Tafuta

Askofu mkuu Nicola Girasoli, Balozi mpya wa Vatican nchini Slovakia. Askofu mkuu Nicola Girasoli, Balozi mpya wa Vatican nchini Slovakia. 

Askofu mkuu Nicola Girasoli Balozi mpya wa Vatican nchini Slovakia

Askofu mkuu Nicola Girasoli alizaliwa tarehe 21 Julai 1957, nchini Italia. Baada ya majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 15 Juni 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 2006 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 11 Machi 2006 na hapo akatumwa kwenda kuwa Balozi wa Vatican nchini Malawi na Zambia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Nicola Girasoli, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Slovakia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Girasoli alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Perù. Amewahi pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini: Trinidas, Tobago, Barbuda, Bahamas, Barbados, Dominica, Jamaica, Guyana, Grenada St. Kitts, Nevis, St. Lucia, St. Vincent Grenadine, Saints Kitts & Nevis, Suriname pamoja na kuwa ni Mwakilishi wa kitume huko kwenye Visiwa vya Antille.

Askofu mkuu Nicola Girasoli, Balozi wa Vatican nchini Slovakia
Askofu mkuu Nicola Girasoli, Balozi wa Vatican nchini Slovakia

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Nicola Girasoli alizaliwa kunako tarehe 21 Julai 1957, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 15 Juni 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 2006 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 11 Machi 2006 na hapo akatumwa kwenda kuwa Balozi wa Vatican nchini Malawi na Zambia. Tarehe 16 Juni 2017 Papa Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Perù na hatimaye, tarehe 2 Julai 2022 akamteuwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Slovakia.

Uteuzi Slovakia
02 July 2022, 16:49