Tafuta

Vita nchini Ukraine vina hatari ya kukosekana kwa ngano katika mataifa yanayotegemea mazao yake ya kilimo kama cha ngano Vita nchini Ukraine vina hatari ya kukosekana kwa ngano katika mataifa yanayotegemea mazao yake ya kilimo kama cha ngano 

Vatican kwa FAO:vita na ukosefu wa usalama wa vyakula vinahatarisha janga ulimwenguni

Katika hotuba yaMwakilishi wa Kudumu wa Vatican Monsinyo Arelano kwenye kikao cha 170 cha Baraza la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Chakula na Kilimo(FAO)amebainisha wito wa Baba Mtakatifu kuhusu amani na mazungumzo na kuzindua kwa upya wito juu ya ukosefu wa usalama wa vyakula kwamba vizingiti vya kupeleka ngano vinahatarisha maisha ya mamilioni ya watu.Inahitaji kufanya kazi pamoja ili mkate upatikane kwa wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumuiya ya kimataifa imejitolea kwa dhati kukomesha uvamizi wa kijeshi nchini Ukraine mara moja. Hili ni ombi la Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika la Kikao cha 170 cha Baraza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kilichofunguliwa tarehe 14 Juni  mjini Roma na kitamalizika tarehe 17 Juni 2022. Katika hotuba iliyotolew, katika  mazungumzo kuhusu “Athari za mzozo wa Ukraine na Urussi katika usalama wa chakula duniani na masuala yanayohusiana nayo, Monsinyo Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa Kudumu katika  Baraza Kuu  FAO, IFAD na WFP, alisisitiza kama jinsi ambavyo  Baba Mtakatifu Francisko amesihi mara kadhaa kwa moyo wenye uchungu, kwamba “mauaji hayo ya kikatili yakomeshwe, silaha zinyamazishwe na mchakato wa mazungumzo mazito yatawale, njia pekee yenye hadhi ya kutoka kwenye mzunguko wa vita, ambavyo vinaleta ghadhabu ya umwagaji damu na hatari”.

FAO imekuwa bega kwa bega kusaidia tangu baada ya vita kuu ya Pili ya dunia

Hata hivyo Monsinyo Arellano pia alionesha hata wasiwasi kuhusu suala la usalama wa chakula linahusishwa kwa karibu na amani na vikwazo ambavyo Ukraine inakumbana navyo katika kusafirisha ngano nje ya nchi vinasababisha wasiwasi mkubwa, pamoja na kuleta matatizo kwa nchi zinazotegemea mahitaji ya Ukraine. Kilicho hatarini ni maisha ya mamilioni ya watu, haki ya binadamu ya kupata chakula kwa wote na utulivu wa maeneo makubwa ya sayari, alisema Mwakilishi wa Kudumu, huku akisisitiza kwa upya wito uliozinduliwa na Papa kwenye Katekesi yake mnamo tarehe 1 Juni iliyopita, ya kutotumia ngano kama silaha ya vita. Monsinyo Arellano amekumbusha kwamba FAO ilizaliwa mwishoni mwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ili kukomesha uharibifu unaosababishwa na migogoro, kwa kufahamu kwamba ukosefu wa chakula, muhimu kwa maisha ya binadamu, umekuwa sababu kuu ya kukosekana kwa utulivu, machafuko na maasi yanayopendwa na watu wengi.

Kufanya kazi pamoja na haraka ili watu wapate mkate

Kwa hiyo Mwakilisho huo alisisitiza kuwa ni muhimu kufanya kazi pamoja na kutenda kwa usahihi na uharaka na dhamira ili kuwe na mkate kwa ajili ya kila mtu na kuepuka kuwa mbaya zaidi ya hali tete sana ambayo imetokea. Katika nchi maskini zaidi, ambazo tayari zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya tabianchi na uhaba wa maji, ukosefu wa mbolea unaweza kuchochea kushuka kwa uzalishaji, na hatari ya kupunguza idadi ya watu wote kwenye uharibifu na utapiamlo, ambayo inatoa mwaliko wa kukabiliana kwa haraka na kwa busara, athari zenye madhara za mzozo wa chakula unaoendelea, unaochochewa zaidi na mapigano ya silaha katika maeneo yaliyo hatarini zaidi duniani. Kwa kuzingatia, ongezeko la bei za vyakula, lazima pia izingatiwe kwamba ukosefu wa chakula, ifikapo 2023, unaweza kusababisha janga la kimataifa.

FAO inachukua hatua madhubuti

FAO lazima itoe mchango wake wa kuona mbali ili kujibu kwa ujasiri changamoto ngumu zinazotungoja, kwenda kwenye mzizi wa tatizo, kufanya mipango madhubuti na kutafuta manufaa ya wote ni mwaliko wa Monsinyo Arellano, ambaye amehimiza kufanya mengi zaidi kwa sababu wale wanaopatwa na matokeo ya vita wanahisi kwamba wanasaidiwa kiukweli. Mwakilishi wa kudumu wa Vatican aliongezea kwamba uchungu wa ndugu na dada wengi hutulazimisha na kututia moyo kujenga amani, kuiheshimu na kuitoa kuwa zawadi bora zaidi. Na amesisitiza kwamba suluhisho la tatizo la sasa haliko katika nguvu za kijeshi, jambo ambalo linaweza kusababisha ongezeko la hila zaidi kwa kila mtu, bali ni kuachana na maslahi ya upande mmoja, ili hali ya chuki na kifo ambayo watu wako wanakumbana nayo, na kwa ushirikiano kwa ajili ya utunzaji wa dunia.

15 June 2022, 17:26