Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Ephrem Ndjoni kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Franceville, lililoko nchini Gabon. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Ephrem Ndjoni kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Franceville, lililoko nchini Gabon.  

Askofu Ephrem Ndjoni Jimbo Katoliki la Franceville, Gabon.

Askofu mteule Ephrem Ndjoni wa Jimbo Katoliki la Franceville alizaliwa tarehe 11 Februari 1973 huko Moanda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 6 Julai 2003 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Katika maisha na utume wake kama Padre, kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2004 alitumwa kwenda Roma kwa masomo ya juu katika Sayansi ya Maandiko Matakatifu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Ephrem Ndjoni kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Franceville, lililoko nchini Gabon. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule Ephrem Ndjoni alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Kanisa kuu la Mtakatifu Hilaria “Saint Hilaire.” Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Ephrem Ndjoni wa Jimbo Katoliki la Franceville alizaliwa tarehe 11 Februari 1973 huko Moanda. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 6 Julai 2003 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Katika maisha na utume wake kama Padre, kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2004 alitumwa kwenda Roma kwa masomo ya juu katika Sayansi ya Maandiko Matakatifu, kwenye Taasisi ya Biblia, Biblicum na baadaye kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2011 akajiendeleza zaidi kwenye Chuo Kikuu cha Biblia cha Wafranciskan, “Biblicum Franciscanum” kilichoko mjini Yerusalemu.

Papa Francisko amemteuwa Mons. Ndjoni kuwa Askofu wa Franceville.
Papa Francisko amemteuwa Mons. Ndjoni kuwa Askofu wa Franceville.

Na huko hatimaye, akatunukiwa Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Maandiko Matakatifu na baadaye kati ya mwaka 2012 hadi mwaka 2016 alipambana kiume na hatimaye akatunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu ya Maandiko Matakatifu. Kunako mwaka 2016 akarejea jimboni mwake na kuteuliwa kuwa Paroko wa Kanisa kuu la Mtakatifu Hilaria “Saint Hilaire” Jimbo Katoliki la Franceville. Aliteuliwa pia kuendelea kufundisha Sayansi ya Maandiko Matakatifu kwenye Seminari kuu ya Mtakatifu Augustin huko Libreville “Saint Augustin in Libreville.” Alikuwa ni Mratibu wa Utume wa Biblia Kitaifa, Mjumbe wa Kamati ya Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Baraza la Maaskofu Katoliki Gabon pamoja na kuwa ni mwakilishi wa Kanisa Katoliki katika Baraza la Taifa la Uchumi, Jamii na Mazingira, “Conseil Économique, Social et Environnemental (CESE).

Uteuzi Gabon
25 July 2022, 15:18