufanya kama kivuli kikubwa  cha  kitaasisi. Kwa maana hiyo Kardinali nParolin kati ya aliyokutana nao ni kijana Guy ambaye Watawa walipomkuta nje ya mlango wa nyumba yao siku moja asubuhi miaka mingi iliyopita, mwili wa Guy ulikuwa umefunikwa na nzi na vidonda.  Alikuwa ameachwa mtaani na wazazi wake waliomshtumu kuwa mchawi baada ya ndugu zake wawili kufariki ndani ya siku chache. Alipigwa hadi kufa, maji ya moto yalikuwa yamemwagiwa juu yake; akiwa amepigwa na butwaa, familia ikamtelekeza kando ya barabara.

Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa
Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa

Masista wa Moyo Mtakatifu wa Yesu walimtibu katika kituo cha matibabu. Leo hii Guy anafundisha  lugha ya Kifaransa kwa vijana na anawaomba waombee uongofu wa familia yake. Kwa njia hiyo Dominika tarehe 3 Julai 2022  alikuwa akitabasamu chini ya bembelezo la Kardinali Pietro Parolin aliyekutana naye katika Ubalozi wa  Kitume jijini Kinshasa, pamoja na wawakilishi wa Masharika ya kitawa ya mahalia na wasaidizi wao. Hawa ni wanadamu ambao, Kardinali Parolin alisema, wamepita kutoka kifo hadi uzima, kutoka katika  unyonge hadi utu, kutoka kwa huzuni hadi furaha. Katika muda wote wa mapngo huo, kadinali aliweza  kutoa  mabembelezo na baraka, akiwasalimia wanaume na wanawake kwenye viti vyao vya  magurudumu, akawapigapiga wavulana shavuni wakitazamana kwa macho. Kwa kujibu alipokea nyimbo, shukrani na waridi zambarau, zawadi ya kawaida ya Kihindi iliyowekwa shingoni mwake na Wamisionari wa Upendo. Wao na wawakilishi wengine wa mashirika ya kitawa  waliokezana  kwenye maikrofoni kueleza historia yao ya utumishi wakifuata mfano wa Kristo.

Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa
Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa

Walianza mabinti wa Mtakatifu Yosefu wa Genoni, shirika la  hospitali lililoanzishwa mnamo mwaka wa 1888 huko Sardegna Italia, lenye bidii ya utume katika mabara  manne ambapo  Sr Marie Chimene alizungumza kwa niaba yao na kutoa mfano wa kujitolea kwake kwa watoto wanaojulikana kama watoto wa mitaani ambao, hata hivyo, wanapendelea kuwaita watoto wa Mungu. Wanaenda kuwatafuta katika mitaa yenye vumbi ya mji mkuu, pia kukusanya wavulana waliotelekezwa ambao wanalala chini ya miti. Vijana ambao “hawana tena makao wala familia, kwa sababu wamefukuzwa au kwa sababu nyinginezo ambazo hawatazijua sikuzote, kutokana na mateso makubwa yanayowazuia kuzungumza. Wengine walitekwa nyara na kisha kutelekezwa. wanajaribu kuwapa chakula cha moto cha kawaida, mafunzo ya usafi na elimu ya uraia na wanawafundisha kusali”, alieleza Sista Marie.

Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa
Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa

Na pia kusimulia historia ya Mordekai, aliyeokotwa mitaani saa tano asubuhi na sasa , ana  miaka  14 ambaye ana ndoto ya kuwa rubani, au Marthe na Nathalie, dada wawili wa damu moja  ambao mama yao alipendelea kuwatupa, akiwaacha kando ya barabara. Wale wale ambao wanazurura,  wale wanaotuhumiwa kuwa wachawi labda kwa sababu tu ya kushindwa kutembea kwa usahihi, kwa sababu hiyo  hukataliwa na familia zao.  Wanachukuliwa na Wahudumu wa Hospitali ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambao walianzisha Kituo cha Telema kwa watu hawa ili kuwazuia kula vyakula kutoka kwenye jjalala la uchafu au kukabiliwa na ukatili wa kimwili na unyanyasaji wa kijinsia. Guy ni mmoja wa wageni hao; pamoja naye pia Joséphine, ambaye aliishia kuishi mtaani bila kuoga kwa miaka mingi, akivaa nguo zilizochanika, akijilisha chakula kutoka katika mapipa ya takataka.  Kwa maana hiyo Siku moja, sisita wao  alikutana naye, akampeleka kwenye jumuiya yao  iitwayo Betania, akamtunza na kumpeleka kituo cha  Telema. Mwezi mmoja baadaye, alikuwa na tabasamu lake tena, na hadhi yake. Miezi mitatu baadaye alirudishwa tena katika familia yake,  na sasa ana biashara ndogo  anayojishughulisha nayo.

Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa
Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa

Hatimaye, wawakilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio walimweleza Kardinali Parolin kuhusu Moango wa  Dream kwa wagonjwa wa VVU. Shukrani kwa kituo cha usaidizi, kilichoanzishwa  mnamo mwaka wa 2011, zaidi ya watu 1,700 wanaosumbuliwa na UKIMWI, lakini pia kutokana na utapiamlo, shinikizo la damu, kisukari, malaria, kifua kikuu wanatibiwa bila malipo. Wakati wa janga la UVIKO , Kituo kilibaki wazi na maabara yake kutumika kugundua virusi au kukusanya sampuli. Wafanyakazi wa kujitolea kwa sasa wanashirikiana na wafanyakazi wa afya katika kampeni pana ya uhamasishaji na chanjo katika masoko, bandari, vituo vya afya.

Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa
Kardinali Parolin akiwa na wageni wa Watawa wanaowahudumia huko Kinshasa

Kwa watu hawa wote, Kardinali Parolin, akizungumza kwa hisia inayoonekana, alihakikisha kuwa kwa  hakika atapeleka  majina yao  na nyuso zao  kwa Papa Francisko, akimwomba awaweke katika sala zake,  huku akimshukuru Mungu kwa maajabu aliyowatendea.  Aidha alisema Kanisa la ulimwengu wote linawashukuru na linawahimiza kudumu katika kazi zao, hata kwa gharama ya matatizo na kushindwa dhahiri. Katika maisha yao ya kila siku wanapata uzoefu jinsi upendo, wakati unasambazwa, haugawanyi au kumalizika, lakini huzidisha na kuku. “Majina yenu yanasikika kama noti nyingi nzuri za muziki katika wimbo wa shukrani ambazo ni lazima tuwasilishe kwa Mungu kila siku, aliongeza kardinali. Wakati tu ulifikiria yote yanaweza kupotea, mwanga na maisha inaibuka katika maumivu na kubadilisha kila kitu. Bila shaka, si kila kitu ni cha kupendeza na bado wanapaswa kukabiliana na nyakati ngumu, labda wasiwasi na hofu nyingi za ziku zijazo. Lakini Mungu amewafungulia kila mmoja wao njia mpya, amewarudisha kwa miguu yenu na kuwaalika muendelee kutembea naye, amewaonesha mkono, wasiuache”.

04 July 2022, 16:23