Tafuta

Bi Ursula Von Der Leyen  Rais wa Tume ya Ulaya. Bi Ursula Von Der Leyen Rais wa Tume ya Ulaya.  

Von Der Leyen,Vatican:tumechafua na kutupa,tuboreshe maisha ya watu!

Rais wa Tume ya Ulaya, yuko Roma kwa ajili ya Tamasha Kuhusu Bauhaus Mpya ya Ulaya, alifungua kazi katika eneo la Casina Pio IV mkutano wa Kujenga kwa upya Mustakabali wa Watu na Sayari,ulioandaliwa na Chuo cha Kipapa cha Sayansi na Bauhaus Earth.Kwa mujibu wake amesema Papa ana sababu kwani wanadamu hawatakiwi kuzamishwa kwenye zege.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ubinadamu bado una uwezo wa kufanya kazi pamoja kujenga nyumba yetu ya pamoja. Ni wakati wa kuunganisha familia nzima ya kibinadamu. Kwa sababu tunajua kuwa mambo yanaweza kubadilika. Nimaneno ya hotuba ya Bi Ursula von Der Leyen, Rais wa Tume ya Ulaya akimnukuu maneno ya Papa Francisko ya  Waraka wake wa  'Laudato si',  wakati wa kutoa hotuba yake katika makao ya Chuo cha Kipapa cha Sayansi huko Casina Pio IV, ambapo mkutano kuhusu  “Kujenga Upya kwa Watu na Sayari” ulifanyika Alhamaisi 9 Juni 2022 asubuhi, ulioandaliwa na  Chuo cha Sayansi na  Bauhaus Dunia.

Rais wa Tume ya Ulaya alizindua toleo la kwanza la Tamasha la Ulaya Mpya ya Bauhaus Dunia ambao ni mpango  unaolenga kuharakisha mabadiliko ya sekta mbalimbali za kiuchumi, kama vile sekta ya ujenzi na nguo, ili kuhakikisha upatikanaji wa mali ya mzunguko kwa wote,  wananchi na kupunguza kiwango cha hewa chafuzi. Akiwa katika  Bustani za Vatican  alisema, kwamba kujitolea kwa sayansi na maendeleo kunakutana na kujitolea kwa maadili. Hotuba ya Bi Von der Leyen ijihusisha na  mambo miwili: kwa upande mmoja, utafutaji wa suluhisho zilizotokana na mabadiliko ya tabianchi; kwa upande mwingine, mchango madhubuti katika kuboresha maisha ya watu kwa jinsi tunavyobuni na kujenga nyumba na miji. Kuna kanuni tatu zilizooneshwa na kiongozi wa Ulaya ambazo ni uendelevu, uzuri, ushiriki.

"Uendelevu ambao naonatia shaka wajibu wa kila mwanadamu kuhifadhi viumbe, kuvitunza na hivyo kuvipitishia vizazi vijavyo. Kwa muda mrefu sana, ubinadamu umesahau jukumu hili. Kizazi baada ya kizazi kimenyonya maumbile nje ya mipaka ya sayari yetu. Tumechukua, kuchafuliwa, na kutupwa. Na hiyo lazima ikome” alisema Bi von Der Leyen. Kinachohitajika ni mfano mpya, ambao unarudi kwa asili badala ya kuiondoa. Kimsingi, hii ni Mkataba wa Kijani wa Ulaya, mpango unaofikia mbali wa kufanya Ulaya kuwa bara la kwanza lisilo matatizo ya tabianchi ifikapo 2050, alisisitiza kiongozi huyo.

Katika ufunguzi wa kazi ya mkutano huo  chini ya uenyekiti wa Rais Joachim von Braun, uliwaleta pamoja wanasayansi, ulimwengu,  wasanii wa majengo mashuhuri, wapangaji ardhi na watunga sera. Lengo ni kujadili mabadiliko ya mazingira: kutoka katika injini ya migogoro ya hali ya hewa na kijamii hadi nguvu ya kuzaliwa upya kwa sayari. Kikao hicho kilifunguliwa kwa salamu kutoka kwa Kansela Mkuu, Kadinali Peter Appiah Turkson,  ambapo baadaye  kati ya wengine  kulikuwapo na  Francis Kéré, mbunifu kutoka Burkina Faso lakini anayefanya kazi huko Berlin, mshindi wa Tuzo ya Pritzker ya mwaka huu 2022, ambaye alizungumza juu ya uendelevu, usanifu, na Hans Joachim Schellnhuber, mwanzilishi wa Bauhaus Earth na msomi wa PAS, ambaye alisisitizia  umuhimu wa sekta ya ujenzi katika mabadiliko ya kijani.

Kusudi ni la kutamani, lakini linawezekana kwamba  Ulaya inaweza kuonesha kuwa inawezekana kuunda uchumi wa mzunguko ambao unathamini asili na afya ya binadamu. Kwamba hakuna maelewano kati ya ukuaji wa uchumi na upunguzaji wa hewa ya ukaa. Na kwamba jamii zetu zinaweza kustawi bila kuweka vizazi vijavyo hatarini. Mojawapo ya mikakati ya kwanza iliyowasilishwa ni wimbi la uboreshaji, linaloungwa mkono na euro bilioni 53 na mpango wa kuzindua tena, NextGenerationEU. “Tunahitaji kurudisha asili katika miji yetu,” von Der Leyen alisema, akitoa mfano wa Seville, ambapo Tume ya Ulaya imetoa mwanga wa kijani kwa jengo jipya litakalohifadhi zaidi ya wanasayansi 400 wa kimataifa na halitaegemea upande wowote kutoka katika mtazamo wa utoaji wa hewa ya ukaa, lakini pia chanya kutoka kwa mtazamo wa nishati. “Jengo ambalo linarudisha zaidi kuliko inavyohitajika. Hii ndio nguvu ya uvumbuzi wa kijani kibichi”.

Pamoja na utendaji wa kuzingatia lakini, lakini pia uzuri. Kile ambacho binadamu wanahitaji uzuri ili kustawi. Uzuri ulimaanisha ubora wa maisha. Bi Ursula von Der Leyen alisema kuwa Papa Francisko yuko sahihi anaposema kwamba wanadamu hawajaumbwa kuzamishwa kwenye zege na chuma. Kujenga zaidi kwa vipengele vya asili, kama vile miti, ni vizuri kwa sayari na ustawi wa watu”. Mkataba wa Kijani wa Ulaya utafanikiwa tu kwa ushiriki wa kila mtu. Bauhaus Mpya ya Ulaya inatoa mfumo mzuri wa hii, na hatimaye alihitimisha rais wa Tume ya Ulaya, akiorodhesha baadhi ya mipango mpya iliyozinduliwa shuleni, kufanya majengo kuwa endelevu zaidi, lakini pia bora kwa wanafunzi na walimu, au katika Jamhuri ya Czech, ambapo raia na wasanifu wanashughulikia dhana ya kubadilisha jiji zima kuwa mahali pazuri pa kuishi.

10 June 2022, 09:42