Tafuta

Matazamo wa mbali wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Matazamo wa mbali wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro 

Vipindi 4 vilivyowekwa kwa ajili ya Mtume Petro katika Kanisa Kuu

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,baada ya “safari za Maria” zilizowekwa kwa ajili ya Mama Yetu mnamo mwezi Mei,tukio jipya litakuwapi mwezi wa Juni na matukio manne yaliyowekwa kwa ajili ya Mtume Petro.

Vatican News

Utajiri wa marejeo ya Mtakatifu Petro katika Kanisa Kuu ni kwamba  ni muhumu kufanya vituo vya sala hii ya msafiri ambavyo   vinaweza kubadilishwa mara kwa mara, ambavyo vinakusudiwa kuwa “safari ya kiroho", iliyo wazi kwa wote, kama mwaliko wa kutafakari, kupitia uzuri wa kisanii wa Kanisa Kuu (Basilika), haiba na uzuri wa maana na mafundisho ya Kikristo yaliyomo ndani ya picha hizo. Ratiba hizo zinaanzia kwenye ukumbi wa Kanisa Kuu na kuishia kuungama kila Jumatano alasiri, kuanzia tarehe 8 Juni  hadi Juni 29, ikijumuisha Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo, kuanzia saa 10.00 hadi saa 11.00 jioni, zikiishia karibu na adhimisho la mahali Patakatifu, Misa itakayoadhimishwa kwenye Altare ya Kanisa Kuu.

Imani na sanaa

Kanisa Kuu la ka Kipapa la Mtakatifu Pietro ni Kanisa ambalo mahujaji hupata mahali pa kutua baada ya kuwasili kutoka kila kona ya dunia. Kanisa hilo limeinuka kuzungukia kaburi la mtume Petro, huku likikumbatiwa na nguzo ya Bernini, katika fahari yake ya usanifu, linakaribisha kila mtu katika kukumbatia kwake  na kujumuisha. Maisha ya kiliturujia ya Kanisa Kuu  humruhusu mhujaji kwa hakika kushiriki kila siku katika siku za Juma na sherehe mbali mbali za siku kuu sherehe zinazoadhimisha katika siku hiyo. Kwa kuzama katika hali hiy, Kanisa kuu la Mtakatifu Petro linaendelea kuwa tunda la kazi ya binadamu na uhifadhi wa kazi adhimu za sanaa zinazoshuhudia na kusimulia taaluma za imani ya Mtakatifu Petro ambazo Baba Mtakatifu Francisko alizieleza kwa maneno haya: "kwa sababu alikuwa mtu imara na wa kutegemewa. Alifanya makosa mengi, hadi kufikia hata kumkana Mwalimu wake. Lakini alichagua kujenga maisha yake juu ya Yesu. Maandiko hayasemi kuhusu mwili na damu, yaani, kuhusu yeye mwenyewe, kuhusu uwezo wake, lakini juu ya Yesu. Yesu ndiye mwamba ambao Simoni alifanyika jiwe”.

Taarifa muhimu

Wanakumbusha kuwa ili  kuingia katika Kanisa Kuu la  Mtakatifu Petro kunaruhusiwa tu kwa wageni ambao wamevaa nguo zenye heshima. Kiingilio ni bure, na kama vile huduma ya chumba cha kuhifadhia vitu.Kabla ya kuingia kwenye Kanisa Kuu la  Vatikani, wageni wanatakiwa kuweka kwenye chumba cha kuhfadhia, viti vya watoto, mizigo, masanduku, begi za mgongoni, vifurushi na vitu ambavyo kwa ukubwa wake na sifa zake  havistahili kuingizwa katika Kanisa Kuu  kwa mujibu wa wafanyakazi wanaohusika

09 June 2022, 17:59