Tafuta

Wahamiaji ni kaka na dada waheshimiwe. Wahamiaji ni kaka na dada waheshimiwe. 

Vatican:Wahamiaji ni kaka na dada na sio idadi,wahemiwe hadhi yao!

Wahamiaji wana wajibu wa kuheshimu maadili,mila na sheria za jumuiya ambayo inawackaribisha,na jumuiya zinazowapokea zinaitwa kutambua mchango wa manufaa ambao kila mhamiaji anaweza kuutoa kwa jamii nzima.Amesema hayo Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Makao ya Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Mataifa huko Geneva.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Vatican kwa mara nyingine tena imesisitiza kwamba haki  msingi za binadamu na hadhi ya  wahamiaji lazima zilindwe zaidi ya mazingatio yoyote ya kisiasa, na kulaani vitendo vya kusukuma nyuma vinavyofanywa na nchi kadhaa. Akizungumza siku ya Ijumaa tarehe 24 Juni 2022 kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu, Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika makao ya  Umoja wa Mataifa huko Geneva, alisema kwamba mazoea kama hayo mara nyingi hupuuza hata fikira za msingi za kibinadamu, na kushindwa kuhakikisha usalama na hadhi ya wahamiaji.

Hatupaswi kusahau wahamiaji kuwa sio idadi ni kaka na dada zetu

Askofu Mkuu Nwachukwu alisema “Hatupaswi kamwe kusahau kwamba wahamiaji sio idadi tu, lakini dada na kaka zetu ambao hawawezi kuachwa nyuma. Mwakilishi wa Vatican alikumbuka vitenzi vinne muhimu vilivyopendekezwa na Papa Francisko  kushughulikia changamoto zinazoletwa na uhamiaji wa kisasa ambavyo ni ukaribu, kulinda, kuhamasisha na kufungamanisha”.

Wahamiaji wana jukumu la kuheshimu maadili ya wanaowapokea

Katika suala hilo, alikiri kwamba ushirikiano ni mchakato wa pande mbili kwa sababu “Wahamiaji wana jukumu la kuheshimu maadili, tamaduni na sheria za jumuiya ambayo imewakaribisha  lakini vile vile na jumuiya zinazowapokea zinaitwa kutambua mchango wa manufaa ambao kila mhamiaji anaweza kutoa kwa jamii nzima.”

Kupanua njia mbadala za uhamiaji salama

Askofu Mkuu Nwachukwu alisisitiza umuhimu wa kupanua idadi na njia mbadala za uhamiaji salama, wa kawaida, na wa hiari na makazi mapya, kwa heshima kamili ya kanuni ya kutorejeshwa kwenye mataifa yao. Lengo kuu la juhudi za kimataifa katika muktadha wa uhamiaji linapaswa kuhakikisha kuwa uhamiaji ni salama, halali na wa utaratibu.  Askofu Mkuu akizungumzia hasa mazoezi ya hivi karibuni ya  kusumbua ya uhamishaji wa nje wa taratibu za hifadhi na urasimu, kwa wakala, jukumu la kupokea wahamiaji wapya wanaowasili. Alihitimisha taarifa yake akikumbuka ombi la hivi karibuni la Papa Francisko la kuacha kupitisha suala la uhamiaji kwa wengine, kana kwamba halijalishi mtu yeyote na ni mzigo usio na maana wa kubebwa na mtu mwingine.

HOTUBA ZA MWAKILISHI WA KUDUMU WA VATICAN KATIKA UN HUKO GENEVA
26 June 2022, 11:13