Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Joseph Spiteri kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Mexico. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Joseph Spiteri kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Mexico.  

Askofu Mkuu Joseph Spiteri, Balozi Mpya wa Vatican Nchini Mexico

Askofu mkuu Joseph Spiteri alizaliwa tarehe 20 Mei 1959 huko mjini Sliem, Kisiwani Malta. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 29 Juni 1984 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 21 Februari 2009, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Sri Lanka na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu 24 Mei 2009.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Joseph Spiteri kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Mexico. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Joseph Spiteri alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Lebanon. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Joseph Spiteri alizaliwa tarehe 20 Mei 1959 huko mjini Sliem, Kisiwani Malta. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 29 Juni 1984 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 21 Februari 2009, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Sri Lanka na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa ni Askofu mkuu.

Askofu mkuu Joseph Spiteri, Balozi mpya wa Vatican nchini Mexico
Askofu mkuu Joseph Spiteri, Balozi mpya wa Vatican nchini Mexico

Aliwekwa wakfu kama Askofu mkuu kwa ajili ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu tarehe 24 Mei 2009. Ibada hii iliongozwa na Kardinali Tarcisio Pietro Evasio Bertone, Katibu mkuu mstaafu wa Vatican. Ilipogota tarehe 1 Oktoba 2013, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Pwani ya Pembe “Ivory Coast.” Ilikuwa ni tarehe 7 Machi 2018, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Lebanon. Na hatimaye, tarehe 7 Julai 2022, Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena, amemteuwa Askofu mkuu Joseph Spiteri kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Mexico.

Uteuzi Mexico
08 July 2022, 14:35